Barua ya wazi kwa Zitto Kabwe: Sisi Watanganyika nani atatusemea

Barua ya wazi kwa Zitto Kabwe: Sisi Watanganyika nani atatusemea

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Mheshimiwa Zitto:
Siku hizi Nchi inakopa na sehemu kubwa ya mikopo(Kiuwiano) inakwenda Zanzibar.
Nchi ya watu chini ya milioni mbili inapewa zaidi ya 25% ya mikopo ambayo Jamhuri ya muungano wa Tanzania inakopa.
Na tunajua sehemu kubwa ya hilo deni itakuja kulipwa na Watanganyika kwa sababu kiukweli uchumi wa Zanzibar hauna uwezo wa kuhimili hilo deni.

Sisi Watanganyika hatuna shida na Wazanzibar kunufaika na mikopo lakini tunachosema ni mambo mawili
1. Kama mkopo ni wa Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, basi siyo haki nchi ya watu milion 1.5 wapewe 25% ya pesa, halafu watu milion 50 waliobaki wapewe kilichobaki wakati at the end of the day mkopo wote kwa kiasi kikubwa utalipwa na watu hawa milioni 50

2. Lakini kama Mkopo unaokwenda Zanzibar ni mkopo makhsusi uliokopwa na SMZ ila tu kwa kupitia udhamini wa JMT ni jambo la kheri isipokuwa tunaamini kabisa Zanzibar haina uwezo wa kiuchumi wa kulipa mikopo hiyo mikubwa sana relative na pato lao, kwa hiyo hapa napo ni dhahiri haya madeni tutayabeba sisi Watanganyika.

Ndugu Zitto :
Sisi tunajua, ACT ni pro Zanzibar, maana huwa inazungumzia maslahi ya Zanzibar kuliko Tanganyika katika muungano, lakini tunataka muelewe kuwa huu ukimya wetu sisi Watanganyika msiuchukulie kama uzuzu.

1. Tunajua 21% ya ajira za Muungano zinaenda kwa Wazanzibar(at least kwenye makubaliano) na tuliona waziri aliyekuwa na dhamana na utumiashi aliyebadilishwa ndugu Mchegerwa akilisimamia hilo

2. Tunajua kodi zote zinazokusanywa huko Zanzibar hata za TRA zinabaki hukohuko Zanzibar.

3. Tunajua kuwa Watanganyika mara kibao wamefinance uendeshaji wa serikali ya SMZ ikiwemo kulipa mishahara

Lakini at the same time wazanzibar wanaendelea kucomplain na kucomplain tu, Sasa ndugu Zitto Kiongozi wa chama, unatueleza nini sisi Watanganyika katika hili suala?

Wakati wa Magufuli mlipiga kelele sana alivyokuwa anaipendelea Chato, Sasa mbona mko kimya kwa namna Samia anavyoipendelea Zanzibar waziwazi?

Ninajua kuwa kuna hoja kuwa Zanzibar inaidai Serikali ya muungano pesa nyingi, well hata kama ni kweli, lakini hii haijustify upendeleo huu wa kimikopo, lazima itafutwe arrangement ya kusolve hiyo issue lakini siyo arrangement hii ya kuumiza upande mmoja.

Ndugu Zitto, sisi Watanganyika unatusemeaje na unatusemea wapi manung'uniko yetu?
 
Bila ya 'vurugu zetu' wa Tanganyika tusingekuwa na Rais kutoka Znz hivi sasa

Bila ya 'vurugu zetu' Wanaume tusingekuwa na Rais Mwanamke mapema sana

Hvi wakati JPM anafariki kulikuwa na Mawaziri wangapi (Full minister) kutoka Znz kwny cabinet yake?


Vita ya kunguru…
 
Kelele nyingi za wazanzibar kuhusu muungano wa Nyerere na Karume ni danganya toto kuwazubaisha wadanganyika kuwa wao ndo wenye kufaidika na muungano lakini nyuma ya pazia wao ndo wanufaika wakubwa kuanzia kwenye ardhi ya bara,ajira nk
 
Wenye dhamana ya kutusemea watanganyika ni watu wawili. Makamu wa Rais Dr. Philip Mpango na waziri ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dr. Sulemani Jafo ila wamekaa kimya.
 
Kelele nyingi za wazanzibar kuhusu muungano wa Nyerere na Karume ni danganya toto kuwazubaisha wadanganyika kuwa wao ndo wenye kufaidika na muungano lakini nyuma ya pazia wao ndo wanufaika wakubwa kuanzia kwenye ardhi ya bara,ajira nk
Uko sahihi
Hawa wanaweza kumiliki ardhi Tanganyika ila mtanganyika kumiliki ardhi Zenji haruhusiwi labda aende kama mwekezaji

Pia Wazenji wana haki ya kuomba na kupata ajira kwa Mambo yote ya Tanganyika yasiyo ya muungano, ila huko Zenji ajira za SMZ ni Wazanzibar tu
 
Tanganyika ndo imeiweka Zanzibar mateka. Msilie maana Wazanzibari wamelilia uhuru wao miaka na miaka.

Tanganyika isione gharama kuilisha na kubeba mzigo wa kiuchumi itokanayo na muungano.

Wazanzibari na CHADEMA wameipigia kelele suala la muungano na kupendejeza uundwaji wa serikali tatu ila majitu majinga CCM wameamua iwe hivyo.

Basi hakuna sababu ya Tanganyika kulalamika
 
Kutokana na matatizo hayo, kwanini tena wakubwa wa Tanganyika wanaung'ang'ania na kuahidi kuulinda kwa nguvu zote za dola?
 
Mkuu nakuona unatumia nguvu zako kumpigia mbuzi guitar ukiamini atacheza mziki na kukushukuru.

Zitto ni mtu wa kucheza na fursa kama hizi hasa za kujioendekeza kwa watawala ili aendelee kupata mkate wake wa kila siku.
 
Bila ya 'vurugu zetu' wa Tanganyika tusingekuwa na Rais kutoka Znz hivi sasa

Bila ya 'vurugu zetu' Wanaume tusingekuwa na Rais Mwanamke mapema sana

Hvi wakati JPM anafariki kulikuwa na Mawaziri wangapi (Full minister) kutoka Znz kwny cabinet yake?


Vita ya kunguru…
Kilichomuweka rais mwana mama hapa nchini ni kwa mujibu wa katiba ya JMT hapo wala usitoe lawama upande wowote.
 
Bila ya 'vurugu zetu' wa Tanganyika tusingekuwa na Rais kutoka Znz hivi sasa

Bila ya 'vurugu zetu' Wanaume tusingekuwa na Rais Mwanamke mapema sana

Hvi wakati JPM anafariki kulikuwa na Mawaziri wangapi (Full minister) kutoka Znz kwny cabinet yake?


Vita ya kunguru…

Kama ni huyo JPM unamtetea kubaki madarakani, ni bora kuongozwa kila ngazi na wanawake wa kizanzibari. Hututaki kutawaliwa na mtu mnyama bila ridhaa yetu.
 
Back
Top Bottom