Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,897
Nimetafutwa na uongozi wa JamiiForums ili kutoa maelezo kuhusu barua iliyowekwa jukwaani inayoonyesha kuwa ndani ya chama kuna kutoelewana kuhusiana na msimamo juu ya kesi inayomkabili mmoja wa viongozi waandamizi wa chama Ndg. Wilfred Lwakatare, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama.

Maelezo yangu ni kama ifuatavyo:

1. Niliandika barua kwa Katibu Mkuu wa chama mnamo tarehe 15 Machi 2013 kutaka chama kifanye uchunguzi wake wa ndani kuhusiana na ukweli wa video iliyowekwa kwenye mitandao inayoonyesha kuwa Kiongozi wetu mwandamizi anapanga mipango ya kumdhuru Mhariri wa moja ya magazeti hapa nchini​. Sikuamini kabisa mambo yale na hivyo kutoa ushauri kwa chama kwamba tufanye uchunguzi wetu wa ndani ili kujiridhisha. Uchunguzi wa ndani ungetufanya kuweka mikakati wa namna bora zaidi ya kulinda chama dhidi ya njama zozote, za ndani au za nje ya chama.

2. Mapendekezo yangu ndani ya chama kamwe hayakulenga kumtosa ndugu Lwakatare wakati huu anakabiliwa na changamoto hii bali yalilenga kuhakikisha kuwa wakati tunamlinda na kumtetea ili haki itendeke, lazima tuhakikishe kuwa chama hakitaathirika na sakata hili kwa namna yeyote ile. Ni jukumu letu kuhakikisha sura (image) ya chama inabakia salama maana hatujui mikakati (game plan) ya maadui zetu kisiasa hasa baada ya kauli zao kwamba chama kitakufa kabla ya 2015 ambayo imerudiwa rudiwa sana. Ni lazima kutilia shaka (doubt) kila linalotokea sasa kwa kulipima kwa jicho la mbele zaidi. Ikumbukwe maneno ya Mwenyekiti wetu "Mwenyekiti Freeman Mbowe anataka ikithibitika kuwa Lwakatare alishiriki kurekodi mkanda huo iwe kwa kurubuniwa, ‘kushikishwa' au kuingizwa mkenge, itamlazimu kuwajibika kwa kosa la kukosa umakini" (Gazeti la Jamhuri).

3. Barua ile ya tarehe 15 Machi 2013 ilikuwa ni ya ndani ya chama, haikuwa ya kiofisi bali ya Zitto Kabwe kwa chama, ilisainiwa na haikukusudiwa kuwa ‘public'. Nimeshangazwa sana kusikia na baadaye kuona barua yenye maudhui kama yale yale ya barua yangu kwa Katibu Mkuu imewekwa mtandaoni. Barua imewekwa masaa machache baada ya kikao cha Kamati Kuu kwisha ambapo tuliweka msimamo wa pamoja wa chama juu ya namna bora ya kushughulikia suala la Lwakatare kama chama. Wakati mweka barua anadai kuwa kulikuwa na mgawanyiko katika kikao, ukweli ni kwamba ajenda hiyo haikuwa na mjadala wenye mgawanyiko kabisa na msimamo wa chama ulipatikana kwa mwafaka bila mgawanyiko. Ni dhahiri kuwa maadui zetu walitaraji mgawanyiko na baada ya kushindwa sasa wanatengeneza mgawanyiko huo kwa kusambaza uwongo wenye uzandiki.

4. Baada ya kufanya uchunguzi mdogo nimegundua kuwa ID iliyoweka video ya Lwakatare mtandaoni na ID iliyoweka barua hii mtandaoni ni IDs za mtu mmoja. ‘Coincidence' ya namna hii inashangaza na kushtusha, lakini inatuambia jambo moja kubwa ‘kwamba kuna kirusi ndani ya chama kilicho karibu sana na viongozi wa chama chenye kazi moja tu, yani kuonyesha kuwa CHADEMA hapako shwari, kuna migogoro na hatimaye kusambaratisha chama'. Kirusi hiki lazima kina nafasi andamizi au kipo karibu sana na viongozi waandamizi. Inawezekana kabisa kirusi hiki kinahusika na suala zima la Lwakatare katika kupanga, kuendesha na kutekeleza mpango mzima. Maswali kama ‘kwanini Dennis Msacky na Zitto ndani ya Video ya ‘Lwakatare' lazima sasa yaanze kutafutiwa majawabu.

5. Natoa wito tena kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA kwamba, huu ni wakati wa kuwa na umoja na mshikamano kuliko wakati wowote ule katika uhai wa chama chetu. Chama cha Mapinduzi kitatumia njia zote kutugawa, kutugombanisha na kupenyeza chuki miongoni mwetu katika juhudi za wao kubakia madarakani. Umakini wa Kiongozi huonekana wakati wa changamoto kama hizi!

6. Msimamo wa chama umetolewa na Kamati Kuu iliyomaliza vikao vyake jana siku ya ijumaa tarehe 5 Aprili 2013. Huo ndio msimamo wangu pia! Kesi ya Lwakatare ipo mahakamani, chama kimeonyesha dhahiri kumwamini Jaji aliyekabidhiwa kesi hii, sasa tuache mahakama ifanye kazi yake na tusubiri hukumu. Msemaji wa chama kuhusu suala hili ni ndugu Tundu Lissu na amekuwa akitoa ufafanuzi kila inapohitajika.

Asanteni
 
Ahsante Zitto.

CDM tufanye kazi ya ziada ya kubaini mikakati michafu ya CCM ya kuiharibu CDM.
 
Ok....

Hongera sana mkuu kwa kuja kusawazisha mambo mapema...

Niliwahi kusema mapema kuwa the central point ya mikakati ya CCM kuivuruga CDM ni kwa kumtenganisha Zitto na Chama... Nashukuru Zitto bando yupo Imara ingawa ni majaribu magumu sana...

Niliwahi kusema tena kama inavyonenwa kuwa "Sio kila anayesema Bwana Bwana ataurithi ufalme wa mbinguni" basi pia "Sio kila anayesema Slaa, Slaa ni mwenzetu katika CDM"... Na leo naongeza usemi kuwa kama ilivyoandikwa "Watakuja wengi kwa jina langu, lakini muwe makini maana ni waongo"... Wafuasi wa CDM tujue kuwa "Watakuja wengi kwa jina la Slaa, lakini, kahika wao ni wana wa yule ibilisi, CCM"

Walijitokeza watu hapa wakajifanya kuwa karibu sana na Dr Slaa, na kumshambulia Zitto kwa nguvu nyingi sana. Wanachadema wengi 'walizolewa' nao kwa bahati mbaya, lakini wachache tulioziona nyufa nyembamba kwao, tulisimama imara kuitetea CDM, bila kumtenga Zitto,.. tulitukanwa sana na hadi sasa kuna watu wananiona mimi kama msaliti.

Barua ya Zitto iliyowekwa hapa, na maelezo yake haya yanathibitisha umuhimu wa wanachadema tusimuamini kila mtu anayekuja hapa akijifanya kuwa yeye yuko karibu sana na Slaa, huku akiponda viongozi wengine wa chama. Hiki ni kielelezo kuwa ndani ya CDM, kuna watu bado wanahakikisha kuwa wanakigawa chama kwa kumchonganisha Zitto... Kama Zitto anasema kuwa barua aliyomwandikia Slaa ilikuwa imesainiwa, lakini barua hiyo tumewekewa hapa ikiwa haijasainiwa, ina maana kuwa kuna mtu alimsomea mtu kwa simu kilichokuwa humo ndani, na huyo aliyesomewa akaandika barua hiyo...

Kama mtu aliyeweka video ya Lwakatare ndiye aliyeweka barua ya Zitto... Kama barua ya Zitto imewekwa wka lengo la kuonyesha Zitto haungi mkono chama, ina maana kuwa lengo ni kumchonganisha Zitto na chama na wanachama. Ukiangalia video ya Lwakatare, utaona lengo ni kuonyesha kuwa CDM inamchukia Msaky kwa sababu yuko karibu na Zitto. Matendo yote haya mawili yana lengo moja... kuhakikisha Zitto anatenganishwa na CDM...

Namchukuru sana Zitto kwa kuendelea kuwa imara ndani ya chama, nawashukuru wanachadema wanaoamini kuwa Slaa ndiye chaguo la wengi katika kuiongoza CDM kuwatetea wanyonge, lakini viongozi wengine pia akiwemo Zitto ni muhimu sana katika kuhakikisha uimara na umoja wa CDM unadumishwa na nawaomba CDM wajue kuwa TISS wapo pale makao makuu Kinondoni pia, wanaitana Kamanda, wanasalimiana Peoples power, wanashiriki M4C, wanajifanya kuwa wanamuunga mkono Slaa na CDM kwa ujumla... lakini tusipokuwa makini kuna siku tukishakusambaratika, tutainua macho tuwaone wale "Wenzetu" wakiwa wananeemeka katika utawala wa Ibilisi...

Wake up people.... CCM hawatakubali kuachia madaraka so easily kama tunavyodhani...
 
Napata raha sana nikisoma maelezo yako ...unanipa imani kuwa wewe kweli ni mwanafunzi wa shahada ya uzamivu....wewe ni kiongozi usiyemung'unya maneno..asante sana zitto...tukutane kule twitter
 
Atleast you said it well

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mh. Zitto, haya ni maelezo mazuri kabisa, excellent! Pia umesema jambo la muhimu sana ambalo lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo, kuwa kuna mtu aliyekaribu na viongozi ambaye ni double agent. Nivizuri kuwa umeligundua hili mapema, shirikisha viongozi wenzako kulifanyia kazi mara moja.

Suala la mshikamano ni la muhimu sana, lazima lifanyike kwa vitendo na sio kwa maneno. Viongozi shikamaneni na wananachama watafuata mkondo. Mkigawanyika ninyi vivyo hivyo na wananchama wenu.

Good!
 
Kaka..hakuna coincedence dunian..everythings happen for a reasons,ccm wamewekeza pesa nyingi sana kurubuni vijana wa chadema..na vijana wengi hatuaminiki kaka
 
"Mwenyekiti Freeman Mbowe anataka ikithibitika kuwa Lwakatare alishiriki kurekodi mkanda huo iwe kwa kurubuniwa, ‘kushikishwa' au kuingizwa mkenge, itamlazimu kuwajibika kwa kosa la kukosa umakini"

Kama hadi muda huu bado haijathibitika kuwa yule ni Rwakatare na ameshiriki katika kurekodi mkanda huo, haitakaa ithibitike tena
 
Zitto,

Kwa kweli hapo ndipo unapoonyesha umakini ktk siasa. MWAKA JANA niliwahi kukushauri ndugu yangu kuwa WW huna sababu ya kupambana na mtu yeyote ndani ya chama chako muda UTAFIKA na hapo mambo yote yatakuwa mteremko kwako na kwa nchi yetu.

Nukuu bible "JINYENYEKEZE CHINI YA MKONO WA BWANA ULIOHODARI NA YEYE AYEKUNYANYUA KWA WAKATI WAKE" hila hizi za sasa ni hatari sana tena sana ila tutashinda.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom