BASATA waweka wazi Nominations za Tanzania Music Awards. Ali Kiba Aongoza

BASATA waweka wazi Nominations za Tanzania Music Awards. Ali Kiba Aongoza

Hizi tuzo kuandaliwa na Basata ni sawa tu.Kwenye maandalizi ya tuzo huwa kunatangazwa Categories na wasanii wenyewe hupeleka kazi zao kwenye hizo Categories na sio muandaaji so waandaaji huchagua ama zote au huchambua kazi zilizofikia vigezo them sasa hutoa hadharani na kusikia opinions za watu au kura. Sasa kama wewe msanii hukupeleka kazi hutakuwepo. Wasafi wasanii wao hawakupeleka kazi zao so hawatakuwepo na hawalazimishwi .
Ooh kumbe, so inaweza kuwa wakina wizkid Burnaboy @focalist n. K, na wao walipeleka kazi zao kuomba ushiriki?
 
Wakisema watende haki.....
Hizo list zote zitajaa Alikiba tu, Mwamba 2021 ulikuwa ni mwaka wake. Alitoa kazi nyingi na zote zilipokelewa vyema.
Mfano, Ndombolo ilistahili kuwepo kwenye category karibu zote ila imetajwa sehemu moja tu.
 
Loooooo kumbe maisha Tanzania 🇹🇿 yanakwenda kasi hivi, BASATA hii ndio Ile au nyingine..yaani imeua kabisa mziki wetu wa kitanzania na kutuletea uchafu huu wa Harlem, hakuna juwata jazz, ddc sikinde, vijana jazz, etc etc, why DRC kuna generation mpya ya wanamziki ILA beat ya muziki wao ipo vile vile, ukisikiliza wimbo mpya kutoka DRC hujiulizi unajua hii ni product ya DRC,angalia SA,Zimbabwe;ngoja nisogee nikapate ulanzi, karibuni lingusenguse
 
#Tanzania music awards haha afu wale wanaongoza kwa viewers,shows,followers wameondolewa hivi hawachek tuzo za wenzao huko nje?bora wangeacha tu mambo ya tuzo afu ndio wanampango wakukuza tasnia ya Music na ubaguzi huu haya tutafika tu.
 
Barnaba Classic,katemwa mazimaaa hayupo hata kipengele kimoja!! ile Cheketua ft Kiba,BaSaTa wanaiona ndogo sana au?

Kuna uwezekano mkubwa jamaa hajataka kuwepo kwenye hizo tuzo maana walichofanya serikali ni kuwaweka kwenye categories wale tu walio submit kazi zao. Tusiwalaumu BASATA kwa hili walikuwa fair sana.
 
Kama msanii, lazima pia kujisajili basata, wengine wanafanya mziki Ila hawajasajiliwa basata, ndomana kwenye list wengine wametemwa, na kuna michango hawatoi au hata kwenda kwenye vikao hawaendi, na super wetu kasema hatak tuzo zao, wakat alipewaga hizo tuzo, matokeo kawaharibia wenzake kina zuchu, na Ray.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom