BASATA: Wimbo wa WAPO wa Ney wa Mitego kufungiwa, hauna Maadili

BASATA: Wimbo wa WAPO wa Ney wa Mitego kufungiwa, hauna Maadili

BASATA wanatumia moyo kutoa maamuzi. Wamesema hauna Maadili. Na unaleta uchochezi
Unatakiwa ujiulize maadili ambayo wimbo umeyakiuka ni yapi ? Na uchochezi ni upi ? Au watu kumbukuka Jakaya "wapo" ndiyo maneno ya uchochezi ? Tatizo mnatenda kuangalia namna ya kufurahisha wakuu wenu hasa Mkuu Wa mkoa kama ndiyo kipimo cha maadili
Wimbo wowote utakaoondoa furaha ya Waheshimiwa wenu hauna maadili !
Mkuu uko sahihi sana,,, japo avatar yako inatisha
 
Kuna na ule mwingine nao unavunja maadili... ule wa "NDIO MZEE!!" waupige marufuku

Nakumbuka Tshimanga Kalala Asossa aliwahi kuzuiliwa kupigwa wimbo wake " BOMOA TUTAJENGA KESHO!!" baada ya miaka nikasikia unapigwa tena wimbo huo!
 
Ney alikua anajua utafungiwa by the time anautoa. BASATA guys are just playing to his tune. Jamaa keshaurelease na watu wameusikia na wanao kwenye devices zao.
watu wanausikiliza kama vile ni wimbo wa taifa
 
Nyimbo inafungiwaje wakati kila mtu anayo na ninavyoirudia maana inabits nzuri na maneno ndio usiseme. Wamechelewa bora waache tuu.
 
Hili jipu jipya toka Koromije ni noma, mwenye jipu yuko tayari kukosa vyote lakini si mwana kipenzi.
 
Ambao tunao huo wimbo haturuhusiwi kuusikiliza sabab umefungiwa? Naulza tu
 
Ambao tunao huo wimbo haturuhusiwi kuusikiliza sabab umefungiwa? Naulza tu
 
Kupigwa radio halikuwa Lengo la wimbo huu,
Wimbo umeshawafikia wahusika (targeted market). Utaendelea kusikilizwa tuu.

Roma mkatoliki alitumia mbinu hii 2015 akatusua.

Ney anapita mule mule hakuna kitakacho haribika.

Kwa kuendelea kumshikilia Ney nikuupa 'kìki' wimbo huu, majority watautafuta n.a. kuusikiliza.

Hivyo basi kila kinachoendelea kwa sasa ni sawa na kumpiga chura teke.
 
Kupigwa radio halikuwa Lengo la wimbo huu,
Wimbo umeshawafikia wahusika (targeted market). Utaendelea kusikilizwa tuu.

Roma mkatoliki alitumia mbinu hii 2015 akatusua.

Ney anapita mule mule hakuna kitakacho haribika.

Kwa kuendelea kumshikilia Ney nikuupa 'kìki' wimbo huu, majority watautafuta n.a. kuusikiliza.

Hivyo basi kila kinachoendelea kwa sasa ni sawa na kumpiga chura teke.
Ni kweli. Kumshikilia Nay ni kufanya hata wale ambao walikuwa hawajaupata au hawakuwa na interest ya kuutafuta wautafute kwa hali na mali. Lengo la Nay limetimia, na hakuna kesi hapo...kesho kutwa atakuwa uraiani.
 
Ukitaka kujua nguvu ya mwanaume we mtukane mke wake.
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema wataufungia wimbo wa 'Wapo' wa Nay wa Mitego kwani hauna maadili. Amesema haufai unachochea vurugu.


Huyu anafahamu ishara hiyo aliyotuonyesha?? Au kama anafahamu tumuweke kwenye kundi moja na wao????
 
bd7288bbbb04f011014580d2665266a5.jpg
Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) limeeleza kuwa wimbo wa Nay wa Mitego uliosambaa kwenye mitandao hivi karibuni ukiwa na jina la ‘Wapo’ una matusi na haufai.


Katibu Mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza ameeleza kuwa Baraza liliusikiliza wimbo huo na kubaini kuwa ni wimbo usiofaa kwa jamii na zaidi unachochea vurugu.


“Ule wimbo tumeusikiliza, kama Baraza tunasema ule wimbo hauna maadili, ni wimbo ambao una matusi, ni wimbo ambao unachochea vurugu, ni wimbo ambao haufai kwa jamii,” alisema.


Aliongeza kuwa vyombo vyote vya habari ambavyo vitaucheza wimbo huo vitakumbwa na mkono wa sheria kutoka kwa vyombo husika.


Nay wa Mitego alikamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro majira ya saa nane usiku, na lifikishwa Dar es Salaam anakoshikiliwa kwa mahojiano na Jeshi la Polisi.


Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei alithibitisha kukamatwa kwa msanii huyo usiku wa kuamkia jana.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, wakili Peter Kibatala amesema kuwa atasimamia kesi dhidi ya msanii huyo na kwamba tayari ameshamjulia hali katika kituo cha kati jijini Dar es Salaam.
 
Sijawahi kuona wimbo makini wa kuasa uongozi kama wimbo wa ney, jamaa amekwenda na wakati kweli kweli na anastahili pongezi. Kuhufuta ni dalili za uoga na kuficha criticism ya kweli kabisa. Namna hii ngumu kuendelea kifikra
Wapuuzi mbona wimbo wa Mjomba Enzi za Kikwete haukufungiwa au ule wimbo wa wagosi wa Kaya. Hata Ndiyo mzee wa Prof. J. Mimi sioni tofauti au kwa sababu kuna kisehemu kinataja Bashite na vyeti feki. Basi wafute na basi la Musukuma
 
Back
Top Bottom