mack255
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 551
- 1,230
Bashe ametoa Siri aliyoificha kwa muda, kuwa Magufuli alitaka amtumbue na amuuweke ndani. CHEKI VIDEO
Waziri Bashe amesema, alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo alikumbana na sakata la korosho ambapo ghala la Serikali lilijaa korosho, na korosho mpya zilikuwa zinaingia.
Ili kukabiliana na hilo akatoa kauli ya ununuzi binafsi wa korosho ambao utakuwa wa uwazi. Kauli hiyo aliitoa mkoani Lindi alipokuwa na Rais Magufuli ziarani.
Rais Magufuli alimuuliza kama mfumo anaoupendekeza utafanikiwa, ambapo Bashe alimhakikishia Rais kuwa mfumo huo utafanya kazi tofauti na mfumo wa Serikali kununua korosho.
Rais Magufuli akamwambia ikitokea mfumo huo umefeli atamtumbua na kumuweka ndani. Bashe akajibu kwa kumwambia Rais abariki mfumo huo na ataona matokeo.