BASHE: Hayati Magufuli aliniambia mfumo wa korosho ungefeli angenitumbua na Kuniweka ndani

BASHE: Hayati Magufuli aliniambia mfumo wa korosho ungefeli angenitumbua na Kuniweka ndani

JPM hakuwa na kuchekeana kwenye kazi.

Sasahivi ni mwendo wa kulamba asali.

#MaendeleoHayanaChama
 
Bush mpaka leo anadunda!
Obama mpaka leo anadunda na ameua watu wengi sana huko duniani kwa ajili ya maslahi yake!
.mungu wako angekuwa na akili kama angeiua ccm, maana mpaka leo bado inakutesa!
VIROBOTO hawataweza kujibu iyo hoja yao ya kishetani wao wanaamini MUNGU anafanya kazi kama wanavyo fikiri na roho zao za chuki
 
Kuna tofauti kati ya kuua raia wako wanaokukosoa wakati wa amani na kuua raia wa nchi nyingine vitani kupitia majeshi. Bush angeteka, kutesa na kuua Wamarekani kwa kutumia watu wasiojulikana ingekuwa habari nyingine kabisa. Na kwa Marekani isingewezekana. Vita za Marekani Iraq, Afghanistan na kwingineko zimezungumziwa sana hapa JF na kwenye media zote duniani. Uovu hata wa kimataifa haushabikiwi na watu wenye akili.

Urusi Putin anashambuliwa kwa kuteka, kutesa na kuua wapinzani wake nchini mwake sio kwa malaki ya waSirya au waUkraine aliowaua katika vita.

Usilinganishe mambo tofauti kabisa.
We kiroboto Kenya watu walikufa Uganda watu wanakufa nn kimewapata viongozi wa nchi iyo
 
Na ndiyo maana huyu waziri wa kilimo hajawahi kunena mabaya dhidi ya jpm ni waziri ambaye hapendi kujipendekeza anajali kazi zake, kwa kumuangalia uso wake huyo jamaa ana mazito aliyonayo lakini anaona maisha yapo na yanapita. Bashe mimi kiujumla nakutakia kila heri katika utendaji wak! Usiishi kama jamaa zako wale wanaosema chama kinawenyewe hawajui hao wenyewe ipo siku na wao watapita. Kijana kama NAPE kwa sasa vijana wengi wa kitanzania na wananchi kwa ujumla walishamjuwa ni kiongozi wa namna gani katika taifa . Piga kazi endelea hata vijana wako Bashungwa na Biteko wanafanya kazi hawashida ya kusifu na kuabudu popote watakapopelekwa wanafanya kazi. Hawana mda wa vijembe kwenye media za makongamano au mikutano yoyote.
 
Bashe ametoa Siri aliyoificha kwa muda, kuwa Magufuli alitaka amtumbue na amuuweke ndani. CHEKI VIDEO


Waziri Bashe amesema, alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo alikumbana na sakata la korosho ambapo ghala la Serikali lilijaa korosho, na korosho mpya zilikuwa zinaingia.

Ili kukabiliana na hilo akatoa kauli ya ununuzi binafsi wa korosho ambao utakuwa wa uwazi. Kauli hiyo aliitoa mkoani Lindi alipokuwa na Rais Magufuli ziarani.

Rais Magufuli alimuuliza kama mfumo anaoupendekeza utafanikiwa, ambapo Bashe alimhakikishia Rais kuwa mfumo huo utafanya kazi tofauti na mfumo wa Serikali kununua korosho.

Rais Magufuli akamwambia ikitokea mfumo huo umefeli atamtumbua na kumuweka ndani. Bashe akajibu kwa kumwambia Rais abariki mfumo huo na ataona matokeo.
Sasa hapo ndio umeandika nini ?
 
MJINGA NI WEWE UNAYEAMINI HIVYO NDIO MAANA MOLA akafanya yake Katika Maisha OGOPA SANA kumpa HAKI mwanadamu ya kukunung'unikia Kwa MUNGU kwa ULIYOMTENDEA kama vile Kumtia kilema Kutoa Uhai wake HAKIKA MUNGU hatakuacha MALIPO ya UOVU huo ni hapa hapa Duniani
Mwendazake Ananung'unikiwa mpaka LEO
Wewe ni mjinga wa kiwango Cha SGR Magufuli alikuwa mtu na nusu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hayati hakuwa na muhali zingua akuoneshee sebene tena hapo hapo.
Yeye alikuwa yupo kwa ajiri ya wasukuma tu. Wengine hata mfe poa yeye hajari kabisa ndo Mana ilikuwa ni vilio kila Kona ispokuwa chato Mana hata mbuga zilianzishwa na viwanja vya ndege pia ambapo Sasa wanafuga kuku
 
Kama nimemuelewa vizuri Bashe Inaonekana ndani ya Serikali ya Magufuli kulikuwa na watu waliokuwa wanamdanganya mheshimiwa kwa kumuaminisha uongo na kwa maslahi yao…,
Na hao watu wapo bado wanamuaminisha chifu
 
Makasiriko ya nn Boss,
Hata wewe utakufa, Na siku ya kufa kwako adui zako watafurahi sana
Muhimu Ni ujue ukifa unaenda wapi kuishi milele
Haya maneno yako ungemwambia mwenda zake juu ya Bensanane etc.
 
Mheshimiwa Hussein Bashe nakuomba radhi Sana, nimewahi kukubeza sikujua kama una "big brain" ya namna hii....
Mungu akupe nguvu na maarifa zaidi!
 
We kiroboto Kenya watu walikufa Uganda watu wanakufa nn kimewapata viongozi wa nchi iyo
Kwanza jitahidi kuandika kwa staha. Hunifahamu. Ustaarabu ni muhimu sana hapa JF.

Hakuna anayeunga mkono au kushangilia mauaji yanayofanywa na viongozi waovu popote pale duniani. Haisaidii kuhalalisha mabaya yaliyotokea katika utawala wa Magufuli na ya Uganda na Kenya.
 
Makasiriko ya nn Boss,
Hata wewe utakufa, Na siku ya kufa kwako adui zako watafurahi sana
Muhimu Ni ujue ukifa unaenda wapi kuishi milele
Ukifa umekusha hakuna cha kuishi milele kifo ni kinyume cha uhai, kuishi ni mara moja tu
 
Back
Top Bottom