Bashe jitokeze utueleze ulipofikia na BBT

Bashe jitokeze utueleze ulipofikia na BBT

Ridomil gold

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2020
Posts
2,790
Reaction score
2,232
Habari za muda huu

Kama kichwa kinavyosema namuomba mkuu BASHE aseme mafanikio na maendeleo ya BBT yake ilipofika maana mpaka sasa hatuoni matunda na hiyo kitu. Je, wamelima mazao ya mwaka mmoja au wamelipa zabibu tu?

Maana kuna madogo wanasema mpaka leo hiii bado wapo mtaani na hawajachukuliwa na waliochukuliwa wazazi wao wanalazimika kuwatumia pesa za kujikimu na BASHE hatumsikii akiongelea hicho kitu, hata wizara ya kilimo nayo imekaaa kimya.

Mfano MATI ILONGA walinunua chakula hao BBT wenyewe hakuna JITOKEZE BASHE UNIJIBU
 
Ile project ilikua failure

1. Lilipoanza swala la mashamba yawe dodoma nadhani na kigoma pia. Wakati hii Tanzania yote ina udongo wa kilimo.

2. Uvccm na wana ccm kuingilia zoezi kwa kupewa kipaumbele. Imechangia wizi wizi maana wamezoea kuiba pasipo wajibishana

3. Wake na wapenzi wa watu walioenda na mabegi walipoanza kulana kimasihara tukahesabu tayari hii
 
B.B.T nadhan ni project ya muda kidgo ..inahitaji uvumilivu kuona au kupata matunda yake...
Kwahyo kua mvumiliv kidgo...

Kuhusu vijana kutumiwa pesa na wazazi wao Hilo ni jambo lakawaida sana ..hata wanafaika wa mikopo ya elimu ya juu Kwa asilimia 100%
Hutumiwa pesa za kujikimu na wazazi wao.
 
Ingawa project nyingi za selikali Ilifeli ikiwemo

1. Kilimo kwanza ...
Chini ya waziri mkuu Pinda hakuna tulichovuna...
Utekelezaji wake ulikua mgumu Sana.

2.Big results Now.
Nayo Ilifeli ilikua ni matokeo makubwa kweny Elimu na kilimo hakuna kilichotokea Hadi Sasa ni porojo tu na pesa zililiwa.
 
Ile project niliona haina mwelekeo sababu bado inajikita kwenye uzalishaji ambapo kwa Tanzania sio tatizo yaani wakulima wengi wanazalisha sana tena kwa mbinu mbalimbali
Nadhani ni vema wizara ikajikita katika kutafuta na kusimamia masoko ya mazao hapo ndo uchawi wa wakulima wote ulipo.
 
Zilongwa Mbali, Zitendwa Mbali

Subiri HasarA Toka Kwa CAG
TANZANIA Inaliwa Na Hawa Vigogo Kama Hujui
 
Ile project ilikuwa ni mlango wa kupigia pesa tu hakuwepo la maana, unachagua vijanaa hawajawahi kushika hata jembe au hajwahi hata kuona ng'ombe akiwa hai Bali nyama kwenye friji ndo unawepeleka Huko. Huu ulikuwa ni upuuzi.
 
Kama kuna Mdau yupo huko atuambie nini kinaendelea usikute wanamtumia mama Ripoti za Uongo tu kama walivyozoeaa.
 
Kama kuna Mdau yupo huko atuambie nini kinaendelea usikute wanamtumia mama Ripoti za Uongo tu kama walivyozoeaa.
Zile zinazofanya mtumishi unaajiriwa unapangiwa kituo Cha kazi unafika eneo unakuta jengo lipo kwenye msingi na limeota majani
 
Habari za muda huu

Kama kichwa kinavyosema namuomba mkuu BASHE aseme mafanikio na maendeleo ya BBT yake ilipofika maana mpaka sasa hatuoni matunda na hiyo kitu. Je, wamelima mazao ya mwaka mmoja au wamelipa zabibu tu?

Maana kuna madogo wanasema mpaka leo hiii bado wapo mtaani na hawajachukuliwa na waliochukuliwa wazazi wao wanalazimika kuwatumia pesa za kujikimu na BASHE hatumsikii akiongelea hicho kitu, hata wizara ya kilimo nayo imekaaa kimya.

Mfano MATI ILONGA walinunua chakula hao BBT wenyewe hakuna JITOKEZE BASHE UNIJIBU

Hizi mambo za Siasa kwenye kilimo zime wapotezea vijana wengi sana muda,malengo na maono yao katika kilimo, huu mradi hauna tofauti na ule wa PASS/AIC pale morogoro ni upigaji tu uliojificha kwenye kivuli cha tunasaidia vijana, wazee ukitaka kujikwamua kiuuchumi komaaa kivyako hivi vyakuitiwa vipo tayari havinaga muda ukiona unaitiwa fursa jua wewe ndio fursa yenyewe.
 
Ile project niliona haina mwelekeo sababu bado inajikita kwenye uzalishaji ambapo kwa Tanzania sio tatizo yaani wakulima wengi wanazalisha sana tena kwa mbinu mbalimbali
Nadhani ni vema wizara ikajikita katika kutafuta na kusimamia masoko ya mazao hapo ndo uchawi wa wakulima wote ulipo.
Nilishangaa kuona Eti wanalima Chinese[emoji23][emoji23][emoji23] hii nchi hii
 
Ili tufanikiwe, serikali ilitakiwa hizo hela iwekeze kwenye cold rooms katika miji mikubwa yote, ianzishe viwanda vidogo vya kusindika mazao perishable ( matunda na mboga, samaki), kisha viwanda hivyo vikodishwe kwa private sector kuviendesha, na serikali ichukue kodi tu bila kuchomeka management yake. Vijana wangeacha kuzurula sababu akilima nyanya zake anajua atapeleka wapi, na msindikaji anajua nikishasindika napeleka wapi, hiyo chain ingevutia wengi kuingia katika kilimo sbb hofu ya hasara ingepungua sana.
 
Habari za muda huu

Kama kichwa kinavyosema namuomba mkuu BASHE aseme mafanikio na maendeleo ya BBT yake ilipofika maana mpaka sasa hatuoni matunda na hiyo kitu. Je, wamelima mazao ya mwaka mmoja au wamelipa zabibu tu?

Maana kuna madogo wanasema mpaka leo hiii bado wapo mtaani na hawajachukuliwa na waliochukuliwa wazazi wao wanalazimika kuwatumia pesa za kujikimu na BASHE hatumsikii akiongelea hicho kitu, hata wizara ya kilimo nayo imekaaa kimya.

Mfano MATI ILONGA walinunua chakula hao BBT wenyewe hakuna JITOKEZE BASHE UNIJIBU
Nasikia pesa yote wanachumua na boss wake. Wamenunua kiwanda cha Tumbaku Morogoro na wanaanza tena kujenga. Kimebatizwa jina ni MKwawa!
 
Nimepita juzi kwenye Mradi wa BBT Dodoma Chinangali, Hakuna zao walilootesha mpaka sasa, wameishia kujenga uzio na nyumba za kuishi kama apartments! Sasa najiuliza kuna Mkulima kweli pale? Hakuna cha trekta Au watu wanapiga jembe!!? Usanii mtupu! Hii project ikaguliwe na CAG na kama kuna upigaji wahusika wawajibishwe.
 
Back
Top Bottom