The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Baada ya kutupwa nje katika baraza jipya la mawaziri Hussein Bashe kupitia ukurasa wake wa Instagram anasema:
Natumia nafasi hii kumshukuru Allah kwa kila jambo na kwa baraka zake katika safari yangu ya utumishi.
Namshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa imani kubwa aliyonionyesha katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi na kuniteua kuwa Naibu Waziri, na baadae Waziri wa Kilimo.
Ni heshima niliyothamini kwa moyo wangu wote, na ninaendelea kuwa mwenye shukrani kwa nafasi hiyo ya kuwatumikia Watanzania.
Natoa pongezi za dhati kwa Ndugu Daniel Chongolo kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo. Namfahamu kama Mkulima na mzalendo. Nina uhakika atamsaidia Mheshimiwa Rais kutimiza matarajio ya Watanzania. Vilevile, nampongeza Ndugu yangu David Silinde kwa kuendelea kuaminiwa kama Naibu Waziri. Sina mashaka nae Mzazi najua atakuwa msaada mkubwa kwa Waziri wake.
Nawashukuru pia watumishi wote wa Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano wa hali ya juu mliyonipa katika kipindi cha miaka sita. Nawatakia heri na fanaka katika kuendelea kutekeleza majukumu yenu ya kuwatumikia Watanzania.
Asanteni sana.
Turudi shambani ❤️