Bashiru kusuka au kunyoa - ni baada ya Kinana kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti CCM

Biashara ya meno ya tembo itashamiri sana kipindi hiki.
 
yaani CCM kama hawampendi Bashiru si wamuue / wamfute uraia aende burundi tuu! maana kila kukicha anaongezewa stress mwisho wa siku atajinyonga yule mzee.
Watoto wa mjini wanasema kawekewa ngwaka
 
Ndani ya CCM mabadiliko ni kitu cha kawaida. Kumbuka wakati Makamba anaingia kwenye Ukatibu Mkuu Mangula alifanyiwa figisi za nguvu na wanamtandao wakati anatoka ndani ya ukumbi akakuta gari yake ya Ukatibu Mkuu limeshachukuliwa hadi akaomba lift lakini baada ya miaka mitatu akachaguliwa kuwa Makamo wa Mwenyekiti Bara. Kwa hiyo haya si mageni ndani ya CCM. Labda ni mageni kwa wana CDM.
 
Uzuri wa hawa watoto wa mjini, wala hawanaga makelele. Wanajua kucheza rafu za kimyakimya, anaechezewa ndio atapiga kelele mwenyewe.

Hautasikia Nape anamsimanga Makonda, wala hautasikia Kinana anamsema Bashiru. Watoto wa mjini wanajua kumchinja kobe hakuhitaji papara wala kelele. Ni TIMING tu!
 
Hili ni fundishon kwetu sisi kama binadamu kuwa madaraka ni koti la kuazima leo unalo kesho mwenye nalo kalichukua.
Muhimu tutende kwa mujibu wa sheria na taratibu.Na wamshukuru Mungu Rais wa sasa wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu mpendwa Samiah Suluhu Hassan hana roho ya kisasi.
 
Ukiwa mnyoofu kwa maadili ya uongozi kitu walichokafanya Kinana, Makamba Sir, Makamba son na Nape hawakupaswa kurudi kuwa viongozi kabisa! Sema tu kwakuwa Mamanae ndiyo timu yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu jinsi tu ulivyoandika inaonekana una maumivu makali sana. Unatafuta faraja kwa lazima.
 

Bashiru kuikimbia nchi​

 
Ila pasipo kushangalia ujio wa kishindo, na kwa namna ile ile ya awali, yaani ujio wa kivingine wa "ari mpya, nguvu mpya, na kasi mpya" slogan iliyoibuliwa na Prof. Mukandala huyu huyu.

Uongozi wa sasa unalazimika kuendeleza na kudumisha mazuri yaliyofanywa na mwendazake. Wananchi wa kada ya chini walimkubali, kumuhusudu na kumwamini.

Wakishindwa kufanya hivyo, utazaliwa upinzani ndani ya CCM, yaani CCM Mpya yenye kumuwakilisha na CCM Maslahi ya hawa wanamtandao na wafanyabiashara wanaokishikilia chama na serikali yake.

Hizi sauti zinazosikika kuhusu haja ya kuwaindoa wahuni waliopo ndani ya chama si za kubeza. Chama kikubwa na kikongwe husambaratika kupitia "its internal weaknesses" na wala siyo kwa kupitia "its external threats"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…