Ewe mshirika wageuza maneno kwenda kinyume nyume, hapo anazungumzia kiti katibu mkuu wa chama sio kwenye utendaji wa serikali. Yaani umeenda ukachomoa kipande cha hotuba nzima halafu unaleta hapa kufumbata hoja yako mfu.
Kwa wenye akili wamethibitisha kwamba hajakatalia kukalia kiti hicho kwa muda mrefu hadi kuwa mkurugenzi wa nchi nzima. Kama unakitaka kiti hicho basi fuata taratibu za kuomba kupitia kwa mwenekiti wa chama hicho ijapokuwa itakuwa ni mazingaombwe kwa mtu kama wewe ulikunywa rangi za bendera ya v na kuapishwa na mizimu kukengeuka kwenda kwenye kijani.
Alikoteuliwa imezingatia utii , weledi, nidhamu na utendaji kazi uliotukuka na unaozingatia usawa kwa kadri anavyoamini. Ili kukata mzizi wa fitina unazozichomoza hapa weka picha mwendo ya picha mwendo ya hotuba kamili ili chenga zipembuliwe kuliko kuleta uchonganishi usio na mashiko yoyote.