Bashiru tunza ahadi yako ya kutokubali uteuzi mwingine wowote

Bashiru tunza ahadi yako ya kutokubali uteuzi mwingine wowote

Kujipendekeza, kujiapisha, kupayuka, kujisemea, upofu, upogo na kutochelea kesho. Sijui ataramba matapishi yake au kufunika kombe. Ila Mungu anamuona, umma unamuona na sijui kwanini aliyemteua alisahau nadhili hii ya kichovu. Unajua limbukeni na maskini akipata. Hawa madaktari wa Bongo wa kuungaunga wana taabu sina mfano. Kama Bashiru angekuwa muungwana, kama alivyojiapiza angekataa ua kuomba kikombe hiki kimuepuke. Kwa vile ni mchumia tumbo na mnafiki, atanywea na kula mahanjumat. Hawa ndiyo aina ya viongozi tulio nao. Kazi kweli kweli. Shame on you Bashiru.

Hapa hakuna cha ajabu kwani wote wapo hivyo* kizuri hapa huyo bwana kaonyesha rangi zake zote kwa jamii , kwa wana ccm wenzie*
 
😂"Only stupid people don't change their minds"....Former UN Secretary General ..(1992- 1996).
Boutros Boutros-Ghali Quotes 😂
 
Ukitoa comment kama unaonekana ni mnafiki, na una uwendawazimu wa aina fulani. Hata mtu mwenye akili ndogo kabisa, hawezi kuwa na fikra kama hizo.

Ujinga ujinga unaouandika kama huu, unakufanya wanaJF wakuouuze na wakuone bwege. Hata siki moja ukileta jambo la maana, hakuna atakayelipa umuhimu, kwa kuamini kuwa hakuna hoja ya maana inayoweza kutoka kwa mwendawazimu.
Mama Pekupeku wa Chakubanga huyo. Nadhani hazimtoshi kabisa. Ile kitu inaitwa aibu aliinya chooni! Vinginevyo angeiendea. Bila aibu ni hayawani tu. Naye ndivyo alivyo.
 
Bila shaka unaikumbuka kauli hii, tunaomba uitunze, uiheshimu na kuitekeleza kama maneno yako yalivyotamka.
View attachment 1712608
Ewe mshirika wageuza maneno kwenda kinyume nyume, hapo anazungumzia kiti katibu mkuu wa chama sio kwenye utendaji wa serikali. Yaani umeenda ukachomoa kipande cha hotuba nzima halafu unaleta hapa kufumbata hoja yako mfu.

Kwa wenye akili wamethibitisha kwamba hajakatalia kukalia kiti hicho kwa muda mrefu hadi kuwa mkurugenzi wa nchi nzima. Kama unakitaka kiti hicho basi fuata taratibu za kuomba kupitia kwa mwenekiti wa chama hicho ijapokuwa itakuwa ni mazingaombwe kwa mtu kama wewe ulikunywa rangi za bendera ya v na kuapishwa na mizimu kukengeuka kwenda kwenye kijani.

Alikoteuliwa imezingatia utii , weledi, nidhamu na utendaji kazi uliotukuka na unaozingatia usawa kwa kadri anavyoamini. Ili kukata mzizi wa fitina unazozichomoza hapa weka picha mwendo ya picha mwendo ya hotuba kamili ili chenga zipembuliwe kuliko kuleta uchonganishi usio na mashiko yoyote.
 
Back
Top Bottom