Bashiru tunza ahadi yako ya kutokubali uteuzi mwingine wowote

Ndo umemaliza kuweka ushahidi..!? Tuna safari ndefu sana wallah...
Baradhuli uitwaye johnthebaptist watia kinyaa kufuru. Ungekuwa na uelewa walau kiduchu ungeelewa kuwa jj Mnyika kaenda zaidi ya mahakamani. Wamefukuzwa chamani na nafasi zao zimetangazwa kuwa wazi. Wakwenda mahakamani sasa nani? Shauri lako Mashauri ( Mbowe na Matiko) analitupa kwa Matupa ( Tundu Lissu) likitoka kwa Simba ( wabunge wa cdm+ mashinji!) Wasindikize mahakamani watetee uanachama wao na hizo nafasi zao chamani. Vinginevyo funga hilo bakuli!
 
Jina lenyewe la kuokoteza na ulewa pia wa kuokoteza. Ungesoma ukiri wa Stoic #145 usingetuletea utopolo wako hapa. Bandiko refu bure tu. Uliona wapi pumba kupembua chenga. Sikiliza tena clip. Kuna sehemu anang'aka kabisa kuwa hatokubali cheo chochote nchini. Itakuwa nchini Tanzania na nchini si chamani. Akili kama zako anahamaki kuwa hakuulizwa na m/ kiti. Je, angeulizwa angekataa? Hata uteuzi wa jana kauona mtandaoni. Hakuulizwa wala kushauriwa. Tanzanian style! Wote watakubali tu. Watake wasitake. Kaishateua. Hapangiwi. Sasa zamu yake. Atake asitake, akubali asikubali lazima atawale milele. Atapangiwa. Mwosha daima dumu huoshwa. Magufulification. Patrice Lumumba original angesema Mobutufication!
 
Ikiwa atakataa uteuzi huo nitaamini maccm wamebadilika na wameanza kutenda ama kutekeleza kwa matendo kauli zao. Lakini nijuavyo wao husema yaliyo kinyume na nafsi zao... walioshangilia "akiporoja" sitoshangaa wakimshangilia tena...
 
Hiyo ilikuwa ni kauli ya siasa ,hamna haja ya kukumbuka vitu vya kijinga kama kauli hizo kwa sasa,labda kuanzia 2026
Nanukuu tu sentensi yako Mkuu "...vitu kama kauli hizo za kijinga!!" Kisha natafakari ni mtu wa aina gani hutamka vitu vya kijinga... natafakari zaidi ni kina nani hushangilia na kuunga mkono huku wakisifia kauli za kijinga... nawaza tu ikiwa neno lile "malofa wapumbavu" kuna liliowalenga basi kuna shimo tunalokwenda kudumbukizwa...
 
Hakuna kinacho niuma bali nasikitika kuona anakula matapishi yake na MATAGA kama wewemnafurahia kama mazuzu vile
"Lowasa fisadi, Lowasa si fisadi" list of shame - Chadema hao
 
"Lowasa fisadi, Lowasa si fisadi" list of shame - Chadema hao
Sasa hivi lowasa yupo ndani ya ccm mliko kuwa mnamporomoshea matusi ya nguoni.

Wewe mwenyewe ulikuwa mmoja wapo na mwenzako Kasheku
 
Labda kwa uungwana angetengua kwanza kauli yake hii ya awali na kisha kusonga mbele!! Mbona prof Lipumba alitengua barua yake na akasonga mbele!!
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† Magoli yanapanuliwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…