Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Mungu ni mwema sana sana.
Hivi sasa roho wa uharibifu ameanza kumalizia kazi yake ndani ya CCM, na tukae mkao wa soap series yenye maeneo mengi ya wanaCCM kutafunana wenyewe kwa wenyewe huku wakielekea kwenye anguko lao taradadi.
I am not joking. Nilishaona kuyumba kwa mwelekeo wa chama hiko since 2005 na hatimaye leo tunaahuhudia nyufa kubwa zisizorwkwbishika.
Hivi karibuni amesikika aliyewahi kuwa Katibu Mkuu CCM Taifa akiwahamasisha wanyonge hususani wakulima kuwavimbishia shingo wanyonyaji ambao ndiyo watawala akisema ni sharti wakubwa watimize wajibu na siyo sahihi kuwasifia sifia.
Kishindo hiki cha dafu kuanguka kutoka kwenye mti wa komamanga kumewaibua wapayukaji na wale wanaoongea huku akili zao zikiwa zimwfungiwa kwenye kasiki wakimnanga na kumuonya Bashiru kuwa hapaswi na hana haki ya kumkosoa kiongozi mkuu wa chama.
Kwa mnaotembelea mitandaoni, fuatilieni pia posts za chakubanga wetu kipepe mfukuza wahuni za hivi karibuni mtagundua kuwa kuna muunganiko usio wa kawaida na tukio la Katibu Mstaafu kutoa msimamo wake na kauli yake ya kwanza baada ya kuenguliwa Ukatibu na kung'olewa pale Ikulu.
Nasema muunganiko usio wa kawaida ni kwa sababu post yake ya mwisho ya bwana yule amerudia kauli yake iliyompelekea kuteuliwa ili kumziba mdomo inayohusu masela fulani wa kihuni.
Ninatabiri kuwa wawili hawa wanaweza kutema nyama ama kutemeshwa wakati wowote na upo uwezekano orodha ikawa ndefu na kilichokuwa kinasubiriwa ni nani ataanza kuongea wakati wa kula ili timua timua ianze.
Kwa ninavyoifahamu CCM inachoangalia ni nafasi yake kuendelea kushika dola hata kama kuna nafsi kadhaa zitakazopaswa kukutanishwa na Ziraili.
Bado msimamo na imani yangu kwamba Watanzania tusiwe moved na drama maana chama dola kina hulka ya kuja na episodes zinazosisimua nyakati za kuelekea uchaguzi lakini this time wamemeza mwiba wa pono na umenasa kooni.
#KataaCCMuliokoeTaifa