Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake katika kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya matukio mbalimbali ya kihalifu, ikiwemo tukio la kukamatwa na kuhojiwa kwa mtu anayetuhumiwa kutoa ujumbe wa vitisho kabla ya shambulio dhidi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima.
Bashungwa ametoa pongezi hizo leo Mei 5, 2025, mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Jumanne Muliro, kuhusu hatua zinazochukuliwa na Jeshi hilo kufuatia matukio mbalimbali ya kihalifu.
"Nimepata taarifa za kukamatwa na kuhojiwa kwa aliyetoa vitisho kabla ya tukio la kushambiliwa la Padri Kitima. Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada mbalimbali zinazoendelea za ufutiliaji wa matukio mbalimbali yaliyotokea" amesema Waziri Bashungwa.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Aidha, Bashungwa amelielekeza Jeshi la Polisi kuendelea na msako dhidi ya washukiwa wa matukio yote ya kihalifu na kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria kwa haraka.