Bashungwa: Barabara za mwendokasi ambazo hazijaanza kutumika, zitumike kwa magari binafsi ili kupunguza foleni

Mbona Hakufanya Hivyo alipokuwa Waziri wa TAMISEMI??
 
Badala ya kusonga mbele tunarudi reverse ikibidi hata dereva wa kushoto apite kulia kukwepa foleni.
 
 
Au wamemnukuu vibaya? Walahi napata wakati mgumu kuelewa.
Mimi nafikiri anamaanisha zile njia ambazo mwendokasi haijaanza kazi kama kilwa road. Ila kama anamaanisha morogoro road kwa kweli anastahili msaada wa kimawazo. Namuona kama mmoja wa mawaziri wanaojitambua
 
Kilwa road kuanzia uhasibu hadi posta ni kawaida tunatumia sana njia ya mwendokasi. Magari hayajaanza kazi kwanin ? Ingawa kuna siku wanafunga eti mkandarasi analalamika miundombinu inachakaa
Juzi na Jana nimepita kwenye mwendokasi kuanzia pale mataa ya kamata,darajani PUMA,mivinjeni,mtongani Hadi mbagala kizuian
 
An argument from the person with a short-sighted mind.
Huyu Waziri anapaswa akumbuke kwamba Kabla ya kutafuta suluhisho kuhusu tatizo lolote lile ni LAZIMA kwanza afanye utafiti wa kina kabisa ili kujua chanzo halisi cha tatizo husika.
Baada ya kujua chanzo cha tatizo ndipo Sasa anaweza akatafuta suluhisho au utatuzi wake.
Aidha, daima anapaswa akumbuke kwamba muda wowote ule anapotaka kufanya Uamuzi wa kudumu ni LAZIMA azingatie sababu za kudumu. Asiwe anakurupuka katika kufanya Maamuzi.

KIINI cha kuwepo kwa Janga la foleni za barabarani katika mifumo ya usafiri na usafirishaji katika Mji wa Dsm ni kutokana na kukosekana kwa Mipango-miji, kuna tatizo la kifo cha taaluma ya Mipango-miji katika nchi hii.
 
Iwapo wataruhusu tu basi hakuna cha kukataza tena maana tunajijua
Angalia walipoambiwa jamaa zetu zile hela za kubrashi walivyoongeza kasi kuzidai
Na mwingine akasema kuleni kiasi, ndio akafungulia ziliwe zote

Who let the Dogs out?
 
Wazo zuri sana.
Ingependeza gari za Abiria tu ndio zipite Mwendokasi Asubuhi na Jioni ili kuwawahisha Wafanyakazi Makazini.
Ila Malori ya mizigo yapite njia ya kawaida.
Kuyapitisha Malori kwenye Mwondokasi ni kuharibu Barabara na pia kuongeza foleni kwakuwa mengi yanaharibikia barabarani na kusababisha foleni muda mwingi.
Naunga mikono Hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…