Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Heee kumekucha! Wameanza kuchomeana mingo zao
Kazi ipo mbona, acha nikae siti ya mbele kabisa!
===============
Basi la abiria aina ya Yutong linalomilikiwa na kampuni ya
Abood, lenye namba ya usajili T 181 EMJ, limekamatwa katika eneo la Tegeta Kibo jijini Dar es Salaam likiwa limesheheni kilogramu 101.2 za mirungi zilizokuwa zimefichwa kwa ustadi mkubwa ili kukwepa kugundulika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema basi hilo lilikuwa likifanya safari kati ya Mombasa, Kenya na Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa dawa hizo zilifichwa katika maeneo
mbalimbali ya basi, ikiwemo ndani ya mfumo wa hewa wa kiyoyozi (AC).
Soma Pia: Wakazi wanne wa Wilaya ya Same wamefikishwa Mahakamani wakidaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, watu watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Waliotajwa ni dereva Ramadhan Mohamed (52), kondakta Salma Sanga (26), pamoja na Twahilu Athuman (38), Mohamedy Mikidadi (37) na Ibrahim Mohamed (39).
Milungi ndio nini hizo?Je hizo kgs za milungi zitateketezwa au huwa zinapelekwa wapi? Naomba mamlaka ziwe zinateketeza hizo dawa hadharani.
Cc Malaria2, Stuxnet, FaizaFoxKwa mujibu wa mamlaka hiyo, watu watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Waliotajwa ni dereva Ramadhan Mohamed (52), kondakta Salma Sanga (26), pamoja na Twahilu Athuman (38), Mohamedy Mikidadi (37) na Ibrahim Mohamed (39).
sijakuelewa.Milungi ndio nini hizo?
Pole Kwa conductor, 26yrs bado mdogo sana kwenye safari ya kuishi, kua Mke na Mama
Ni coincidence majina yote ni watu wa Religion moja?
“Yalifichwa kwa ustadi mkubwa” imekuaje yagundulike 20km kutoka final destination?
Hapo kuna msela kaamua tu kuunguza picha,uhalisia hii nchi hakuna ukaguzi wa namna hiyo barabarani.
Kinachokamatwa ni tone tu ya vile vinafika sokoni.
Ba kwa sheria za nchi hii hilo basi nalo linataifishwa au namna gani?
Sio kweli!Ndio maana magari yanagoma kukaa stendi ya 'Magufuli' pale Mbezi.
Wanaingiza pesa nyingi kwenye mizigo kwasababu huko kwenye stendi zao hakuna ukaguzi wa mizigo