TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,864
- 5,254
Basi la abiria aina ya Yutong linalomilikiwa na kampuni ya Abood, lenye namba ya usajili T 181 EMJ, limekamatwa katika eneo la Tegeta Kibo jijini Dar es Salaam likiwa limesheheni kilogramu 101.2 za mirungi zilizokuwa zimefichwa kwa ustadi mkubwa ili kukwepa kugundulika.
Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 13, 2026, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema basi hilo lilikuwa likifanya safari kati ya Mombasa, Kenya na Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa dawa hizo zilifichwa katika maeneo mbalimbali ya basi, ikiwemo ndani ya mfumo wa hewa wa kiyoyozi (AC).
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, watu watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Waliotajwa ni dereva Ramadhan Mohamed (52), kondakta Salma Sanga (26), pamoja na Twahilu Athuman (38), Mohamedy Mikidadi (37) na Ibrahim Mohamed (39).