TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,864
- 5,254
Dereva na konda kazi wanayo kwakweliBasi la abiria aina ya Yutong linalomilikiwa na kampuni ya Abood, lenye namba ya usajili T 181 EMJ, limekamatwa katika eneo la Tegeta Kibo jijini Dar es Salaam likiwa limesheheni kilogramu 101.2 za mirungi zilizokuwa zimefichwa kwa ustadi mkubwa ili kukwepa kugundulika.
Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 13, 2026, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema basi hilo lilikuwa likifanya safari kati ya Mombasa, Kenya na Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa dawa hizo zilifichwa katika maeneo mbalimbali ya basi, ikiwemo ndani ya mfumo wa hewa wa kiyoyozi (AC).
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, watu watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Waliotajwa ni dereva Ramadhan Mohamed (52), kondakta Salma Sanga (26), pamoja na Twahilu Athuman (38), Mohamedy Mikidadi (37) na Ibrahim Mohamed (39).
Inawezekana mtu kawafix. Wabongo jau sana.Dereva na konda kazi wanayo kwakweli
Wameuzwa haoInawezekana mtu kawafix. Wabongo jau sana.
Kwenye kufixiana huko inategemea dili walivyokuwaInawezekana mtu kawafix. Wabongo jau sana.
Wala mirungi khat miraa jaad 😄 huwa hawalali ni watu wa kukesha tu wanamungunya mpaka alfajiriMirungi,bangi,gongo viruhusiwe tu kwa wahitaji msipoteze muda nao wanunuzi.
Mirungi sh 100 pisi
Bangi 100 msokoto
Gongo 500 lita.
Unawakamato hao watu,utawalaza bure,wanakula wali maharage bure huduma zote za kijamii unampa mtu naulevi wake simple tu.
Kwenye issue za heroine,cocaine mdeal nao bila maswali.
Ila hawa wanakula majani km mbuzi waache tu mpaka waombe poo wenyewe.
Uchunguzi ndiyo utaamua.Hapo kuna msela kaamua tu kuunguza picha,uhalisia hii nchi hakuna ukaguzi wa namna hiyo barabarani.
Kinachokamatwa ni tone tu ya vile vinafika sokoni.
Ba kwa sheria za nchi hii hilo basi nalo linataifishwa au namna gani?
Mraibu wa mirungi anakuwa mchafu mchafu sana kwa kujaza hayo matakataka mdomoni kutwa bila kupumzika.Wala mirungi khat miraa jaad 😄 huwa hawalali ni watu wa kukesha tu wanamungunya mpaka alfajiri
Ni kweli hawa wangeachwa tu wasagee mpaka wenyewe waseme basi
Ova
Bangi 100 msokoto?Mirungi,bangi,gongo viruhusiwe tu kwa wahitaji msipoteze muda nao wanunuzi.
Mirungi sh 100 pisi
Bangi 100 msokoto
Gongo 500 lita.
Unawakamato hao watu,utawalaza bure,wanakula wali maharage bure huduma zote za kijamii unampa mtu naulevi wake simple tu.
Kwenye issue za heroine,cocaine mdeal nao bila maswali.
Ila hawa wanakula majani km mbuzi waache tu mpaka waombe poo wenyewe.
Kama fungu la mchicha 10,000Bangi 100 msokoto?
Location?Kama fungu la mchicha 10,000
Dogo Semenya hydroxo umesoma hayo majina mtu wangu wa udindivu?Heee kumekucha! Wameanza kuchomeana mingo zao
Kazi ipo mbona, acha nikae siti ya mbele kabisa!
===============
Basi la abiria aina ya Yutong linalomilikiwa na kampuni ya
Abood, lenye namba ya usajili T 181 EMJ, limekamatwa katika eneo la Tegeta Kibo jijini Dar es Salaam likiwa limesheheni kilogramu 101.2 za mirungi zilizokuwa zimefichwa kwa ustadi mkubwa ili kukwepa kugundulika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema basi hilo lilikuwa likifanya safari kati ya Mombasa, Kenya na Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa dawa hizo zilifichwa katika maeneo
mbalimbali ya basi, ikiwemo ndani ya mfumo wa hewa wa kiyoyozi (AC).
Soma Pia: Wakazi wanne wa Wilaya ya Same wamefikishwa Mahakamani wakidaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, watu watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Waliotajwa ni dereva Ramadhan Mohamed (52), kondakta Salma Sanga (26), pamoja na Twahilu Athuman (38), Mohamedy Mikidadi (37) na Ibrahim Mohamed (39).