Basi la Bawacha kuondoka Geita kesho kuelekea bungeni Dodoma kuwang'oa akina Halima Mdee na wenzake

Hao kinamama wanapigania ugali,wanajua wakina,mdee wakitolewa bungeni hizo nafasi watazichukua wao,ogopa sana wanasiasa!
 
Karibuni dodoma, napendekeza wakifika wakutane na akina mdee wajadiliane wafikie mwafaka hili mbona linazungumzika,
 
Aisee.. Ngoja nimshtue imhotep, salary slip, Bak, na bawacha wengineo wawapokee hapo dodoma.
Kwakweli mimi nitaenda kuwaunga mkono na kumbebea Bango Ndugai asiendelee kuikanyaga Katiba ya Jamhuri.
 
Ulicho andika ni upumbavu uliokuwepo enzi za Magufuli, na sio sifa kujinasibu nao kwa sasa.
Matumizi ya nguvu katika kupambana na mawazo tofauti kwa wakati huu ni ushamba kabisa. Jaribu kutoka kwenye fikra hizo
 
Haya mawazo ya kijinga na kishamba yatatawala vichwa vyenu mpaka lini?View attachment 1778876
Mtaji wa wanasiasa ni wana
Haya mawazo ya kijinga na kishamba yatatawala vichwa vyenu mpaka lini?View attachment 1778876
Mtaji wa wanasiasa wa upinzani Tz ni kuwatumia wanachama mbumbu kama ww ambao huwatumia kama daraja kufikia malengo yao. Tuliona wanasiasa wa kweli kama kina Mandela ambao walijitoa wao na familia zao kama vile Winnie Mandela akiwa bega kwa bega na mumewe wakipigania haki za wenzao. Lakini Tz viongozi wa vyama vya siasa wamekuwa wakiwaswaga wanachama wao kama mifugo inayokosa mchungaji waingie barabaran kupambana na kile wanachokiita uonevu, huku viongozi na familia zao wakiwa majumban kwao ndan ya viyoyozi wakiiangalia misukule yao inavyohenyeshwa na vyombo vya dola. Hii imesababisha vijana wengi waanze kujitambua na kugomea maandamano au vurugu zinazoandaliwa na viongozi hao, kama walivyomgomea Lisu. Inasemekana vijana wengi walihitaji kumuona kwanza Lisu na familia yake wakiwa mstari wa mbele ili kuwaongoza, lkn walipoona Lisu yupo nyumban kwake na familia yake akisubiri kuona ktk tv kinachoendelea na wao pia wakagomea kujitokeza barabarani.
 

Acha vitisho vya yule dhalimu aliyeko motoni. Wapigwe kwa kosa gani. We nyeshea maua hapo kwenye kaburi la dhalimu ndio kazi inayokufaa.
 

Umekuwa msemaji wao siku hizi?
 

Ww una bahati maana hao wanaoongoza nchi wakitembelea maVXR wananchi pia huwa wanayapanda. Hao wananchi waonakunywa maji ya matope, mbona hawali vizuri kama watoto wa viongozi wanaowaambia wanawajali wanyonge?
 
UTAWALA WA KIJIMA UTAWAPIGA MABOMU.

HUO NI UHALIFU DHIDI YA BINADAMU LAZIMA MKUU WA NCHI AELEWE!.

KATIBA IHESHIMIWE.
 
Bila ya taarifa yako kuwa na source, labda kama wewe umekuwa msemaji wao.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Kwa sasa chadema hainaga source rasmi, nawasiliana direct na makamanda wa Geita!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…