Basi la timu ya JKT Tanzania FC, likitokea Dodoma baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji, limepata ajali leo, tarehe 27 Oktoba 2024, saa 1:00 asubuhi, eneo la Mbweni. Basi lilikuwa likiendeshwa na MT 92327 Cpl Hassani Bakari Darajani, liliacha njia na kuanguka mtaroni.
View attachment 3136468
Wachezaji kadhaa wako chini ya uangalizi wa madaktari. Miongoni mwao ni Dany Lyanga, John Bocco, Salum Gado, Gamba Matiko, Said Ndemla, Yakoub Suleiman, Hassan Dilunga, Maka Edward, Hassan Kapalata, Hassan Machezo, na Mohamed Bakari.
Timu inakabiliwa na mechi ya ligi dhidi ya Simba SC, Jumanne Oktoba 29, saa 10:15 jioni, katika Uwanja wa KMC
View attachment 3136466