Basi la Klabu ya JKT Tanzania lapata ajali, Wachezaji 12 wapo chini ya Uangalizi

Basi la Klabu ya JKT Tanzania lapata ajali, Wachezaji 12 wapo chini ya Uangalizi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kikosi cha timu ya soka ya JKT Tanzania, kimepata ajali baada ya basi lililowabeba kuacha njia na kuanguka mtaroni majira ya saa 1:00 asubuhi leo na kusababisha maumivu kwa baadhi ya wachezaji na wafanyakazi wengine.
IMG_0403.jpeg

Basi hilo limepata ajali likiwa linatokea jijini Dodoma kucheza mechi ya NBC Premier League dhidi ya Dodoma Jiji

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, miongoni mwa wachezaji waliopata maumivu ni pamoja na John Bocco, Dany Lyanga Said Ndemla, Hassan Dilunga na Maka Edward.
IMG_0401.jpeg

Timu inakabiliwa na mechi ya ligi dhidi ya Simba SC, Jumanne Oktoba 29, saa 10:15 jioni, katika Uwanja wa KMC
 
Basi la timu ya JKT Tanzania FC, likitokea Dodoma baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji, limepata ajali leo, tarehe 27 Oktoba 2024, saa 1:00 asubuhi, eneo la Mbweni. Basi lilikuwa likiendeshwa na MT 92327 Cpl Hassani Bakari Darajani, liliacha njia na kuanguka mtaroni.
View attachment 3136468
Wachezaji kadhaa wako chini ya uangalizi wa madaktari. Miongoni mwao ni Dany Lyanga, John Bocco, Salum Gado, Gamba Matiko, Said Ndemla, Yakoub Suleiman, Hassan Dilunga, Maka Edward, Hassan Kapalata, Hassan Machezo, na Mohamed Bakari.

Timu inakabiliwa na mechi ya ligi dhidi ya Simba SC, Jumanne Oktoba 29, saa 10:15 jioni, katika Uwanja wa KMC
View attachment 3136466
Mbweni ya wapi maana zipo nyingi nazo
 
Last time basi la timu ya polisi Tanzania nalo lilipata ajali na kumsababishia ulemavu wa kudumu yule mchezaji somebody.... Mdamu!!
Safari hii ni JKT Tanzania!!

Nadhani majeshi yetu kuna mahali yanazembea kwenye kuyafanyia service magari yao. Hivyo ni vizuri hatua zikachukuliwa mapema ili kuzuia hizi ajali ambazo zinaweza kuzuilika.
 
Wapone haraka Mungu awafanyie wepesi wanatakiwa kumalizana na Simba ASAP
 
Tatizo madereva wa vyombo vya ulinzi huendesha kibabe barabarani Kwa kigezo Cha ukamanda
 
Back
Top Bottom