Basi la Mwendokasi lanusurika kuwaka moto Morogoro road

Basi la Mwendokasi lanusurika kuwaka moto Morogoro road

Kama bado unapanda mwendokasi itoshe kusema huupendi uhai wako🥲🥲❗
 
Wakuu,

Kuna basi moja la mwendokasi limenusurika kuwaka moto asubuhi hii. Stori inaanzia Mitaa ya Shekilango ambapo limetupita, mimi na rafiki yangu tukiwa kwenye bolt. Kwa moshi uliokuwa unatoka haikuwezekana hata kusoma number plate yake, ulikuwa mzito sana kiasi cha kuziba barabara yote.

Nawaza, dereva alikuwa haoni moshi huu kupitia side mirror? Maana hakusimama, aliendelea kwenda tu. Vipi lingewaka huku abiria wote wakiwemo?

Tulipokaribia maeneo ya kituo cha Mwembechai, tulishangaa kusikia kelele na watu wakiruka kutoka kwenye moshi mzito, kumbe ilikuwa ni ile mwendokasi watu wanaruka kutoka madirishani.

Ilibidi barabara ifungwe kwa muda maana watu walikuwa busy kujiokoa. Nasikitika sikuweza kurekodi video nzuri sababu ya upande niliokuwa nimekaa kwenye gari lakini nilichokiona asubuhi hii kinanipa wasiwasi sana kuhusu mustakabali wa usafiri huu wa umma unaopigiwa kelele kila siku bila mabadiliko yoyote.

Nasikia devera akisaidiana na wapita njia walizima ule moto kwa fire extinguishers.

View attachment 3313829
Siisiiemuuuuu oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee mitano tena kwao
 
Na mimi kuna siku nimepanda mwendokasi kutoka gerezan kwenda kimara, kuna yale magari madogo ambayo wanatangaza ukipanda halishushi mpaka kimara, wao wanayaita bombadier wanaotumia usafiri huu wanajua, basi safari inaanza tu gari linatoa moshi mwingi sana mpaka watu walioko pembezoni mwa barabara wakawa wanatushangaa tuliomo ndani ya basi, tulipofika maeneo ya kibo watu walioko nje wakaanza kupiga kelele basi linawaka moto, tukamwambia dreva ila yeye hakukubali akaendelea tu kuendesha, alitokea mtu mmoja pembezoni mwa barabara akawa analikimbiza gari kwa pembeni uku akitupigia kelele gari linaungua, tuliponyanyuka wote kwenye seat na kumpigia kelele dereva asimame ndipo akasimama kituo cha corner na kufungua milango, ebana eee, kutoka nje tunakuta kweli moto unawaka kwenye exos,wakaja wale walinzi wa kituoni wakiwa na fire extinguisher wakauzima, tangu siku hyo ata nikipanda mwendokasi sikai nyuma ng'o, nakaa karibu na dereva ili atakapotokea na mimi natokea hapo hapo
 
Back
Top Bottom