Kitimoto
JF-Expert Member
- Aug 25, 2012
- 6,941
- 7,808
BAADA ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuliamuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulipa deni la Sh 56,446,700, wakili wa Taasisi za Filbert Bayi, Karoli Tarimo amefungua maombi kukazia hukumu akiiomba mahakama iruhusu kulikamata basi la TFF lenye namba za usajili T581 CGR liuzwe ili kulipa deni hilo.
Taasisi hiyo inaidai TFF fedha hizo kwa miaka mitatu ambazo kwa mujibu wa Tarimo zilikuwa ni gharama ya kambi kwa timu za vijana chini ya miaka 13, 15, 17 na ile ya wanawake katika taasisi hiyo Kibaha mkoani Pwani.
Alisema Juni 3, 2019 taasisi hiyo iliingia makubalino na TFF ya miaka mitatu kutoa huduma za viwanja, usafiri, kambi na chakula wenye thamani ya Sh521.4 milioni ambazo walikubaliana zilipwe kwa awamu na kusalia Sh76.4 milioni ambazo Julai 20, mwaka jana rais wa TFF, Wallace Karia alikiri katika mahojiano na gazeti hili na kusema suala hilo lilikuwa linashughulikiwa.