Basi laacha njia na kugonga magari saba Moshi, watu 15 wajeruhiwa

Basi laacha njia na kugonga magari saba Moshi, watu 15 wajeruhiwa

Nina wasiwasi na dereva,spidi ilikuwa kali sana katikati ya mji au alikuwa tayari kaanza xmass.Poleni wote walioumia.
Nikusaidie,

Kutoka round about ya YMCA kuelekea round about ya NBC kuna mteremko. Hivyo kwa jinsi inavyoonekana ni dhahiri hilo Basi lilifeli Breki na Dereva alijitahidi kunyooka na barabara maana kwa mazingira ya lile eneo asingeweza kulikita sehemu yeyote.

Na angefanikiwa kuizinguka hiyo round about basi angeweza kusimama bila kusababisha madhara makubwa maana kuna kampando kadogo baada ya huo mzunguko wa NBC kuelekea stendi.

Poleni wahanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dereva alivhukuliwe hatua kali sana iwe fundisho kwa wengine wazembe na waenda mwendo kasi kama yeye.
Huyo wamnyang’anye na leseni kabisa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Gari ilifeli breki,hata abiria wenyewe wamesema dereva alitoa taarifa mapema kwamba breki zimekataa...
Abiria wamempongeza dereva kwa kujitahidi kuokoa maisha yao....
 
Hizo ngoma zinafukuzagwa over speend hata katikati ya mji bila kujali alama za barabarani za 50kmph kutembelea mjini zinavyoelekeza.

Angelikuwa na mwendo wa 'kistaarab', kosa lolote la kiufundi lisingeweza kusababisha kuparamia magari yote hayo!

Halali yenu huyo dereva mvuta bhangi, mhangaike naye!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungekuwa unalijua hilo eneo nadhani usinge andika hicho ulichoandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gari ilifeli breki,hata abiria wenyewe wamesema dereva alitoa taarifa mapema kwamba breki zimekataa...
Abiria wamempongeza dereva kwa kujitahidi kuokoa maisha yao....


Ni nini kinachosababisha break ku fail?

Ni uzembe wa mmiliki wa gari na dereva.

Kwanini hawapeleki magari service regularly Kama inavyotakiwa?

Kwanini hawakubadilisha break pads?

Ni uzembe na uzembe lazima wawajibishwe wote dereva na mmiliki wa gari!

Waache kucheza na maisha ya watu!

Na iwe mfano kwa wengine wajifunze


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akilinjema,

Usihukumu bila ya kuwa una taarifa kamili.

Inawezekana pia kwamba gari limefanywa service vizuri tu, ila uzembe wa fundi ndio uliosababisha breki kufeli ghafla huku gari likiwa kwenye mteremko huo.

Uchunguzi wa polisi utatujulisha ni nani hasa aliyefanya makosa yaliyoisababisha ajali hii itokee.
 
Jamaa anaongea tu kwaajili ya kubishana,vitu vingine vinatokea tu bila sababu za moja kwa moja.
Mtu anaweza akatoka hospitali leo yuko vizuri,kesho inasikia amekufa.!@KakaBlaza,

Sent using my 6x6 bed.
 
Back
Top Bottom