Jamaa aliondoka home na 60$, akanunua mbuzi. Then akauuza kwa 70$.
Mfukoni akawa ana 70$. Akaona hii biashara mbona nzuri.
Akaenda mnadani akamuulizia yule mbuzi bei yake.
Wakamwambia tunakuuzia kwa 80$, jamaa akasema, "aahaa hawa wapuuzi yaani nimewauzia mimi wameshapandisha bei mara hii"
Haina noma. Akampigia simu rafiki yake niazime 10$. Kuna mbuzi hapa nichukue.
Akapewa 70$+10$(anatakiwa kuirudisha) jumla 80$.
Akanunua mbuzi. huyooo hadi kwa mangi, si kuna wakwe wamekuja.
Akamshaeishishi mangi kwa mbinde, mangi akanunua mbuzi kwa 90$.
Jamaa huyo akasepa zake. Akapitia kwa rafiki yake akamuachia 10$, uzuri alimpa bila riba. Akabaki na 80$.
Akafika home, mke akamuuliza wewe si uliondoka na 60$ mbona una 80$.
Jamaa akamjibu mkewe, mjini akili mke wangu nimefanya biashara nimepata 20$ kama faida.