Basilla Mwanukuzi: Wakweli hawatakiwi nchini. Uongozi wangu ni kuweka maslahi ya wananchi mbele hata ikibidi kukosa cheo

Basilla Mwanukuzi: Wakweli hawatakiwi nchini. Uongozi wangu ni kuweka maslahi ya wananchi mbele hata ikibidi kukosa cheo

Nimenukuu mwanzo-mwisho

""Na Basilla Mwanukuzi

KUNA CHA KUJIFUNZA

Aina yangu ya uongozi siku zote na muda wote ilijikita na itajikita katika kwanza kuweka mbele maslahi ya wananchi kwa gharama zote (hata ikibidi kukosa cheo)

2. Pili kuleta matokeo

Hakuna jambo kwangu ni hasara kama kua kwenye hali ya kutakiwa kuleta matokeo halafu kwenye mnyororo wa kuleta matokeo kuna watu wanaamua tu kua hayo matokeo sio shida zao...yani vile haraka ya nini??...hakuna matata...no hurry in Africa...ilihali wananchi wanaumia na kuteseka alafu na wewe ukaendelea kutulia tu kwenda na 'trend'

3. Kuleta matokeo kwa wakati
Muda ni kila kitu Serikali inafanya kazi kubwa MNO kuleta fedha kwa ajili ya wananchi inaleta fedha na muongozo mradi uishe ndani ya miezi 3. Inapaswa uishe ndani ya miezi 3 sana sana ukichelewa kidogo basi siku chache za nyongeza sio kama hapo ambapo ujenzi wa miezi 3 umechukua miaka 3 na fedha inaisha mradi haujaisha . Zahanati zote 3 . Wananchi wanateseka hawapati huduma
HAIKUBALIKI duniani wala mbinguni.

Uongozi ni dhamana, uongozi ni UTAKATIFU utakatifu uwe sio kwa mtu mmoja , ukiwa kwa mtu mmoja matokeo yake you will be THE ODD ONE OUT.
Uongozi ni UJASIRI

HASARA YA AINA HII YA UONGOZI (kama ni 'Hasara")
1. Utagombana na wote wenye maslahi yao hata ambao wanatakiwa kukuandikia taarifa zako (unaweza kuimagine watakachoamua kukuandikia ) kifupi utaharibiwa ma-file (uwe tayari)

FAIDA
Faida ni KUBWA ZAIDI utabaki na uadilifu wako na uaminifu wako , kwako , kwa nafasi yako, kwa mamlaka yako ya uteuzi, kwa WANANCHI, kwa Taifa lako, na kwa Mungu wako . Utakua na furaha na amani ya moyo

SWALI ambalo kila Mtanzania anatakiwa ajiulize kwa nini Mtandao wa wenye MASLAHI unanguvu ina maana kuna unakoanzia na kuna ukoishia. Ukideal na unakoishia unajikaanga na mbaya zaidi hata wanaotakiwa kuungana nguvu na wewe badala yake watakua wanaongeza mafuta ukaangike vizuri

Mwenyezi Mungu aendelee kumpa mwanga Mhe Rais wetu @samia_suluhu_hassan katika kuliongoza Taifa
Kumpa wasaidizi wenye mioyo safi kutoka kila NGAZI na kila IDARA na kuweka maslahi ya Taifa mbele. Ili tufike tunakotakiwa kufika kama Taifa

Instagra: basillamwanukuzi""
 
Ni busara ukiachia uongozi kukaa kimya. Tatizo watu wengi wakipewa nafasi, hawaamini ile nafasi ilishawahi kuwa na mtu mwingine ambaye labda alikuwa mzuri zaidi yake au inaweza kuchukuliwa na mtu mwingine yeyote. Ujumbe huu unaonesha ni mjinga.
Kwahiyo alichosema ni sahihi au sio sahihi! NB: Ukiachana na dhana ya wabongo kutopenda ukwel usemwe!!
 
Yeye alikuwa mkweli kwenye nini?
Snapped alichoongea so unaweza tafuta alikua mkwel kweny lipi nadhan Wananchi husika wapo waeza pata jibu. NB: ifike mahali kuna dhana tuachane nazo ili tusonge mbele, penye ukwel usemwe, penye hitilafu au mapungufu yasemwe, tusiwe taifa la kusifia sifia na unafiki mwingi. Hatuwatendei haki kizazi kijacho kwa jinsi yako!!
 
Ni busara ukiachia uongozi kukaa kimya. Tatizo watu wengi wakipewa nafasi, hawaamini ile nafasi ilishawahi kuwa na mtu mwingine ambaye labda alikuwa mzuri zaidi yake au inaweza kuchukuliwa na mtu mwingine yeyote. Ujumbe huu unaonesha ni mjinga.
Na ujinga mkubwa wa nchi hii,ni pale ambapo kila mtu anasujudu kwa mteule.

Kuna watu walikuwa na trend zao nzuri,ila wakatii mamlaka na kuzikubali teuzi hizi za sasa za ajabu ajabu.

Halafu unaondolewa kihuni kihuni.

Ndio sababu kuu ya chimbuko la sasa,ambapo baadhi ya wenye kunitambua wanakataa huo upuuzi wa uteuzi na kuamua kubaki kwenye tasluma zao.
 
Ni busara ukiachia uongozi kukaa kimya. Tatizo watu wengi wakipewa nafasi, hawaamini ile nafasi ilishawahi kuwa na mtu mwingine ambaye labda alikuwa mzuri zaidi yake au inaweza kuchukuliwa na mtu mwingine yeyote. Ujumbe huu unaonesha ni mjinga.
Akae kimya kwa faida ya nani? You are just advocating for cowardice. Shame on you!
 
Snapped alichoongea so unaweza tafuta alikua mkwel kweny lipi nadhan Wananchi husika wapo waeza pata jibu. NB: ifike mahali kuna dhana tuachane nazo ili tusonge mbele, penye ukwel usemwe, penye hitilafu au mapungufu yasemwe, tusiwe taifa la kusifia sifia na unafiki mwingi. Hatuwatendei haki kizazi kijacho kwa jinsi yako!!
Wanaofuatilia siasa za korogwe!
Waliofuatilia na kutunza kumbukumbu zake akiwa korogwe,wao wote wanafaha.u utendaji wake.
Ameelezea vizuri bila unafiki.soma bandiko lake na ulijibu ki ufasaha kulingana na alichokisema.
 
Poleni sana Ninyi akina mwanukizi mnajisikia sana. Mna makandokando kibao. Wakati mwingi mnaficha roho mbaya kwenye uadilifu. Mungu anawajua.
 
Wanaofuatilia siasa za korogwe!
Waliofuatilia na kutunza kumbukumbu zake akiwa korogwe,wao wote wanafaha.u utendaji wake.
Ameelezea vizuri bila unafiki.soma bandiko lake na ulijibu ki ufasaha kulingana na alichokisema.
Nadhan umedandia swali mwingine bila kujua namaanisha nn!! Soma tena comment yangu utaelewa!!
 
Snapped alichoongea so unaweza tafuta alikua mkwel kweny lipi nadhan Wananchi husika wapo waeza pata jibu. NB: ifike mahali kuna dhana tuachane nazo ili tusonge mbele, penye ukwel usemwe, penye hitilafu au mapungufu yasemwe, tusiwe taifa la kusifia sifia na unafiki mwingi. Hatuwatendei haki kizazi kijacho kwa jinsi yako!!
Uongo kama ule wa kuita ugonjwa wa covid ni "matatizo ya kupumua"?

Angetoa mfano mahsusi kama huo, kuwa aliongea ukweli gani ndio ukamponza, nimeona blah blah tu
 
Nadhan umedandia swali mwingine bila kujua namaanisha nn!! Soma tena comment yangu utaelewa!!
@Pac the Don
Samahani sana mkuu!nimekuelewa!
Kuomba msamaha ni moja ya Uzalendo uliotukuka

Tuendelee kama tunavyoendelea.
..pitia na hii nimekutana nayi humu,maana najua mods wa sasa!
hawakawii kuzitoa za hivi!
Kwa taarifa za uhakika kabisa ni kuwa waarabu wa Dubai na Saudia wanelekea kishiwa maeneo nyeti ya Taifa letu. Bandari ya Dar es Salaam tipo mbioni kukabidhiwa kampuni ya Dubai. Ndio maana jana mmeona Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE alikuwa Zanzibar kukamilisha mazungumzo, hamkuambiwa kwenye press ya Ikulu walizungumza nini.

Huu ni mwendelezo wa ziara ya yule mwana mfalme aliyekuja majuzi toka UAE akakutana na Pindi Chana Waziri wa kipindi kile wa maliasili ambaye aliondolewa siku mbili baadaye baada ya kuonekana mrasimu.

Kama haitoshi wizara ya maliasili akapelekwa waziri mkwe na Katibu Mkuu rafikiye ili wakamilishe madili na waarabu. Kama haitoshi Said Yakubu aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu pale Utamaduni akapandishwa Cheo kuwa Katibu Mkuu Utamaduni na leo hii yupo Saudi Arabia na Mwamfalme Binti eti wanaongea mambo ya utamaduni. Saidi huyu alikuwa msaidizi binafasi wa Ndugai ambaye maadili yake ni mashaka tupu, ni mbadhirifu na mdanganyifu na mpiga dili.

Kwa hili la UAE kupewa Bandari tayari kundi la kwanza la Wabunge lilipelekwa Dubai kuangalia namna hiyo Kampuni inavyoendesha bandari za huko na kundi la pili wanaenda India mwishoni mwa mwezi huu. Lengo ni kuwaziba midomo dili likikamilika kati kati ya mwaka huu.

Sikumpenda Magufuli kwa udikteta, wizi na ujambazi lakini angalau alijitahidi kulinda strategic resources za nchi kusalama kama bandari. Huyu wa sasa na hawa waarabu tunarudi enzi za Mwinyi na Loliondo. Nadhani tuutizame Muungano wetu vizuri pengine vya watanganyika vinafanywa kuwa vya bure pale mzanzibari anapokuwa rais.
 
Ni busara ukiachia uongozi kukaa kimya. Tatizo watu wengi wakipewa nafasi, hawaamini ile nafasi ilishawahi kuwa na mtu mwingine ambaye labda alikuwa mzuri zaidi yake au inaweza kuchukuliwa na mtu mwingine yeyote. Ujumbe huu unaonesha ni mjinga.
ANgekaa kimya tusingepata kujua. Hii ni faida kwa watu wengi. Knowledge is power!!!!!
 
Back
Top Bottom