Basilla Mwanukuzi: Wakweli hawatakiwi nchini. Uongozi wangu ni kuweka maslahi ya wananchi mbele hata ikibidi kukosa cheo

Basilla Mwanukuzi: Wakweli hawatakiwi nchini. Uongozi wangu ni kuweka maslahi ya wananchi mbele hata ikibidi kukosa cheo

Uongozi ni utakatifu.🙏🙏🙏

Uongozi wa Umma ni Utumishi sawa na Utumishi HEKALUNI, hivyo hutakiwi kusubiri kusimamiwa,

Unawajibika Kwa Mungu moja Kwa moja.

Kauli Yako, imehifadhiwa Kwa matumizi ya BAADAYE.

Aamen
 
@Pac the Don
Samahani sana mkuu!nimekuelewa!
Kuomba msamaha ni moja ya Uzalendo uliotukuka

Tuendelee kama tunavyoendelea.
..pitia na hii nimekutana nayi humu,maana najua mods wa sasa!
hawakawii kuzitoa za hivi!
Kwa taarifa za uhakika kabisa ni kuwa waarabu wa Dubai na Saudia wanelekea kishiwa maeneo nyeti ya Taifa letu. Bandari ya Dar es Salaam tipo mbioni kukabidhiwa kampuni ya Dubai. Ndio maana jana mmeona Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE alikuwa Zanzibar kukamilisha mazungumzo, hamkuambiwa kwenye press ya Ikulu walizungumza nini.

Huu ni mwendelezo wa ziara ya yule mwana mfalme aliyekuja majuzi toka UAE akakutana na Pindi Chana Waziri wa kipindi kile wa maliasili ambaye aliondolewa siku mbili baadaye baada ya kuonekana mrasimu.

Kama haitoshi wizara ya maliasili akapelekwa waziri mkwe na Katibu Mkuu rafikiye ili wakamilishe madili na waarabu. Kama haitoshi Said Yakubu aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu pale Utamaduni akapandishwa Cheo kuwa Katibu Mkuu Utamaduni na leo hii yupo Saudi Arabia na Mwamfalme Binti eti wanaongea mambo ya utamaduni. Saidi huyu alikuwa msaidizi binafasi wa Ndugai ambaye maadili yake ni mashaka tupu, ni mbadhirifu na mdanganyifu na mpiga dili.

Kwa hili la UAE kupewa Bandari tayari kundi la kwanza la Wabunge lilipelekwa Dubai kuangalia namna hiyo Kampuni inavyoendesha bandari za huko na kundi la pili wanaenda India mwishoni mwa mwezi huu. Lengo ni kuwaziba midomo dili likikamilika kati kati ya mwaka huu.

Sikumpenda Magufuli kwa udikteta, wizi na ujambazi lakini angalau alijitahidi kulinda strategic resources za nchi kusalama kama bandari. Huyu wa sasa na hawa waarabu tunarudi enzi za Mwinyi na Loliondo. Nadhani tuutizame Muungano wetu vizuri pengine vya watanganyika vinafanywa kuwa vya bure pale mzanzibari anapokuwa rais.
Upo sahihi hasa kwa upande wa JPM kweny issue kama hizi, but upande wa scenario ya mwanamfalme na kinachoendelea cna uhakika ingawa yamesemwa mengi san! Nadhan eventually kila jambo litakua wazi tu!
 
She is very arrogant in person. Sio sifa nzuri kwa kiongozi.

Asubiri kamba nyingine.
 
Pole basila, naona walijua kuwa wewe ni mweupe kichwani kutokana na historia ya CV yako!
Pole sana mama
 
Nimenukuu mwanzo-mwisho

""Na Basilla Mwanukuzi

KUNA CHA KUJIFUNZA

Aina yangu ya uongozi siku zote na muda wote ilijikita na itajikita katika kwanza kuweka mbele maslahi ya wananchi kwa gharama zote (hata ikibidi kukosa cheo)

2. Pili kuleta matokeo

Hakuna jambo kwangu ni hasara kama kua kwenye hali ya kutakiwa kuleta matokeo halafu kwenye mnyororo wa kuleta matokeo kuna watu wanaamua tu kua hayo matokeo sio shida zao...yani vile haraka ya nini??...hakuna matata...no hurry in Africa...ilihali wananchi wanaumia na kuteseka alafu na wewe ukaendelea kutulia tu kwenda na 'trend'

3. Kuleta matokeo kwa wakati
Muda ni kila kitu Serikali inafanya kazi kubwa MNO kuleta fedha kwa ajili ya wananchi inaleta fedha na muongozo mradi uishe ndani ya miezi 3. Inapaswa uishe ndani ya miezi 3 sana sana ukichelewa kidogo basi siku chache za nyongeza sio kama hapo ambapo ujenzi wa miezi 3 umechukua miaka 3 na fedha inaisha mradi haujaisha . Zahanati zote 3 . Wananchi wanateseka hawapati huduma
HAIKUBALIKI duniani wala mbinguni.

Uongozi ni dhamana, uongozi ni UTAKATIFU utakatifu uwe sio kwa mtu mmoja , ukiwa kwa mtu mmoja matokeo yake you will be THE ODD ONE OUT.
Uongozi ni UJASIRI

HASARA YA AINA HII YA UONGOZI (kama ni 'Hasara")
1. Utagombana na wote wenye maslahi yao hata ambao wanatakiwa kukuandikia taarifa zako (unaweza kuimagine watakachoamua kukuandikia ) kifupi utaharibiwa ma-file (uwe tayari)

FAIDA
Faida ni KUBWA ZAIDI utabaki na uadilifu wako na uaminifu wako , kwako , kwa nafasi yako, kwa mamlaka yako ya uteuzi, kwa WANANCHI, kwa Taifa lako, na kwa Mungu wako . Utakua na furaha na amani ya moyo

SWALI ambalo kila Mtanzania anatakiwa ajiulize kwa nini Mtandao wa wenye MASLAHI unanguvu ina maana kuna unakoanzia na kuna ukoishia. Ukideal na unakoishia unajikaanga na mbaya zaidi hata wanaotakiwa kuungana nguvu na wewe badala yake watakua wanaongeza mafuta ukaangike vizuri

Mwenyezi Mungu aendelee kumpa mwanga Mhe Rais wetu @samia_suluhu_hassan katika kuliongoza Taifa
Kumpa wasaidizi wenye mioyo safi kutoka kila NGAZI na kila IDARA na kuweka maslahi ya Taifa mbele. Ili tufike tunakotakiwa kufika kama Taifa

Instagra: basillamwanukuzi""


😍😍
 
Huyo dada yupo vizuri kipesa kitambo.

Ana urithi wa kutosha tu wa mijengo prime areas.

Kabla hajateuliwa tu alikuwa anaendesha gari za gharama kuliko v8
Alikua na chuma plate namba kaweka jina lake BASILA MWANUKUZI ilikua European car Jeep moja matatraa.
Extrovert mzee wa European cars aje kutia neno.
 
Wabongo bwana wanafikiri kila mtu anayekubali hizo teuzi ni kwamba ana njaa sana. Basila ni LG kitambo sana.
Waporipori na watoto wadogo ndiyo anaweza kuwa mgeni masikioni mwao
 
NIMETOKA KAPA KWA MARA KWANZA HUMU JF SIJAELEWA KITU KWENYE ANDIKO SIONI KITCHWA SIONI MGUU SIONI KIWILIWILI,🚮🚮🚮
 
Hiyo ni taarifa.
Huyo dada anapaswa kwa sasa kutulia. Alipewa cheo kama fadhila (hakuwa na vigezo vyovyote vya msingi kijamii au kisiasa kutumikia umma), leo ametumbuliwa analalamika kimtindo kuwa ameonewa, kwanini alipopewa cheo hakukikataa na kusema amependelewa?

Aliyemteua hapo awali ndiye yule yule aliyemtumbua, kuna kipi cha ajabu?

Kama anaamini ana uwezo mkubwa wa kuitumikia jamii, aitumikie sasa jamii akiwa mtu huru, asilalamike tena, sio lazima awe DC ndio aitumikie jsmii.
We jamaa sikuwahi kujua na wewe huwa unatetea WEZI!
 
Anasemaje huyu ? Asifikiri watu walikua hawamjui? Amesahau alichomfanya William Mngazija ?
Amefanya nini Cha ajabu tangu aje hapa?
Korogwe ndio mji pekee hapa duniani ambao katikati yake kunapita mto wenye maji mengi yanayozalisha umeme, lkn Korogwe HAKUNA MAJI YA BOMBA. MIAKA HII MITANO YA BASILA NDIO SHIDA YA MAJI IMEFIKIA KILELENI.
A kwendre huko.....
Sasa hio shida ipo tokea uhuru sasa huyo basila ana nn mpakaaimalize ndani ya miaka mitano?
 
Back
Top Bottom