Bastola iliyoua wawili Sinza ni dili kishirikina, lakini pengine pia imebeba mikosi na laana

Mshana kwa hiyo haya magari used ya Beforward na SBT ambayo sisi tukinunua tunaita gari mpya tuachane nayo?
Mkuu ukisoma uzi wa Mshana almost 99.9% umejitosheleza. Nashangaa watu sijui hamsomi vizuri,hamuelewi au ndo namna gani sielewi nyie mnakwama wapi.

Kwa swali lako hili nikusaidie. Usiachane nayo amesha sema nenda kaliombee,bariki au Takasa kwa imani yako. Sisi RC tunaenda kumuona Padri ataliowekea baraka na kuondoa hayo mazaga na maagano incase kama yatakuwepo. Iyo ni kwa upande na kulingana na Imani yangu.
 
Jamaa inasemekana juzi alisherekea birthday yake kwenye cack kulikuwa na picha ya bastola sasa bado anazidi kuibua mijadala alikuwa na maana gani
 
Natamani kuona hiyo attachment, lakin alas! Imepigwa spana.
 
Na birthday yake ilikuwa tar13, tarehe inayoogopwa mno na wazungu.. Zaidi mdogo wake alikufa last month same date
Basi hiyo family kuna shida mahali kuna kitu kinawafuata.
Ila kitaalam silaha inaendana na damu au jadi fulani kuna koo zikishika vitu kama hivyo zinaamsha kichaa.
Nakumbuka kipindi niko jkt kuna jamaa kipindi ha gwaride la silaha jamaa akipokea tuu silaha anaamsha mashetani
 
wanasema tusiyasema vibaya ya marehemu lakini huyo jamaa wala siyo,alishawahi kumshika mke wa jamaa yangu tako hapo hapo jamaa akamaind ba bomba juu ikatolewa he deserve kwa hukum aliyojipa
 
Kwa hiyo silaha inapaswa isiue mtu si ndio?

Tena hiyo mie ningekuwa nahitaji ningeinunua maana inaonyesha unapiga kazi nzuri.

Kuna vibaka wapuuzi kila siku wanapita kudokoa kitu nyumbani kwangu na wameniulia mbwa kwa sumu. Hawa ningekuwa nahitaji silaha ningeinunua hiyo Glock nimtoe mtoto wa mtu makalio.

Tatizo nimepita mafunzo ya jeshi huko nyuma hivyo naelewa namna silaha inaweza kukupa akili mbovu, au namna ambavyo mtu innocent anaweza kujidhuru kama ataikuta sehemu.

Pia silaha unajifanya use mtumwa kuitunza na kuilinda kila wakati, ukishazoea kuwa nayo mpaka kiuno kinakuwa na sugu. Siitaki.
 
MBNA mshana kaeleweka vzuri sana sema tu watu mnataka kucomplicate mambo ila jamaa kafafanua vzuri sana
 
wanasema tusiyasema vibaya ya marehemu lakini huyo jamaa wala siyo,alishawahi kumshika mke wa jamaa yangu tako hapo hapo jamaa akamaind ba bomba juu ikatolewa he deserve kwa hukum aliyojipa
Mmh kuna kilichokuwa kinamtafuta kumbe
 
Tuliwahi kununua bastola pale Obay na raia mmoja wa nje.. Shida tulizopata na ile silaha sitakaa nizisahau....kuja kupata historia yake ya kweli niliogopa na kutishika mno...
Alafu nimesikia mmoja wa marehemu tarehe alokufa ndo hiyohiyo alikufa mdogo wake mwaka jana
Hii imekaaje
 
Yeah hii ni kweli kabisa .. Jamaa yetu chuoni alikuwa hashiki kisu na hilo liko kwenye familia yao.. Yaani anakwambia wakishika visu lazima viwakate tena hasa
 
Kwa Mila zetu sisi tunaamini kama uliuua na kunyang'anya mtu siraha nawe itatoka kama ulivyoipata. Kama uliipata kwa maumivu nayo itatoka kwa maumivu, tutumie busara na kuchunguza kwa umakini vitu tunavyonunua.
Mshana Jr amenena vyema kabisa

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
[emoji817][emoji736][emoji1545]Asante sana Kwisense
 

Wewe unaamini kwamba Bastola ndiyo itakulinda?

Kama Sio mtu wa Mambo ya Ulinzi Na Usalama , silaha unayomiliki kama hujaua nayo mtu basi itakuuwa wewe, yaani put that on note.

History inaonesha wazi Raia wengi wanaomiliki Bastola ni aidha Ina wamaliza au inamaliza wengine for no reason. Nina miliki Bastola lakini kwa sababu ya nature ya kazi yangu inanitaka hivo. Na kuna siku almanusura ilitaka kunimalizia kiumbe changu. I totally discourage mtu kumiliki Bastola kwa matumizi ya kawaida, eti kwa kigezo cha kulinda mali zangu nyumbani.

Bastola hailindi mali zako, watu wakiamua kukufanyia unyama wanakufanyia Na Bastola yako .... maana it is all about timing. Erasto msuya alikuwa na Bastola , ilimsaidia ?kila siku tunasikia polisi na wanajeshi wanapigana Bastola for no reason. Yaani mtu anakuja ofisi and Yupo desperate, anafika na kulipua wenzie, na haijulikani sababu ni nini. Ndiyo ipo Hivyo, ni vile tu haitakiwi kutangazwa. Lakini jeshini na polisi matukio hayo ni kawaida sana

Kwanza Bastola zenyewe mnazomiliki ni hizi za Taa, halafu inajikoki tena for more that 30sec, ndio usikie tena Taa ..yaani ina shout then Ina reload . .., wakati yako ina reload , mwenzio kashakupiga mwili mzima.

Ditopile aliulizwa, Dito kwa nini umemuua huyu maskini, alijibu kwa hakika hakukusudia kumuua bali alitaka kumtisha Tu, wakati ana knock kioo cha gari kwa kutumia Bastola, trigger ikajiset na kujiachia.... !

Bastola kama haijakuua basi utaua wengine hata kwa bahati mbaya. Na ukishaua mtu huwezi kuwa sawa sawa tena. Sishauri kabjsa kama Sio mtu wa ulinzi na usalama. Ishi vyema na watu, epuka wizi wizi, na ubishi ubishi usio na msingi, usiweke bifu na watu. Asilimia 80 yetu ni mania Bipolar , akiwa kwenye moody, atafanya kisha kujuta. Wengi wetu ni machizi wasomi so be careful
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…