Ndiyo mana Trump haipendi Africa na waafrica wenyewe, ameenda mbali zaidi kwamba hata mtu mweusi hamuamini kabisa, ni kwasababu ya upuuzi kama huu, watu wanajua kabisa Rais wa sasa ni incompetent lkn wakikumbuka aliyepita alikuwa smart na kuwakosesha ulaji kwa nia ya kuleta usawa katika jamii wakaona waende na huyu huyu ili upigaji wao uendelee, huu unaitwa ubinafsi wa mtu mweusi.
Mwanzoni nilikuwa simuelewi kabisa Trump ila baadaye nikagundua yupo sahihi kabisa, Africa ni upuuzi sn unaendelea, yn hatutokuja tuendelee hata iweje, na aliyesababisha hilo wala sio mzungu bali ni roho mbaya ya mtu mweusi, tuko hivyo na nafikiri tuliumbwa hivyo na haitobadilika.
Kuna scenario nyingi sn zinazoonesha udhaifu wa mama lkn wakubwa baada ya kugundua hilo wameajiri machawa kumnadi mama, yn uchawa kwa sasa ndiyo mpango mzima, mpaka mawaziri wamekuwa ndiyo machawa wa kwanza kabisa, ukitaka kuamini udhaifu wa mama jiulize kwann inatumika nguvu kubwa kumnadi ilihali hakuna upinzani wowote? Kama wewe ni CCM ukijaribu kupinga hata kidogo unafukuzwa kabisa chama na ukileta chokochoko unaweza kutolewa uhai kabisa, watu wana jambo lao.
Mama hana anachokijua kabisa wallahi, hivi sasa hata kwenye suala la ajira serikalini, taasisi karibu zote za umma zinaajiri zenyewe, sasa nini maana ya kuwepo UTUMISHI? hivi kwa huu ubinafsi uliopo hapa Africa unategemea kitatokea nn?
Ndugu zangu tushukuru Mungu alipita hayati nchi hii, la sivyo hata haya maendeleo machache tuliyonayo tusingeyapata kabisa, na kiukweli yanawapa wakati mgumu sn kumaliza, so wameapa kutorudia kosa.