Mkuu, haujanipata vizuri.
Kwenye hiyo miradi na wao wenyewe WB au IMF wanakuwa na kipengele cha kuchagua mkandarasi wao wenyewe. Serikali inabaki kama msimamizi tu. Kama ni ulaji ni hayo makampuni ya ujenzi na hizo taasisi za fedha ndio wanajua namna ya kupiga hizo hela. Na ndio maana waziri kasema inabidi aihusishe foreign affairs kulingana na situation ilivyo.
Hata jangwani, bado hamna kitu japo WB walishasema wanaweka fedha pale. Hizi taasisi za fedha zinatoa mikopo na bado zinakupangia namna ya kutumia mkopo kama ni wamekupa msaada vile. Shida ndio iko hapo.
Kwani si ujinga wetu, kwamba Sh. 500bn ni za kusubiri bakuli.
Mbona walimfanyia hivyo mzee kwenye JNHPP ila akakaza na domestic revenue $3bn bwawa hilo hapa.
Alikaza Kimara Kibaha Highway tunayo, alikaza Stands tunazo.
Alikaza Magufuli Bridge na mfuko wa Nchi Daraja hilo.
Ni misplaced priority tu, Jangwani under 100bn unasubiri bakuli.
Kibaha Chalinze unasubiri PPP, yaani unasubiri upuuzi.
Muda huo huo 300bn zinateketea kwenye magari ya serikali (Yaani Toyota Reliable and durable car) unataka ibadilisha ndani ya mwaka huku.kuna mwananchi wako ana Land cruiser ya AKV bado ngumu kuliko STM ya serikali ambayo imeanza kuchoka.
Hii miradi funga mkanda kaza kama mradi wa 500bn forecast ya kujenga ni 3 years, kila mwezi mapato ya Kodi 3 Trillion, kubaliana na mkandarasi unamlipa kiasi flani kila mwezi mfano 20 bilion kwa kipindi cha miaka 3, mradi huu hapa.
Kwa hiyo wapo.radhi kutolipa.kwa installment ila wanasubiri.mkopo wa 500bn ambao utaulipa miaka 30 na masharti mengi hadi Mkandarasi wao.ambaye atachukua hizo pesa na kuzirudisha nchini kwao.
Badala ya kujikaza 3yrs na pesa yako, Mkandarasi wako, masharti yako.ambayo yanaweza fanya ajira na mzunguko.wa pesa kuwa mzuri.nchini.
Misplaced priorities ndio tatizo.
Yaani 10bn utasikia zinakopewa, na mwezi.ukiisha unasikia.matarumbeta serikali ya Mama imekusanya 3trilon record huku.unakopa 10bn usenge.