Battle kati ya Fiesta na Wasafi Festival

Battle kati ya Fiesta na Wasafi Festival

Kwani hadi wasafi festival wameshanyonywa?? Hhahahaha wabongo bana
Wasafi Festival hivi itakuwa inajumuisha wasafi tu au na wasanii wengine?
Kama na wasanii wengine watahusishwa sitoshangaa kusikia malalamiko kuwa wasanii wanalipwa pesa ndogo na hapo ndipo utashangaa iweje aliyekuwa analalamika kunyonywa na Ruge naye ananyonya wengine kama ambavyo imetokea kwa Rich Mavoko.
Wasanii uwa sijui wanakuwa wamezibwa macho wakati wakuingia mikataba maana uwa nashangaa mkataba asaini yeye halafu aje kusema ananyonywa.
 
Kwani hadi wasafi festival wameshanyonywa?? Hhahahaha wabongo bana
Mimi sijaongelea wasafi festival mkuu nimeongelea tukio la Rich Mavoko kujiondoa WCB kwa kusemekana kwamba ananyonywa, hapo fikiria label ndo kwanza ina wasanii hata 8 hawafiki lakini ishaanza mambo ya kudai wananyonywa. Je vipi ije kuwa wanaaanda event kubwa kama ya fiesta ambapo wasanii ni zaidi ya 25 unahisi haya maneno hayatoibuka?
Wajua wasanii sijui uwa wanasaini mikataba wakiwa wanawaza jukwaa na shangwe halafu wakishamaliza perform ndipo wanaanza kutafakari.
 
Back
Top Bottom