-Daaah!...ni kwa Mara nyingine tena wale manguli na mahasimu wa BONGOFLEVA nchini...yani ALIKIBA (Ali Saleh Kiba) na DIAMOND PLATNUMZ(Naseeb Abdul Juma) wamekutana kwenye TUZO ZA KIMATAIFA za AFRIMMA AWARDS wote akiwania category moja ya "BEST MALE ARTISTE IN EASTAFRICA",Najua teamondi hawaamini na ni ngumu kwao kukubali ila ndo ivyo tena jamaa(KIBA) ndo kashavuka mipaka ya TANZANIA nayeye...hivyo muache kejeli na dharau,Najua mwaka huu AFRIMMA watashangazwa na mvua ya KURA zitakazopigwa ambayo haijawai kutokea kabla na hasa zikitokea TZ na kama kwenye hizi TUZO wao wanapiga pesa basi ni wazi hawatosita kuwarudisha hawa jamaa tena mwakani kwenye kinyanganyiro hicho.
-Haya sasa kipenga kimeshalia "TEAMKIBA" na "TEAMMONDI"... Let's go!!!!!
CHANZO:
Nominees 2015 |
Kweli ushabiki wa team katika bora wake!
Jamani mambo haya ndio yaliyotufanya juzi south afrika tukaambulia tuzo moja tu. Thanks to Naseeb (Diamond) Mungu akuweke.
Kwenye hizo Afrimama award kuna watanzania wengi wamekuwa nominated jamani kuna (bi Khadija Kopa, Vanesa Mdee, Mrisho Mpoto, Ommy dimpoz, Lady Jeydee, na produzer mmoja nimesahau jina) Hawa wote wanahitaji kura zetu sisi watanzania.
Utoaji huu wa habari unavunja moyo unakatisha tamaa washiriki wengine na hata wapiga kura maana sisi wengine hatumo kwenye hizo team zenu so ukianza na habari hizo mwingine haoni sababu ya kuingia kwenye matusi wengine sijui ndio mnajifunza kuongea matusi kwenye hizo team ndiko mnakofanyia practical. Unawafanya watu wasipige kura. Kwa kutokufanya hivyo unawanyima washiriki fursa nyingine ya kutoka. Tuwe more practical and real.
Kitu kingine Naseeb ameingia kwenye category 7 my dia lakini Aly kaingia category moja tu ambayo pia Naseeb yumo mnavyochochea hivyo si afya kwa hawa wasanii na kazi zao lakini pia si afya kwetu sisi watanzania tutachochea mwisho wa siku nchi nyingine ichukue tukose.
Tijipange ili vijana hawa wachukue tuzo tena ikiwezekana category zote ambazo watz wapo tupige kura tuzo zote zije tanzania tunaweza na itawatia moyo sana wasanii wetu. Sio kuwaza ugomvi tu.
Team hizo ziwe kwa faida yao na iwe furaha kwetu watanzania tujivunie uwepo wao.
Mjue kwenda kwao huko kunafungua fursa kwa watanzania sidhani kama Naseeb na Vanessa juzi south africa walienda wao peke yao lazima walienda na watu, waliokutana na mataifa mengine so kuna kitu wameongeza hao be wide kichwani.
Yangu ni hayo. ....... Haya kampigie kura watanzania tuzo zije nyumbani.