Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Mwanza Inakuwa haraka sijui kwa nn yaani kwa sababu watu wengi wanahamia kule.MNAPATA NGUVU WAPI YA KUIFANANISHA MWANZA NA ARUSHA? SIJAWAHI KUANDIKA KITU KWENYE HUU UZI LAKINI MWANZA IMEIACHA ARUSHA KWA VIWANGO VINGI SAANA...
MIMI NI MSWAHILI NIMEZALIWA HAPO MBELE KIDOGO YA SHULE YA THAQAFA KARIBU NA HOTEL YA PIGEON, JIRANI KABISA NA SOKO LA MILONGO....
NIMEKAA ARUSHA MUDA KIDOGO KWA MIAKA 4 NIKAENDA MOSHI THEN NIKARUDI ARUSHA KWAHIYO ARUSHA NAIJUA KWA KIASI CHAKE.....
LAKINI NI DHAMBI KUBWA SAANA KUIFANANISHA MWANZA NA ARUSHA, ARUSHA ni mkoa ambao umejaa pride sana ushamba mwingi tofauti kabisa na watu wa Mwanza, ukipata tajiri wa ARUSHA misifa mingiii akiingia sehemu atataka ajilikane yeye, tofauti na ndugu zangu wasukuma unaweza kukutana na Don hata usimdhanie (ni kwa sababu ya life style yao wengi wao, too humble)..
Wazee Mwanza inakua vibaya mno, mimi NIMEZALIWA mjini kati, tokea ghorofa lililokuepo la kishimba miaka hiyo, kwa macho nashuhudia maendeleo makubwa sana, mpaka muda mwingine nawaza vipi kusingekua na milima?....nadhani mabatini, nyambiti. Nyamhuge ingekua ni mijengo mitupu, maana mtu wa nyamhuge kufika town kwa kupitia mabatini but kutokana na milima anazungukia maduka 9 au buzuruga.....
Mwanza Bado inapumua, zamani tulikua na mashamba huko nyasaka sio zamani saaana miaka ya 2000 tulikua tunaenda kulima viazi, nimerudi kushangaa Nikabaki kucheka mwenyewe...
Nimechoka Kuandika Lakini juzi kati navuka maji naenda sengerema nilikaa na wakili mmoja akasema juzi kati amefunga mkataba HAPO capripoint milimani mtu kanunua kiwanja kwa million 900...Just imagine sio kiwanja ni mawe, Bado gharama za kusawazisha.
Nina hakika Wapiga Domo wengi wa huko Arusha wakipewa viwanja Bure Hapo capripoint hawatakua na uwezo wa kujenga kitu maana levelling tu, ni gharama ya kujenga stand mpya.
Uliposema matajiri wa mwanza uko sahihi ni wakimya na wapo wengi hata mitandaoni huwezi kuwakuta ila Wana pesa ndefu ila ni madogo tu ...Ila Arusha duh jamaa kwa sifa na ushamba ni noma mtu ana million 20 bank basi anaanza kuita wenzie maskini mara "Tafuta pesa" ..
Yaani nawaonaga washamba sana