Battle: Mwanza (The Rock City) Vs Arusha (A-Town/Chuga)

Battle: Mwanza (The Rock City) Vs Arusha (A-Town/Chuga)

MNAPATA NGUVU WAPI YA KUIFANANISHA MWANZA NA ARUSHA? SIJAWAHI KUANDIKA KITU KWENYE HUU UZI LAKINI MWANZA IMEIACHA ARUSHA KWA VIWANGO VINGI SAANA...

MIMI NI MSWAHILI NIMEZALIWA HAPO MBELE KIDOGO YA SHULE YA THAQAFA KARIBU NA HOTEL YA PIGEON, JIRANI KABISA NA SOKO LA MILONGO....

NIMEKAA ARUSHA MUDA KIDOGO KWA MIAKA 4 NIKAENDA MOSHI THEN NIKARUDI ARUSHA KWAHIYO ARUSHA NAIJUA KWA KIASI CHAKE.....

LAKINI NI DHAMBI KUBWA SAANA KUIFANANISHA MWANZA NA ARUSHA, ARUSHA ni mkoa ambao umejaa pride sana ushamba mwingi tofauti kabisa na watu wa Mwanza, ukipata tajiri wa ARUSHA misifa mingiii akiingia sehemu atataka ajilikane yeye, tofauti na ndugu zangu wasukuma unaweza kukutana na Don hata usimdhanie (ni kwa sababu ya life style yao wengi wao, too humble)..

Wazee Mwanza inakua vibaya mno, mimi NIMEZALIWA mjini kati, tokea ghorofa lililokuepo la kishimba miaka hiyo, kwa macho nashuhudia maendeleo makubwa sana, mpaka muda mwingine nawaza vipi kusingekua na milima?....nadhani mabatini, nyambiti. Nyamhuge ingekua ni mijengo mitupu, maana mtu wa nyamhuge kufika town kwa kupitia mabatini but kutokana na milima anazungukia maduka 9 au buzuruga.....

Mwanza Bado inapumua, zamani tulikua na mashamba huko nyasaka sio zamani saaana miaka ya 2000 tulikua tunaenda kulima viazi, nimerudi kushangaa Nikabaki kucheka mwenyewe...

Nimechoka Kuandika Lakini juzi kati navuka maji naenda sengerema nilikaa na wakili mmoja akasema juzi kati amefunga mkataba HAPO capripoint milimani mtu kanunua kiwanja kwa million 900...Just imagine sio kiwanja ni mawe, Bado gharama za kusawazisha.

Nina hakika Wapiga Domo wengi wa huko Arusha wakipewa viwanja Bure Hapo capripoint hawatakua na uwezo wa kujenga kitu maana levelling tu, ni gharama ya kujenga stand mpya.
Mwanza Inakuwa haraka sijui kwa nn yaani kwa sababu watu wengi wanahamia kule.

Uliposema matajiri wa mwanza uko sahihi ni wakimya na wapo wengi hata mitandaoni huwezi kuwakuta ila Wana pesa ndefu ila ni madogo tu ...Ila Arusha duh jamaa kwa sifa na ushamba ni noma mtu ana million 20 bank basi anaanza kuita wenzie maskini mara "Tafuta pesa" ..

Yaani nawaonaga washamba sana
 
Nimechoka Kuandika Lakini juzi kati navuka maji naenda sengerema nilikaa na wakili mmoja akasema juzi kati amefunga mkataba HAPO capripoint milimani mtu kanunua kiwanja kwa million 900...Just imagine sio kiwanja ni mawe, Bado gharama za kusawazisha.

Nina hakika Wapiga Domo wengi wa huko Arusha wakipewa viwanja Bure Hapo capripoint hawatakua na uwezo wa kujenga kitu maana levelling tu, ni gharama ya kujenga stand mpya.

Arusha ndiyo sehemu pekee hapa Duniani ina 'Mabilionea' wengi zaidi kuizidi China na US .Uliza sasa hao Mabilionea wanamiliki kiasi gani in terms of Assets na Cash utachoka mwenyewe [emoji23][emoji23][emoji23]

Mziki wa kununua viwanja Capri point umewapa mtihani mkubwa sana 'Mabilionea' wa Arusha hawauwezi kamwe.
 
Nimefuatilia hii battle, naona nami nitoe fikra yangu:

Nimezaliwa na kukulia Arusha, na nimepata bahati kutembea Mwanza pia. Mara ya kwanza kufika Mwanza nilishangaa, kuona maendeleo ya jiji hilo, tofauti sana na nilivyokuwa nikifikiria.

Hata hivyo siwezi kulinganisha Mwanza na Arusha kwa sababu ni majiji mawili yasiyofanana kwa namna yoyote tofauti na kuwa wenyeji wazawa ni wafugaji, lakini zaidi ya hapo hakuna.

Arusha ina hadhi yake tofauti sana na maeneo mengine. Kwenye miaka ya 90 kila mtu alikuwa anatamani kufika Arusha, ulikuwa ni mji wenye hadhi kimataifa na ndio kupewa jina la Geneva of Africa.... sema tu hizi siasa zetu zimevuruga mambo, sipendi kutaja majina, ila kama Arusha ingeendelea na maendeleo yake kwa sasa ingekuwa ni kitu kingine kabisa.

Kwa vile tunapima maendeleo ya miji yetu kwa wingi wa majengo na maghorofa, ni kweli Mwanza imeiacha Arusha kwa mbali sana, itachukua muda mrefu kwa Arusha kuwa na Majengo mengi kama Mwanza, hata hivyo kuna hali fulani hivi unaipata ukiwa Arusha, ambayo huipati Mwanza wala miji mingine.

Mazingira ya Arusha yanakukaribisha kutuliza nafsi yako, amazing. Hali ya baridi na uoto wake unafanya kunakuwa na mazingira ya kukukaribisha kutuliza moyo. Nakutana na wageni kutoka Ulaya na nchi za majangwa wanaisifia Arusha.

Ukizungumzia hali ya "sifa" ya watu wa Arusha, ni kweli, watu wetu hujiona wapo level nyingine tofauti na watanzania wengine, hasa ikiwa mtu ameishi Arusha maisha yake yote, akitoka nje anajihisi tofauti sana. Inawezekana hali hii ni kwa sababu ya ukanda wenyewe, kwa sababu ni hali tunaiona pia kwa wakenya.

Kwa kuwa uchumi wa Arusha ulitegemea sana biashara ya madini ya Tanzanite, waliokuwa na migodi na wachimbaji, walipopata mawe na kuuza kwa bei kubwa, walitaka kujulikana mjini, wakaweka misafara ya wapambe na kwenda sehemu za starehe, ambako walijipa uwezo wa kufanya chochote, hata kuchukua msichana wa mtu na uliyechukuliwa ukakaa kimya.

Pakawa na majina makubwa mjini, wao ndio wenye mji, ikasemwa kuwa hawakukubali kufunikwa na wengine. Ikawajengea hofu wafanyabiashara wengine kuwekeza Arusha. Hali hiyo bado ipo akilini mwa watu hadi leo hii, kuwa wanaiogopa Arusha.

Yote na yote, siioni Arusha ikiwa na Maghorofa meengi kama Mwanza, ila kuwe na mazingira rafiki zaidi ya uwekezaji kuendelea kukaribisha watu kutoka mataifa yote duniani kama ilivyo sasa.

Arusha itaendelea kuwa taswira ya Tanzania kimataifa.
 
Arusha ndiyo sehemu pekee hapa Duniani ina 'Mabilionea' wengi zaidi kuizidi China na US .Uliza sasa hao Mabilionea wanamiliki kiasi gani in terms of Assets na Cash utachoka mwenyewe [emoji23][emoji23][emoji23]

Mziki wa kununua viwanja Capri point umewapa mtihani mkubwa sana 'Mabilionea' wa Arusha hawauwezi kamwe.
Capripoint unaweza kuifananisha ata na njiro ya zamani? 🤣 🤣 Washamba bana. Nilikuwa ndugu tena wa damu hapo karibu na hiyo sijui yatch club ushuzi hapo anakwambia mwanza bado sio kama Arusha, sasa ni marehemu rip na alikuwa na viwanda vya kusindika samaki na last time alikuwa anaidai bugando supplies za almost a billion. Wanae wawili wakiume wametimkia arusha mwanza wanaona shambani tu, true story.
 
Capripoint unaweza kuifananisha ata na njiro ya zamani? [emoji1787] [emoji1787] Washamba bana. Nilikuwa ndugu tena wa damu hapo karibu na hiyo sijui yatch club ushuzi hapo anakwambia mwanza bado sio kama Arusha, sasa ni marehemu rip na alikuwa na viwanda vya kusindika samaki na last time alikuwa anaidai bugando supplies za almost a billion. Wanae wawili wakiume wametimkia arusha mwanza wanaona shambani tu, true story.
Ngoja tukuambie ukweli sasa.Hebu acha kumdhalilisha huyo ndugu yako na hiyo supplies ya 1bn Bugando.Hizo biashara za huo mzunguko wanafanya vijana wadogo wadogo na ni wengi tu huko Ziwani na no one even cares kama ni Mabilionea.

Hao wanae waliotimkia Arusha ni wanajua vizuri mziki wa Mwanza hawauwezi,wamerudi huko kwenu ambako kila alie na 200M ni 'Bilionaire'[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Capripoint unaweza kuifananisha ata na njiro ya zamani? 🤣 🤣 Washamba bana. Nilikuwa ndugu tena wa damu hapo karibu na hiyo sijui yatch club ushuzi hapo anakwambia mwanza bado sio kama Arusha, sasa ni marehemu rip na alikuwa na viwanda vya kusindika samaki na last time alikuwa anaidai bugando supplies za almost a billion. Wanae wawili wakiume wametimkia arusha mwanza wanaona shambani tu, true story.
Mbona mna stress sana nyie watu wa Mwanza mnaolazimisha ifanane na Arusha? 🤪🤪
 
Hakuna nyumba ya maana hapo ata moja, hizo njiro wanakuona kima tu. Nyie nyie. Embu kwanza zile picha mbili sijui nimewawekea mnatafutana.
Ni kweli kabisa Mkuu,Njiro kuna mijengo ya maana kweli [emoji23][emoji23][emoji23]
Screenshot_20230221-135024_Chrome.jpg
Screenshot_20230221-134902_Chrome.jpg
Screenshot_20230221-134918_Chrome.jpg
 
Capripoint unaweza kuifananisha ata na njiro ya zamani? 🤣 🤣 Washamba bana. Nilikuwa ndugu tena wa damu hapo karibu na hiyo sijui yatch club ushuzi hapo anakwambia mwanza bado sio kama Arusha, sasa ni marehemu rip na alikuwa na viwanda vya kusindika samaki na last time alikuwa anaidai bugando supplies za almost a billion. Wanae wawili wakiume wametimkia arusha mwanza wanaona shambani tu, true story.
Kwanini mnapenda sana maneno mengiii kuliko vitendo, unaposema njiro kuna watu hawaijui ingekuwa vema kama ungeleta picha za njiro, battle za maneno tuwaachie wakina ashura ndala ndefu na wakina amina kidawa.
 
Back
Top Bottom