Battle: Mwanza (The Rock City) Vs Arusha (A-Town/Chuga)

Mwanza Inakuwa haraka sijui kwa nn yaani kwa sababu watu wengi wanahamia kule.

Uliposema matajiri wa mwanza uko sahihi ni wakimya na wapo wengi hata mitandaoni huwezi kuwakuta ila Wana pesa ndefu ila ni madogo tu ...Ila Arusha duh jamaa kwa sifa na ushamba ni noma mtu ana million 20 bank basi anaanza kuita wenzie maskini mara "Tafuta pesa" ..

Yaani nawaonaga washamba sana
 

Arusha ndiyo sehemu pekee hapa Duniani ina 'Mabilionea' wengi zaidi kuizidi China na US .Uliza sasa hao Mabilionea wanamiliki kiasi gani in terms of Assets na Cash utachoka mwenyewe [emoji23][emoji23][emoji23]

Mziki wa kununua viwanja Capri point umewapa mtihani mkubwa sana 'Mabilionea' wa Arusha hawauwezi kamwe.
 
Nimefuatilia hii battle, naona nami nitoe fikra yangu:

Nimezaliwa na kukulia Arusha, na nimepata bahati kutembea Mwanza pia. Mara ya kwanza kufika Mwanza nilishangaa, kuona maendeleo ya jiji hilo, tofauti sana na nilivyokuwa nikifikiria.

Hata hivyo siwezi kulinganisha Mwanza na Arusha kwa sababu ni majiji mawili yasiyofanana kwa namna yoyote tofauti na kuwa wenyeji wazawa ni wafugaji, lakini zaidi ya hapo hakuna.

Arusha ina hadhi yake tofauti sana na maeneo mengine. Kwenye miaka ya 90 kila mtu alikuwa anatamani kufika Arusha, ulikuwa ni mji wenye hadhi kimataifa na ndio kupewa jina la Geneva of Africa.... sema tu hizi siasa zetu zimevuruga mambo, sipendi kutaja majina, ila kama Arusha ingeendelea na maendeleo yake kwa sasa ingekuwa ni kitu kingine kabisa.

Kwa vile tunapima maendeleo ya miji yetu kwa wingi wa majengo na maghorofa, ni kweli Mwanza imeiacha Arusha kwa mbali sana, itachukua muda mrefu kwa Arusha kuwa na Majengo mengi kama Mwanza, hata hivyo kuna hali fulani hivi unaipata ukiwa Arusha, ambayo huipati Mwanza wala miji mingine.

Mazingira ya Arusha yanakukaribisha kutuliza nafsi yako, amazing. Hali ya baridi na uoto wake unafanya kunakuwa na mazingira ya kukukaribisha kutuliza moyo. Nakutana na wageni kutoka Ulaya na nchi za majangwa wanaisifia Arusha.

Ukizungumzia hali ya "sifa" ya watu wa Arusha, ni kweli, watu wetu hujiona wapo level nyingine tofauti na watanzania wengine, hasa ikiwa mtu ameishi Arusha maisha yake yote, akitoka nje anajihisi tofauti sana. Inawezekana hali hii ni kwa sababu ya ukanda wenyewe, kwa sababu ni hali tunaiona pia kwa wakenya.

Kwa kuwa uchumi wa Arusha ulitegemea sana biashara ya madini ya Tanzanite, waliokuwa na migodi na wachimbaji, walipopata mawe na kuuza kwa bei kubwa, walitaka kujulikana mjini, wakaweka misafara ya wapambe na kwenda sehemu za starehe, ambako walijipa uwezo wa kufanya chochote, hata kuchukua msichana wa mtu na uliyechukuliwa ukakaa kimya.

Pakawa na majina makubwa mjini, wao ndio wenye mji, ikasemwa kuwa hawakukubali kufunikwa na wengine. Ikawajengea hofu wafanyabiashara wengine kuwekeza Arusha. Hali hiyo bado ipo akilini mwa watu hadi leo hii, kuwa wanaiogopa Arusha.

Yote na yote, siioni Arusha ikiwa na Maghorofa meengi kama Mwanza, ila kuwe na mazingira rafiki zaidi ya uwekezaji kuendelea kukaribisha watu kutoka mataifa yote duniani kama ilivyo sasa.

Arusha itaendelea kuwa taswira ya Tanzania kimataifa.
 
Capripoint unaweza kuifananisha ata na njiro ya zamani? 🀣 🀣 Washamba bana. Nilikuwa ndugu tena wa damu hapo karibu na hiyo sijui yatch club ushuzi hapo anakwambia mwanza bado sio kama Arusha, sasa ni marehemu rip na alikuwa na viwanda vya kusindika samaki na last time alikuwa anaidai bugando supplies za almost a billion. Wanae wawili wakiume wametimkia arusha mwanza wanaona shambani tu, true story.
 
Ngoja tukuambie ukweli sasa.Hebu acha kumdhalilisha huyo ndugu yako na hiyo supplies ya 1bn Bugando.Hizo biashara za huo mzunguko wanafanya vijana wadogo wadogo na ni wengi tu huko Ziwani na no one even cares kama ni Mabilionea.

Hao wanae waliotimkia Arusha ni wanajua vizuri mziki wa Mwanza hawauwezi,wamerudi huko kwenu ambako kila alie na 200M ni 'Bilionaire'[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbona mna stress sana nyie watu wa Mwanza mnaolazimisha ifanane na Arusha? πŸ€ͺπŸ€ͺ
 
Kwanini mnapenda sana maneno mengiii kuliko vitendo, unaposema njiro kuna watu hawaijui ingekuwa vema kama ungeleta picha za njiro, battle za maneno tuwaachie wakina ashura ndala ndefu na wakina amina kidawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…