Battle: Mwanza (The Rock City) Vs Arusha (A-Town/Chuga)

😂😂
 
Sisi tunaitwa watu wa mikoani wakiwa na maana sio sehemu ya Tanzania, ukija Mwanza barabara ya maana hamna hata moja, majiji kama mwanza, arusha na mbeya haina miundombinu bora, hata flyover tu wakitaka kuangalia wanaenda Dar, kila kitu kinapelekwa Dar na Dodoma kwa kweli sio sawa kabisaa, itafikia hatua tutaomba serikali za majimbo.
 
Mahela yote hayo yanamwagwa Dar wakati sehemu nyingine tunalia na barabara pesa zote hizo zinawekwa kwenye lisoko, hii nchi ni ya ovyo sana ni bora tuambiwe kuwa Dar ndio Tanzania na wengine hatustahili kupata vitu vizuri, pesa za kujenga Dar huwa zipo lakini pesa za kujenga sehemu nyingine utaambiwa subiri bajeti au wapo kwenye feasibility study.
 
Uhakika
 
Ukweli hii nchi Ina viongozi kasuku sana
 
This is My Country, Pwani na Dar ndio Tanzania Arusha na Tanga ni Kenya Lake Zone Unganeni na Rwanda🤣🤣🤣🤣, na bado tunajenga Arena
Ndio maana kila wawekezaji wakubwa wa viwanda lazima wapelekwe Pwani, ni bora waseme mapema tukaungane na burundi, rwanda au uganda kabisa huu ujinga tumechoka.
 
Mapato ya migodi yanaenda kuhesabiwa dar, Tra makato ya bandari yanahesabiwa dar, kila kitu kinachofanyika mikoani kinahesabiwa Dar ili kuwafnya watu wa mikoani wajione wanyonge kuwa hawachangii chochote kwenye taifa, ili ionekane dar ndio inamapato makubwa wakati kiuhalia dar si chochote.
 
Nilikuwa nawashangaa watu wanaopambana na mwanza wakati hii nchi inaliwa na Dar na Dodoma.
 
Tunachezewa sana ndugu zangu, au wanataka watu wote tuishi Dar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…