Habari zenu wanajamvi kiufupi mi ni mgeni hapa ila hili jambo ni kama silifurahii sana, Hivi ni kwanini watanzania mmeamua kutambiana kuhusu sehemu moja dhidi ya nyingine, ukiangalia karibu 90% ya tunavyotambiana ni Government implementation ni vitu ambavyo havihamliwi na wakazi wa sehemu husika bali ni mpaka serikali ihamue,mi nafikiri tujikite katika kuleta hoja za kuikumbusha na kuishauri serikari kuhusu mambo ambayo yakifanyika mji fulani yataleta mchango mkubwa katika eneo husika, tukiendelea na mada hizi itafika mahali watu wasehemu moja watahisi wenzao wasehemu nyingine wanapendelewa zaidi kumbe hata hao tunaoona wanapendelewa nao bado wapo kwenye safari ya kujikomboa mwishowe chuki zitaanza kidogokidogo mwisho tutaingia kwenye kubaguana, Napendekeza hizi battle za majiji na miji ziishe tulete uzi za kuzikumbusha mamlaka zituletee miundombinu itakayotusukuma mbele! Naomba kuwasilisha!