BAVICHA: Tumesikitishwa na tunalaani kitendo cha BASATA kuufungia wimbo wa ‘MAMA'

Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) tumesikitishwa na tunalaani kitendo cha Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA) kuufungia wimbo uitwao ‘MAMA’ ulioimbwa na Msanii wa Mziki wa Kizazi Kipya, Emmanuel Elibariki (Ney wa Mitego).

Mbali ya kuufungia wimbo huo, Basata limemwagiza kusitisha mara moja kupeleka wimbo huo katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kwa madai ya kwamba unakinzana na Kanuni za Basata za mwaka 2018, kanuni ya 25 (6) (d) na (i);

“Baraza katika kuhakiki maadili katika maudhui ya kazi za sanaa, litajiridhisha kuwa kazi ya sanaa;
(d) Haina maneno ya uongo, uchochezi au yanayokashifu watu wengine.
(i) Haidhoofishi umoja, ushirikiano na ustawi bora wa jamii.”

Bavicha baada ya kuusikiliza wimbo huo wa MAMA wa Msanii Ney wa Mitego hatujaona uongo, uchochezi wala kashfa yoyote zinazodaiwa na Basata kuwa sababu za kuufungia wimbo huo. Wala haudhoofishi umoja, ushirikiano na ustawi bora wa jamii yetu.

Huu ni mwendelezo wa Serikali kuweka taratibu za kisheria kwa makusudi ya kuminya uhuru wa maoni, fikra, mawazo ya kisanaa na kuwapangia maudhui wasanii katika kazi zao.

Aidha, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu uhuru wa mawazo, Ibara ya 18 (1) ”Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.”

Uamuzi wa Basata umevunja haki hiyo ya Katiba na umeingilia haki na uhuru wa Msanii Ney wa Mitego kutoa maoni yake.

Bavicha tunatambua kuwa, Wabunge wa Chadema wakati wa Bunge la 11, walipinga kutungwa kwa taratibu hizo kwa sababu zinaminya na kuua ubunifu katika kazi za sanaa. Lakini kutokana na nia ovu ya Serikali iliyopita na wingi wa Wabunge wa CCM, sheria hizo zilipitishwa na sasa tunaona matokeo yake.

Bavicha tunawataka wasanii washikamane na kuwa wamoja katika suala hili na kupinga matumizi ya kanuni hizi mbovu ambazo zitaua vipaji vya sanaa, kuua ndoto za vijana wengi, kuhatarisha ajira za vijana wengi na mapato yanayotokana na kazi za sanaa.

Imetolewa leo Mei 06, 2021 na,

Twaha Mwaipaya
Mratibu wa Uhamasishaji,
Bavicha Taifa.

View attachment 1775117View attachment 1775118
Kumekucha !
 
Hao BASATA bado wapo na fikra za magufuli, nna uhakika Rais atawashinikiza BASATA wauruhusu uho wimbo wake NEY.
 
"🎧🎤🎤🎤Mama! Baba alikua mkali mkali hata wenyewe unajua......🎶🎶🎶🎺"

Huu wimbo ni Bonge la sanaa... ila ndio msanii mwenyewe keshajua mtu mzima hakosei😅😅

Bigup kwako msanii NayWaMitego, wewe ni mkaliii

Afadhali alikua mkali na sio dhaifu...... aendelee kulala salama dad ake🙏

Hawa basata ni mbwa, wimbo mbona hauna tatizo lolote wapuuzi hawa
 
Samahani wakuu, hivi hawa BAVICHA pamoja na BAWACHA wao huwa hawana majukumu mengine ya kichama na labda ya kitaifa? Maana ukisikia haya majina mawili ujue ni tamko flani.
Hawana majukumu mengine tofauti na hili la matamko?
Unataka hadi wakienda kwenye majukumu yao ya kila siku wawe wanakutangazia.unashindwaje kujua kuna shughuli za kila siku na kuna taarifa kwa umma.
 
Sasa si wamwambie Mama Samia afungulie maana amesema anafungua nchi ndio wamwambie afungue na huo wimbo.
Mama atawakemea hawa wapuuzi wa BASATA, wana roho chafu Kama mwendazake, sijui wanahisi bado tupo mwenye utawala wa kiimla
 
Kuna taasisi zingine nikama hazina majukumu yakutosha.Sanaa yetu haina jambo lolote lamaana lakujivunia mambo mengine ni jitihada binafsi za wasanii na hilo baraza nadhani kazi kubwa wanayoweza ni kulumbana tu na wasanii kwa mambo madogo madogo tu ambayo yangeweza kutatulika kirahisi badala ya malumbano na kutunishiana mithuli isiyo na maana.Kwa mfano ukiusikiliza huo wimbo vizuri utagundua hauna jambo lolote baya ambalo ni hatari kwa jamii ya karne hii maana mambo yote yaliyoimbwa yako wazi.Nchi masikini na akili za kimasikini.
 
Kati ya wizara ambayo haija pata viongozi sahihi ni hii ya habari.
Mh. Rais aliagiza vyombo vya habari vilivyo funguwa kibabe vifunguliwe, hadi leo hamna utekelezaji. Ati waziri anataka wakutane washauriane.
Katibu mkuu nae anachagua chombo gani kipewe offer.

Yaani hawajui wana takiwa kufanya nini.
Hawa viongozi wanatakiwa waende kwao maana bado wanadhani huu ni wakati wa mwenda zake.
Hii Sukuma gang inatakiwa itupishe ssa
 
"🎧🎤🎤🎤Mama! Baba alikua mkali mkali hata wenyewe unajua......🎶🎶🎶🎺"

Huu wimbo ni Bonge la sanaa... ila ndio msanii mwenyewe keshajua mtu mzima hakosei😅😅

Bigup kwako msanii NayWaMitego, wewe ni mkaliii

Afadhali alikua mkali na sio dhaifu...... aendelee kulala salama dad ake🙏

Duh kama wimbo wenyewe upo tayari mtandaoni kuna nini tena hapo?
 
Shangazi Halima bado anaonekana kwenye vikao vya ukoo wakati alishatengwa na familia, inakuwaje hii mama?
 
Hii ndiyo sababu zinazosababisha tunahofia uhusiano na nchi kama Kenya kwa sababu ya kufungia uhuru wa watu wetu. Chombo kama BASATA hakina muda wa kuwainua wasanii bali kuwadhibiti na kuwakomoa na hivyo ndivyo Tanzania ilivyo. Walio juu kazi kubwa waliyonayo ni kuonyesha mamlaka na utukufu wa viti vyao.
Watanzania tunahitaji ukombozi, tunahitaji maombi, watu walioko maofisini hawana shida na maendeleo ya watanzania. Hawa ni watanzania wenzetu lakini wanaishi kama vile walizaliwa sayari tofauti. Tumuombee huyu mama wasije tu wakamuondoa duniani tukarudi kwenye ule limwengu wa kukomoana.
Sijui ni kwa nini utafikiri tumelogwa, watanzania wanatamani muuza maandazi azeeke huku akiuza maandazi tu tena kwenye ungo, tumejaa roho za kishirikina, hatuna muda wa kuwaza taifa linakwenda wapi, hapa tulipo tunasomesha watoto lakini hatujui hao walioko maofisini wataamua nini juu ya hatima ya watoto wetu.
Tanzania spika anajivunia uspika wake, mwalimu wa chuo naye anasema ninaweza kuwafelisha, yaani anataka aonyeshe yeye ni nani, polisi naye ,hakimu naye, kila aayepata cheo ni kilio kwa watanzania.
Nilishuhudia konda wa daladala naye anasema mimi mafuta yameishia hapa tafuteni gari nyingine wakati huo nauli ameshachukua na watanzania wanaondoka huku wakitia huruma. I hate this country sijui tumefanywa nini sisi.

MAMA SAMIA KAMA KWELI ANATAKA KULETA SULUHU TANZANIA AJUE KAZI ALIYONAYO NI KUBWA TENA SANA.
 
Aidha, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu uhuru wa mawazo, Ibara ya 18 (1) ”Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko
BAVICHA ni wajinga sana tena hawana akili hivi unaona huo wimbo haujakiuka hiyo katiba hapo juu ambayo umeiandika mwenyewe? kuna maneno ya uongo kuna uchonganishi yaani mnaleta ujinga ujinga wenu kama wa mdude yaani anatenda makosa ya jinai halafu mnamuita mfungwa wa kisiasa pumbavu nyie tushawachoka
 
Samahani wakuu, hivi hawa BAVICHA pamoja na BAWACHA wao huwa hawana majukumu mengine ya kichama na labda ya kitaifa? Maana ukisikia haya majina mawili ujue ni tamko flani.
Hawana majukumu mengine tofauti na hili la matamko?
Soma Katiba ya CHADEMA
 
Hii ndiyo sababu zinazosababisha tunahofia uhusiano na nchi kama Kenya kwa sababu ya kufungia uhuru wa watu wetu. Chombo kama BASATA hakina muda wa kuwainua wasanii bali kuwadhibiti na kuwakomoa na hivyo ndivyo Tanzania ilivyo. Walio juu kazi kubwa waliyonayo ni kuonyesha mamlaka na utukufu wa viti vyao.
Watanzania tunahitaji ukombozi, tunahitaji maombi, watu walioko maofisini hawana shida na maendeleo ya watanzania. Hawa ni watanzania wenzetu lakini wanaishi kama vile walizaliwa sayari tofauti. Tumuombee huyu mama wasije tu wakamuondoa duniani tukarudi kwenye ule limwengu wa kukomoana.
Sijui ni kwa nini utafikiri tumelogwa, watanzania wanatamani muuza maandazi azeeke huku akiuza maandazi tu tena kwenye ungo, tumejaa roho za kishirikina, hatuna muda wa kuwaza taifa linakwenda wapi, hapa tulipo tunasomesha watoto lakini hatujui hao walioko maofisini wataamua nini juu ya hatima ya watoto wetu.
Tanzania spika anajivunia uspika wake, mwalimu wa chuo naye anasema ninaweza kuwafelisha, yaani anataka aonyeshe yeye ni nani, polisi naye ,hakimu naye, kila aayepata cheo ni kilio kwa watanzania.
Nilishuhudia konda wa daladala naye anasema mimi mafuta yameishia hapa tafuteni gari nyingine wakati huo nauli ameshachukua na watanzania wanaondoka huku wakitia huruma. I hate this country sijui tumefanywa nini sisi.

MAMA SAMIA KAMA KWELI ANATAKA KULETA SULUHU TANZANIA AJUE KAZI ALIYONAYO NI KUBWA TENA SANA.
usitetee ujinga bavicha ni wahuni tu sasa huo ni wimbo wakupigia kelele eti una maadili kweli? acheni ujinga
 
Back
Top Bottom