BAWACHA yamtaka Polepole amtaje aliyempiga Lissu risasi

Mbona unakuja personal ndugu! Mimi nimeleta tu ujumbe wa BAWACHA. Tujikite hapo
 
Ipo siku yaja.
 
Damu nzito kuliko maji, utakuwa umenielewa mzee.

Bawacha kutoka kisiwandui au mchambawima
 
Hatuwezi wote kuwa na akili kama ya kwako kwa vile mimi siyo Kalamu bali ni Stuxnet.

Hii ni nchi huru ambayo Katiba yake inatambua uhuru wa maoni na pia JF ni Jukwaa huru. Sina haja ya ku comment kukuridhisha wewe kwa kuwa mimi ni independent person siyo bendera fuata upepo.
 
Wananchi wangapi wanamuunga mkono Polepole? Yaani ukihesabu hawa wa Twitter na JF na Instagram sijui Tiktok unaona ndiyo umemaliza Tanzania??

Kwanza huko kitaa watu hawajui hata kama Polepole alikuwa Balozi wa Cuba na ameaacha
 
Hapo ndipo CHADEMA mnakosea, mnapiga rungu mawazo mbadala. Ana hoja ya nguvu sana. IJIBIWE
 
Wapumbavu ni wale wanaomuunga mkono Polepole ambaye alikuwa kwenye top 5 ya Magufuli iliyoharibu demokrasia ya vyama vingi, iliyobana uhuru wa maoni, iliyoleta Bunge kibogoyo etc.

Angeanza kwa mpangilio. Atueleze waliopanga na kumshambulia Tundu Lissu, kisha aje na namna walivyomkamata Ben Saanane na kumuua na walikomzika. Angeendeleza na walivyo mteka MoDewji na @Roma_Mkatoliki. Baada ya hayo na mengine mengi ndiyo angekuja sasa na awamu ya Samia
 
Polepole kwa sasa ni zaidi ya balaza lote la mawaziri ambalo limepita
 
Mdee mliyemuita majina yote kama COVID-19, msaliti etc leo anaonekana ni bora kuliko huyu
 
Wenzenu wanatakatisha fedha, nyinyi CHADEMA mnatakatisha wahalifu. Hata Lowassa mliyemuita Fisadi mwaka 2009-15, kwa ghafla alipokuja kwenu mkamsafisha na kumpa nafasi ya kugombea urais
 
Mdee mliyemuita majina yote kama COVID-19, msaliti etc leo anaonekana ni bora kuliko huyu
Mdee ni bora mara elfu kuliko huyu.

Huyu ni zile safu alizopanga mbowe kuelekea uchaguzi wa mwenyekiti taifa.
 
kwa mwendo huuu tunamsahau TAL hivihivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…