Bayport: Majambazi yanayolindwa na Serikali?

saigilomagema

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
4,683
Reaction score
7,222
Ndugu Watanzania wenzangu ni nani anayeilinda kampuni ya Bayport Financial services. Taasisi hii imelalamikiwa muda mrefu mpaka malalamiko kutinga bungeni lakini bado ipo na inawaibia, kuwadhulumu watanzania hasa walimu wa nchi hii. Mimi ni mwalimu niko mkoa wa Simiyu wilaya ya Itilima niliwahi kuchukua mkopo kutoka kwao.

Baada ya kuona katika makato yao mwisho wa siku unakatwa hadi zaidi ya mara 5 ya mkopo uliouchukuwa mwaka juzi (2018) niliamua kuuuza mkopo wangu benki ya NMB. Baada ya hapo nililipa deni lao kama walivyonipigia hesabu zao. niliwalipa kwa cash ofisini kwao. Baada ya hapo sikuona makato yao kwa miezi 6 kwani nilishawalipa.

Cha kushangaza baada ya miezi 6 walianza tena kunikata tena kiwango kikubwa kuliko kile cha awali. Nikaenda kuwaona katika branch yao iliyoko Bariadi Mjini. Kufika pale kwanza sikuwakuta wale loan officers walionihudumia wakati nalipa deni lao, kuwauliza waliniambia wameacha kazi na wamewaibia wateja wetu.

Baada ya kuwaeleza kwamba nilishawalipa mbona bado wananikata? jibu lao ni kuwa wao hawana taarifa yoyote walichogundua ni kuwa mimi sikuwapelekea marejesho kwa muda wa miezi hiyo 6 ndiyo maana makato mapya ni makubwa kuliko ya awali.

Kwa kweli Watanzania wenzangu niliondoka bila kuweza kufanya chochote na waliendelea kunikata upya mkopo hewa maana nilishawalipa, ila kwa kuwa hawakunipatia risiti na fomu ya ku-clear mkopo nikawa sina cha kufanya.

Mwaka huu mwanzoni nikawaenedea tena nikitaka kuachana nao wanipe mahesabu yao ya mkopo hewa nikauuze tena NMB ila sasa kwa kufuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuwaomba NMB Bank wafanye transfer moja kwa moja kwenda akaunti ya Bayport na kunipatia risiti inayoonesha sababu za kufanya hiyo transfer. Baada ya NMB Bank kuwalipa niliwapelekea risiti ili wanipatie fomu ya ku-clear mkopo wao na then nimpelekee mwajiri wangu ambaye ni Halmashauri ya Wilaya ya Itilima ili asimamishe makato ya Bayport na kuingiza makato mapya ya NMB.

Kimbembe sasa ni kupewa hako ka-fomu, mpaka sasa hivi ninavyoandika sijapewa hiyo fomu na NMB imeizuia akaunti yangu siwezi kufanya muamala wowote mpaka niwapelekee hiyo fomu. Nimeenda ofisi yao ya Bariadi mara nyingi nimeshamaliza hela sana kufuatilia, kuna mdada pale ana nyodo, dharau isiyopimika. Kila ukienda ananiambia fomu haijatumwa kutoka makao makuu ambayo yako Mwanza, ukiwapigia makao makuu wanakuambia nenda kwenye branch, huyo Branch Manager hata simu mara nyingi hapokei, ukioenda ofisini anaweza hata akakuacha ofisini anatoka.

Yule Branch Manager ni wazi anajenga mazingira ya rushwa na kwa vyovyote vile anataka aendelee tena kunikata pamoja na kwamba nimewalipa mara 2 bila uhalali wowote.

Sasa naomba mamlaka zinazohusika zinisaidie watoto wangu wafa njaa, akaunti imefungwa nitakatwa tena mara ya 3. Mheshimiwa Rais najua uko popote ndani ya nchi hii naomba utusaidie dhidi ya huyu jambazi katili. Taasisi hii haiogopi chombo chochote cha dola wala cha kisheria sijui nani anakilinda. Tusaidie baba Rais hakuna mwingine anayewaweza hawa tatu.
 
Pole sana, hili mbona halimhitaji hata RC? Usiende kinyonge tena, nenda kalianzishe vizuri tu, watakupatia! Acha kulalamika na kuwa mpole, enzi za kuwa mpole zimeshapita! Ukiwa hivyo utapandiwa kichwani hadi unaingia kaburini. Kapige mkwara wa kufa MTU.

Kitochi Original
 
Kuna kitabu nilisoma na mwandishi aliandika hivi.
Get Out Of Debt (GOOD. Ni nje ya kile ulichoomba msaada kwacho, lakini pia chafaa kwa matumizi ya baadaye.
 
Ndugu Watanzania wenzangu ni nani anayeilinda kampuni ya Bayport Financial services. Taasisi hii imelalamikiwa muda mrefu mpaka malalamiko kutinga bungeni lakini bado ipo na inawaibia, kuwadhulumu watanzania hasa walimu wa nchi hii. Mimi ni mwalimu niko mkoa wa Simiyu wilaya ya Itilima niliwahi kuchukua mkopo kutoka kwao.

Baada ya kuona katika makato yao mwisho wa siku unakatwa hadi zaidi ya mara 5 ya mkopo uliouchukuwa mwaka juzi (2018) niliamua kuuuza mkopo wangu benki ya NMB. Baada ya hapo nililipa deni lao kama walivyonipigia hesabu zao. niliwalipa kwa cash ofisini kwao. Baada ya hapo sikuona makato yao kwa miezi 6 kwani nilishawalipa.

Cha kushangaza baada ya miezi 6 walianza tena kunikata tena kiwango kikubwa kuliko kile cha awali. Nikaenda kuwaona katika branch yao iliyoko Bariadi Mjini. Kufika pale kwanza sikuwakuta wale loan officers walionihudumia wakati nalipa deni lao, kuwauliza waliniambia wameacha kazi na wamewaibia wateja wetu.

Baada ya kuwaeleza kwamba nilishawalipa mbona bado wananikata? jibu lao ni kuwa wao hawana taarifa yoyote walichogundua ni kuwa mimi sikuwapelekea marejesho kwa muda wa miezi hiyo 6 ndiyo maana makato mapya ni makubwa kuliko ya awali.

Kwa kweli Watanzania wenzangu niliondoka bila kuweza kufanya chochote na waliendelea kunikata upya mkopo hewa maana nilishawalipa, ila kwa kuwa hawakunipatia risiti na fomu ya ku-clear mkopo nikawa sina cha kufanya.

Mwaka huu mwanzoni nikawaenedea tena nikitaka kuachana nao wanipe mahesabu yao ya mkopo hewa nikauuze tena NMB ila sasa kwa kufuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuwaomba NMB Bank wafanye transfer moja kwa moja kwenda akaunti ya Bayport na kunipatia risiti inayoonesha sababu za kufanya hiyo transfer. Baada ya NMB Bank kuwalipa niliwapelekea risiti ili wanipatie fomu ya ku-clear mkopo wao na then nimpelekee mwajiri wangu ambaye ni Halmashauri ya Wilaya ya Itilima ili asimamishe makato ya Bayport na kuingiza makato mapya ya NMB.

Kimbembe sasa ni kupewa hako ka-fomu, mpaka sasa hivi ninavyoandika sijapewa hiyo fomu na NMB imeizuia akaunti yangu siwezi kufanya muamala wowote mpaka niwapelekee hiyo fomu. Nimeenda ofisi yao ya Bariadi mara nyingi nimeshamaliza hela sana kufuatilia, kuna mdada pale ana nyodo, dharau isiyopimika. Kila ukienda ananiambia fomu haijatumwa kutoka makao makuu ambayo yako Mwanza, ukiwapigia makao makuu wanakuambia nenda kwenye branch, huyo Branch Manager hata simu mara nyingi hapokei, ukioenda ofisini anaweza hata akakuacha ofisini anatoka.

Yule Branch Manager ni wazi anajenga mazingira ya rushwa na kwa vyovyote vile anataka aendelee tena kunikata pamoja na kwamba nimewalipa mara 2 bila uhalali wowote.

Sasa naomba mamlaka zinazohusika zinisaidie watoto wangu wafa njaa, akaunti imefungwa nitakatwa tena mara ya 3. Mheshimiwa Rais najua uko popote ndani ya nchi hii naomba utusaidie dhidi ya huyu jambazi katili. Taasisi hii haiogopi chombo chochote cha dola wala cha kisheria sijui nani anakilinda. Tusaidie baba Rais hakuna mwingine anayewaweza hawa tatu.
KWa nini uwalipe mara mbili?

Kwa sababu gani?

Unazo risit za bank ukizowalipa mara ya kwanza?

Kama unazo hizo hizo unaenda nazo
 
Mimi niliomba mkopo kwa hawa Bayport kipindi bado sijathibitishwa kazini sababu ya matatizo ya kifamilia,baada ya ile hela kuingia nilikaa km wiki mbili wakaingiza tena kiasi kile kile nilichoomba huku siku km 3 walinipigia simu kuuliza km kuna hela imeingia,uzuri nilikuwa Banki hakukuwa na hela iliyoingia nikawajibu hakuna hela,baada ya hizo wiki hela ilipoingia Mimi nikaitumia.
Sasa nawasubiri nimalize mkopo wangu twende mahakamani hakuna namna mana sina mkata na wao na sitaki kuendelea na wao wala kukatwa na wao km kuwalipa tutafute njia nyingine sio makato yao yasiyoeleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unahakika wamekuibia unyonge hausaidiii....ningekua Mimi hela yangu wangerudisha in legal or illegal way ....walah hao Ni vile hawajakutana na wahuni...hahaaa..eti dada anakujibu nyodo...come-on...andaaa milioni mbili...fanya naniliuuu...anaza ku black mail. .daaah ntaanza kukufundsha umafia...we endelea tu kulia lia
 
Wale ni washenzi wameliza sana watumishi ,mkataba wa makato ni tofauti mtu anakopesha laki 7 anarejesha MILION 6

Togauti na makubaliano ....halafu takukuru hawachunguzi kabisa

Na wengine bado wanajipeleka kukopa wakishalizwa ndio wanaanza kulalalamika

Tuweni makini sana na Taasisi zinazokopesha wanakwambia riba kwa mwezi ni 3.6 %ukicaculate kwa mwaka utalia

Mikopo ni mizuri ila imeangamiza wengi sana

sent from toyota Allex
 
Nyie walimu ni sehemu ya wanyonge wa nchi hii. mwalimu mzima unashindwaje kujisimamia kwenye jambo dogo kama hilo.Hapo sidhani kama ata mkopo wenyewe ni zaidi ya milioni 20.Kwani hao bayport ndo wanaokulipa mshahara au mshahara wako unapitia kwanza kwao ndo wakulipe wewe hadi ukatwe makato zaidi.Ukiona hizo taasisi za mikopo zinakufanyia uhuni jua tatizo ni wewe kutojitambua.Acha unyonge.
 
Back
Top Bottom