Bayport: Majambazi yanayolindwa na Serikali?

Bayport: Majambazi yanayolindwa na Serikali?

Kwanza ulikosea sana kuwapelekea fedha ya kuclear mkopo bila kupewa risiti ya marejesho. Fedha yoyote ile unayorejesha lazima malipo yake yawe na receipt kwa conviniency za baadae. Aidha nakushauri upeleke maelezo yako TAKUKURU haraka naamini watakupa msaada sana. Peleka vielelezo vyako kusapoti malalamiko yako.
 
Kuna watu wapole duniani hapa daah.. Ingekuwa mimi CCN, BBC na mashirika yote makubwa ya habari yangekuja kuripoti hii habati kimataifa kwa action ambayo ningechukua kwa huyo Branch Manager..

~~Kitakachokupa ushindi ni juhudi zako~~
 
Ndugu Watanzania wenzangu ni nani anayeilinda kampuni ya Bayport Financial services. Taasisi hii imelalamikiwa muda mrefu mpaka malalamiko kutinga bungeni lakini bado ipo na inawaibia, kuwadhulumu watanzania hasa walimu wa nchi hii. Mimi ni mwalimu niko mkoa wa Simiyu wilaya ya Itilima niliwahi kuchukua mkopo kutoka kwao.

Baada ya kuona katika makato yao mwisho wa siku unakatwa hadi zaidi ya mara 5 ya mkopo uliouchukuwa mwaka juzi (2018) niliamua kuuuza mkopo wangu benki ya NMB. Baada ya hapo nililipa deni lao kama walivyonipigia hesabu zao. niliwalipa kwa cash ofisini kwao. Baada ya hapo sikuona makato yao kwa miezi 6 kwani nilishawalipa.

Cha kushangaza baada ya miezi 6 walianza tena kunikata tena kiwango kikubwa kuliko kile cha awali. Nikaenda kuwaona katika branch yao iliyoko Bariadi Mjini. Kufika pale kwanza sikuwakuta wale loan officers walionihudumia wakati nalipa deni lao, kuwauliza waliniambia wameacha kazi na wamewaibia wateja wetu.

Baada ya kuwaeleza kwamba nilishawalipa mbona bado wananikata? jibu lao ni kuwa wao hawana taarifa yoyote walichogundua ni kuwa mimi sikuwapelekea marejesho kwa muda wa miezi hiyo 6 ndiyo maana makato mapya ni makubwa kuliko ya awali.

Kwa kweli Watanzania wenzangu niliondoka bila kuweza kufanya chochote na waliendelea kunikata upya mkopo hewa maana nilishawalipa, ila kwa kuwa hawakunipatia risiti na fomu ya ku-clear mkopo nikawa sina cha kufanya.

Mwaka huu mwanzoni nikawaenedea tena nikitaka kuachana nao wanipe mahesabu yao ya mkopo hewa nikauuze tena NMB ila sasa kwa kufuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuwaomba NMB Bank wafanye transfer moja kwa moja kwenda akaunti ya Bayport na kunipatia risiti inayoonesha sababu za kufanya hiyo transfer. Baada ya NMB Bank kuwalipa niliwapelekea risiti ili wanipatie fomu ya ku-clear mkopo wao na then nimpelekee mwajiri wangu ambaye ni Halmashauri ya Wilaya ya Itilima ili asimamishe makato ya Bayport na kuingiza makato mapya ya NMB.

Kimbembe sasa ni kupewa hako ka-fomu, mpaka sasa hivi ninavyoandika sijapewa hiyo fomu na NMB imeizuia akaunti yangu siwezi kufanya muamala wowote mpaka niwapelekee hiyo fomu. Nimeenda ofisi yao ya Bariadi mara nyingi nimeshamaliza hela sana kufuatilia, kuna mdada pale ana nyodo, dharau isiyopimika. Kila ukienda ananiambia fomu haijatumwa kutoka makao makuu ambayo yako Mwanza, ukiwapigia makao makuu wanakuambia nenda kwenye branch, huyo Branch Manager hata simu mara nyingi hapokei, ukioenda ofisini anaweza hata akakuacha ofisini anatoka.

Yule Branch Manager ni wazi anajenga mazingira ya rushwa na kwa vyovyote vile anataka aendelee tena kunikata pamoja na kwamba nimewalipa mara 2 bila uhalali wowote.

Sasa naomba mamlaka zinazohusika zinisaidie watoto wangu wafa njaa, akaunti imefungwa nitakatwa tena mara ya 3. Mheshimiwa Rais najua uko popote ndani ya nchi hii naomba utusaidie dhidi ya huyu jambazi katili. Taasisi hii haiogopi chombo chochote cha dola wala cha kisheria sijui nani anakilinda. Tusaidie baba Rais hakuna mwingine anayewaweza hawa tatu.
Wanashirikiana hao Bayport, benki na waajiri wako. Haiwezekani wote wasijue makato ya deni yasiyo na kikomo. Hata TAKUKURU, polisi na tis wanajua lakini wako kimya!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie walimu ni sehemu ya wanyonge wa nchi hii. mwalimu mzima unashindwaje kujisimamia kwenye jambo dogo kama hilo.Hapo sidhani kama ata mkopo wenyewe ni zaidi ya milioni 20.Kwani hao bayport ndo wanaokulipa mshahara au mshahara wako unapitia kwanza kwao ndo wakulipe wewe hadi ukatwe makato zaidi.Ukiona hizo taasisi za mikopo zinakufanyia uhuni jua tatizo ni wewe kutojitambua.Acha unyonge.
Halafu, tunajua Walimu ni watu waelewa. Cha kushangaza idadi kubwa ya waathirika wa mikopo hii ni Walimu. Mwalimu anashindwa kupiga hesabu ili kujua mwisho wa siku atakuwa amelipa kiasi gani cha pesa. Tatizo hili ni la miaka mingi, ila cha kusikitisha hadi leo bado wanaendelea kukopa tu. Ogopa sana wakopeshaji ambao wanatoa mikopo yao ndani ya saa 24. Kwa vile una shida macho yako kodo kwenye hizo milioni, unasahau kabisa kusoma na kuuliza mkataba wao ukoje. Baada ya hapo utagundua kuwa umeishia mtegoni mwa hao "Mashyloki" ambao wanataka hadi nyama yako. Kumbuka mkopo ni kama mitego mingine tu, ni rahisi sana kuingia lakini ni vigumu kujinasua.
 
Kasema aliwalipa kwa cash.. Sasa sijui toka lini mkopo unalipwa mkononi.
Ndo walimu wetu hawa!

Sent using Jamii Forums mobile app
Na amesema hana risiti wala fomu yyte, yaani alikabidhi hela na kuondoka zake, ndo maana amekubali kulipa Mara ya pili...

Sijui hata wanawafundisha nini watoto wetu huko mashuleni
 
  • Thanks
Reactions: amu
Pole sana mwalimu

Usikute ulikopa ukanunua pikipiki aina ya boxer

Kinachoumiza zaidi boxer ushaibiwa na bado

unagongwa sindano ya klistapeni

Pambana mkuu!


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Bayport platinum credit maboto and the like usijaribu utafilisika

Kama unataka mkopo nenda benki mbona easy Hawa loan sharks wako kwa ajili ya kuumiza watu sio kukusadia

Baware!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hizi taasisi za fedha ambazo mnakabidhi kadi za benki!?????
 
Hata mim nilikopa baypot makato yao wanamaliza mwez wa nane!! je wanaweza wakazidisha miez ya kukata kinyume na mkataba?? nijibun il nijiandae kwa mapambano
 
Back
Top Bottom