Bayport: Majambazi yanayolindwa na Serikali?

Bayport: Majambazi yanayolindwa na Serikali?

Inawezekana hapo katikati ulipokuwa unalipa kwa keshi kunashortcut ulipita kwa kutumia loans officers sasa ikatokea umetumbuliwa na hesabu zikapigwa upya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mim nilikopa baypot makato yao wanamaliza mwez wa nane!! je wanaweza wakazidisha miez ya kukata kinyume na mkataba?? nijibun il nijiandae kwa mapambano
Jiandae na Vita, hao watu ukiwa mnyonge imekula kwako
 
BAYPORT ni matapeli wa muda mrefu na kila kukicha malalamiko hayakauki na wengineo wataendelea kuibiwa kwa kutofanya utafiti kabla ya kuchukua hela za chap chap na masharti nafuu.
 
Unakopaji sehemu kama hizo uchwara,wakati kuna benki kubwa kibao.
Ndugu Watanzania wenzangu ni nani anayeilinda kampuni ya Bayport Financial services. Taasisi hii imelalamikiwa muda mrefu mpaka malalamiko kutinga bungeni lakini bado ipo na inawaibia, kuwadhulumu watanzania hasa walimu wa nchi hii. Mimi ni mwalimu niko mkoa wa Simiyu wilaya ya Itilima niliwahi kuchukua mkopo kutoka kwao.

Baada ya kuona katika makato yao mwisho wa siku unakatwa hadi zaidi ya mara 5 ya mkopo uliouchukuwa mwaka juzi (2018) niliamua kuuuza mkopo wangu benki ya NMB. Baada ya hapo nililipa deni lao kama walivyonipigia hesabu zao. niliwalipa kwa cash ofisini kwao. Baada ya hapo sikuona makato yao kwa miezi 6 kwani nilishawalipa.

Cha kushangaza baada ya miezi 6 walianza tena kunikata tena kiwango kikubwa kuliko kile cha awali. Nikaenda kuwaona katika branch yao iliyoko Bariadi Mjini. Kufika pale kwanza sikuwakuta wale loan officers walionihudumia wakati nalipa deni lao, kuwauliza waliniambia wameacha kazi na wamewaibia wateja wetu.

Baada ya kuwaeleza kwamba nilishawalipa mbona bado wananikata? jibu lao ni kuwa wao hawana taarifa yoyote walichogundua ni kuwa mimi sikuwapelekea marejesho kwa muda wa miezi hiyo 6 ndiyo maana makato mapya ni makubwa kuliko ya awali.

Kwa kweli Watanzania wenzangu niliondoka bila kuweza kufanya chochote na waliendelea kunikata upya mkopo hewa maana nilishawalipa, ila kwa kuwa hawakunipatia risiti na fomu ya ku-clear mkopo nikawa sina cha kufanya.

Mwaka huu mwanzoni nikawaenedea tena nikitaka kuachana nao wanipe mahesabu yao ya mkopo hewa nikauuze tena NMB ila sasa kwa kufuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuwaomba NMB Bank wafanye transfer moja kwa moja kwenda akaunti ya Bayport na kunipatia risiti inayoonesha sababu za kufanya hiyo transfer. Baada ya NMB Bank kuwalipa niliwapelekea risiti ili wanipatie fomu ya ku-clear mkopo wao na then nimpelekee mwajiri wangu ambaye ni Halmashauri ya Wilaya ya Itilima ili asimamishe makato ya Bayport na kuingiza makato mapya ya NMB.

Kimbembe sasa ni kupewa hako ka-fomu, mpaka sasa hivi ninavyoandika sijapewa hiyo fomu na NMB imeizuia akaunti yangu siwezi kufanya muamala wowote mpaka niwapelekee hiyo fomu. Nimeenda ofisi yao ya Bariadi mara nyingi nimeshamaliza hela sana kufuatilia, kuna mdada pale ana nyodo, dharau isiyopimika. Kila ukienda ananiambia fomu haijatumwa kutoka makao makuu ambayo yako Mwanza, ukiwapigia makao makuu wanakuambia nenda kwenye branch, huyo Branch Manager hata simu mara nyingi hapokei, ukioenda ofisini anaweza hata akakuacha ofisini anatoka.

Yule Branch Manager ni wazi anajenga mazingira ya rushwa na kwa vyovyote vile anataka aendelee tena kunikata pamoja na kwamba nimewalipa mara 2 bila uhalali wowote.

Sasa naomba mamlaka zinazohusika zinisaidie watoto wangu wafa njaa, akaunti imefungwa nitakatwa tena mara ya 3. Mheshimiwa Rais najua uko popote ndani ya nchi hii naomba utusaidie dhidi ya huyu jambazi katili. Taasisi hii haiogopi chombo chochote cha dola wala cha kisheria sijui nani anakilinda. Tusaidie baba Rais hakuna mwingine anayewaweza hawa tatu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iv wanawezaje kukata kwa kuzidisha miezi kinyume na makubaliano??? na je kweli wapo waliowafanyia ivi ukiachilia na huyu alieenda kulipa kwa keshi??? naomba mnsaidie majibu il nijiandae kwa mapambano
 
Hivi kweli ndugu yangu unalipa mkopo bila kuchukua risiti?

Hata mtaani ukilipa deni la jirani au rafiki unaenda na shahidi.
 
iv baypot wanawezaje kuzidisha miez ya makato kinyume na mkataba??? je wapo waliokopa na wakakatwa na miez ya ziada kinyume na makubaliano?? ukiachilia mbali na huyu alieenda kulipa kesh!!! naomba majibu il nijiandae kwa mapambano
 
iv baypot wanawezaje kuzidisha miez ya makato kinyume na mkataba??? je wapo waliokopa na wakakatwa na miez ya ziada kinyume na makubaliano?? ukiachilia mbali na huyu alieenda kulipa kesh!!! naomba majibu il nijiandae kwa mapambano
Mkuu Achana na mkopo we tupe burudan ya Mapenz tuu tupia vitu tusome
Usilipe Huo mkopo ni ovyo tuu kimbia

Njoo huku Canada tule maisha

Sent by IPhone
 
Back
Top Bottom