A
Anonymous
Guest
Mimi ni mtumishi wa serikali. Kuna malalamiko yaliwahi pia kuandikwa hapa siku za nyuma lakini lile tatizo nadhani limezidi maradufu. Kampuni za mikopo mfano Bayport, Manoto Bank, ABC na zingine zimekuwa zikituma meseji za huduma zao wakati sijawahi kujiunga wala kujaza fomu zao.
Kwa mfano hao Manoto nimeshawapigia sana kuwaomba wanitoe lakini walinijibu haiwezekani, mfumo wetu hauruhusu kumtoa mtu akishwekwa tena kwa jeuri tukagombana akakata simu. Imekuwa kero na mpaka sasa karibia kwa wiki napokea meseji mara mbili.
Nani anatoa taarifa zetu kwao? Sheria mpya inasemaje kuhusu ukusanyaji wa taarifa za watu? Kwa sheria mpya naweza kuwafungulia kesi? Imekuwa hatua nitafute mwanasheria mzuri nipate fidia. Waziri wa mawasiliano na wa fedha hili limewashinda kabisa kuwadhibiti hawa watu?