BBC, habari za moto Mlima Kilimanjaro anaripoti mwandishi kutoka Kenya, ni sahihi?

BBC, habari za moto Mlima Kilimanjaro anaripoti mwandishi kutoka Kenya, ni sahihi?

Hakuna cha ajabu Hapo. Hiyo ipo Sana hasa hivi vyombo vikubwa vya kimataifa.
 
Hakuripoti mwandishi wa Tanzania kwasababu mtamuona anatumika na Mabeberu. Unajua hii nchi haitaki kabisa kuona ukweli ukiongelewa matokeo yake wanawatumia watu wengine ambao hawawezi kutekwa, kuuliwa wala kufilisiwa mali zao.
 
BBC ni chombo cha kipropaganda cha mabeberu

Wanatekeleza matakwa ya mabwana zao

Wanajaribu kui ignore Tanzania ila kwa neema za Mungu tutasonga bila wao

Shame upon them wakitangaza habari esp za Tanzania haziwi ballanced

Wanawahoji vibaraka wao tu bila kupata majibu ya upande wa pili
 
Vyombo vya habari Tz vimepigwa pini kufungamana na mashirika ya nje nje. Sababu kubwa ni uchaguzi mkuu malaika wa chatoo hataki akosolewe!
 
Niliona wanafunzi wa chuo cha mweka wanakwenda huko asubuhi kwa mbwembwe kweli, nikajua watauzima mara moja ila kufika usiku bado moto unaonekana ni mkubwa.

Nafikiri inahitajika nguvu kubwa zaidi ya kuuzima kwasababu kama mtu upo moshi mjini na unauona huo moto, maana yake ni mkubwa sana.
 
Mkuu katika hili wakulaumiwa ni wanahabari wetu wenyewe yaani wanahabari wa Tz na sekta nzima ya habari Tz ni zero kabisa
Tukianza na wanahabari, wengi ni kama wametekwa na issues ambazo sio sensitive yaani habari ambazo haziwapi high millage kimataifa wao kila kukicha ni kusifia wanasiasa tu.

Leo hii hata tuzo za yule mwanahabari wa BBC, ambaye ni raia wa Ghana, baada ya kufariki,kila kukicha wanashinda Wakenya wanahabari wetu ni kwamba hawana uwezo au hawajali? Yaani ni failure kabisaa.

Pili; Media Houses zenyewe na waendeshaji wake, yaani hapa ni shida pia Tz media houses nyingi zinatumia vyombo vya kizamani, studios mbayaaaa kwa kifupi hapa investment inahitajikaa. Leo hii tazama TVs za Kenya yaani matangazo yao, contents zao, ni za kuvutia.

Hata Rwanda wametupita ukitazama Rwanda TV ukalinganisha TBC1, yaani ni mbingu na ardhi. Media nyingi za Tz kazi yao ni kuanzisha stations ambazo ni miziki tu kama disco, yaani stations za miziki ni zaid ya 10k.

Sasa kwa style kama hii ni wazi hamna kitu. Pia imekuwepo tabia ya wamiliki kuwa na wafanya kazi ambao hawana taaluma ya uandishi wa Habari.
 
Unataka mtanzania aripoti ili aonekane anaisaliti Nchi? Maana bongo ukiongea ukweli unaonekana msaliti
 
Aisee mpaka tunapoongea hivi sasa moto unawaka sana sana, na pia unazidi kuongezeka distance wakati wa usiku kwasababu ya upepo, Mimi nimekaribia hata ukikaa mita kadhaa joto ni kali mno.

Halafu wakati huohuo kwenye mlima wa usangi pia kuna moto unaonekana kwa mbali na pia ni mkubwa kweli.

Sijui ni nini hiki
Usishangae ukiambiwa na serikali yako kwamba ni hujuma za mabeberu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bbc ni chombo cha kipropaganda cha mabeberu

Wanatekeleza matakwa ya mabwana zao

Wanajaribu kui ignore Tanzania ila kwa neema za Mungu tutasonga bila wao

Shame upon them wakitangaza habari esp za Tanzania haziwi ballanced

Wanawahoji vibaraka wao tu bila kupata majibu ya upande wa pili
Ni sawa na wewe unavyotekeleza matakwa ya bwana ako Polepole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua makao makuu ya BBC Afrika Mashariki yako Kenya, huyo aliyeripoti hakuchukua moto wetu wala majivu, tulihakikisha anaondoka mikono mitupu, acha kulialia.
 
Mleta mada unamjua Azory Gwanda?
Hamna kitu chief, Tz tumejaliwa kuwa na vitu kibao vya kuvipa millage achana na siasa! Nikupe mfano

BBC world walitangaza habari ya tukio la jamii ya wamasai,walifanya mkutano mkubwa sana ambao uliwakutanisha wamasai wa kenya na Tz ile habari katika page ya BBC ilipata likes nyingi sana wazungu wengi walicomment kuhusu jamii ya maasai, tena ni hivi majuzi tu mwezi Septemba.

Sasa swali ni je, hivi wanahabari wetu vitu kama hivi wao hawavioni?Ukweli ni kwamba wanahabari wengi wa Tz wanaripoti kuhusu siasa tu.
 
Niliona wanafunzi wa chuo cha mweka wanakwenda huko asubuhi kwa mbwembwe kweli, nikajua watauzima mara moja ila kufika usiku bado moto unaonekana ni mkubwa.

Nafikiri inahitajika nguvu kubwa zaidi ya kuuzima kwasababu kama mtu upo moshi mjini na unauona huo moto, maana yake ni mkubwa sana.
Nimeisikia hiyo habari asubuhi hii msemaji wa Tanapa anasema eti walishirikiana na wanafunzi wa vyuo vikuu vya Moshi.
Hakika inahuzunisha na kuchekesha pia.

Mungu atatenda lakini
 
Back
Top Bottom