Mkuu katika hili wakulaumiwa ni wanahabari wetu wenyewe yaani wanahabari wa Tz na sekta nzima ya habari Tz ni zero kabisa
Tukianza na wanahabari, wengi ni kama wametekwa na issues ambazo sio sensitive yaani habari ambazo haziwapi high millage kimataifa wao kila kukicha ni kusifia wanasiasa tu.
Leo hii hata tuzo za yule mwanahabari wa BBC, ambaye ni raia wa Ghana, baada ya kufariki,kila kukicha wanashinda Wakenya wanahabari wetu ni kwamba hawana uwezo au hawajali? Yaani ni failure kabisaa.
Pili; Media Houses zenyewe na waendeshaji wake, yaani hapa ni shida pia Tz media houses nyingi zinatumia vyombo vya kizamani, studios mbayaaaa kwa kifupi hapa investment inahitajikaa. Leo hii tazama TVs za Kenya yaani matangazo yao, contents zao, ni za kuvutia.
Hata Rwanda wametupita ukitazama Rwanda TV ukalinganisha TBC1, yaani ni mbingu na ardhi. Media nyingi za Tz kazi yao ni kuanzisha stations ambazo ni miziki tu kama disco, yaani stations za miziki ni zaid ya 10k.
Sasa kwa style kama hii ni wazi hamna kitu. Pia imekuwepo tabia ya wamiliki kuwa na wafanya kazi ambao hawana taaluma ya uandishi wa Habari.