BBC: Jinsi Rais Magufuli anavyopambana na corona na "mabeberu"

BBC: Jinsi Rais Magufuli anavyopambana na corona na "mabeberu"

Wanajukwaa !

Leo asubuhi siku happy kabisa baada ya kusoma makala ya hii ya mwandishi Sammy Awami nakala ndefu (long read) kama wanavyoziita kule BBC ya kutia huzuni,dhihaka, na udhalilishaji kwa Rais wa Tanzania imepakiwa na mtanzania mwenzetu tena mnyamwezi wa Tabora juu ya utendaji wa Rais wetu John Magufuli imeniumiza sana tena sana , kwa kuwa nitaandika machache na mods wanisaidie kuuga nakala yote ya English kutoka BBC.

Heading inasema -Tanzania's Magufuli -talking on coronavirus and imperialism

Nitatumia neno 'Eti' kuonesha mashaka makubwa ya mwandishi huyu.

Hoja

1. Eti Rais Magufuli anakosolewa kwa kurudiarudia kuwashambulia mabeberu na kutangaza kuwa ndani ya Afrika mashariki yeye tu ndio ameimaliza corona (huu ni upotoshaji Rais wetu amesema corona bado ipo na kutuwe makini kufuata kanuni za afya na tuchukue tahadhari)

2. Eti ametumia miaka mitano kujifanya mmajumui wa Afrika na kupambana na unyonyaji wa kimagharibi kwa kutumia ukatoriki ( si kweli rais wetu anaheshimu sana mahusiano mema na nchi za ulaya kama wahisani na marafiki ametuma mabalozi na kuwapokea kwa bashasha ikulu na kuwashirikisha kila kitu kwa mujibu wa sheria)

3. Mwandishi Sammy Awami anadai eti aliukataa mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na kusema waliopitisha ni wehu (madman) akimlenga mtangulizi wake Jakaya Kikwete. (Hii si kweli huu makataba serikali ilifafanua ugumu wa vipengele vya ule mkataba ambao hata hivyo hatua za mwisho za kuupitisha zilikuwa bado)

3. Eti Rais wetu anandoto kubwa kupita kiasi/uwezo wa kimadiliko ambao unamfanya ajiamini zaidi na kubinya upinzani na habari huku ameongeza uchunguzi kwa wanao mipinga hasa waandishi wa habari na wanaharakati (hapa mwandishi ameonesha jinsi anavyo beba agenda zake maana yeye mwenyewe tangu afanye kazi hapa Tanzania hajasumbuliwa kwa lolote sasa mbinyo gani na lini alifatiliwa)

4. Eti Rais wetu hapendi kushirikiana na majirani wala hakusaisi mizozo ya mipaka kati ya Kenya na Zambia mipakani ( huu ni uongo na uzushi rais wetu amekuwa anatembelea majirani na marais wote majirani wamefika hapa na yeye kwenda kwao na mara nyingi, hata mzozo wa mipaka kipindi cha korona aliutolea kauli na ukaisha akiwa mkoani Singida na kile kikao cha wakuu wa nchi Afrika mashariki waziri Kabudi alikitolea ufafanuzi kuwa hatukuitwa )

5. Eti kuwa yeye na waziri mkuu wanapishana kauli kuhusu idadi ya corona ( hapa mwandishi hakufanya utafiti mdogo tu maana kasi ya maambukizi huapanda na kushuka sio static leo wanaweza wakawa hakuna kesho wakawa wengi au wakawa wengi na wakaisha hili ni jambo la kawaida)

6. Eti magufuli anaamini ushirikiano wa Afrika tu wazungu anawaona kama maadui - ( huu ni uchochezi hapa tunazo balozi za mataifa mbalimbali pia Rais amekuwa akiwaomba waje kungana na watanzania kupigania maendeleo kama marafiki)

Ubeberu sio tusi ni sawa na wao wanavyotuita wajamaa

Ubeberu ni upebari mkongwe sasa hapo tusi liko wapi

Capitalism -ubepari-capitalist-bepari
Imperialism -ubeberu-imperialist-beberu
Socialism-ujamaa-socialist -jamaa

So mh rais kuwaita mababeru sio kosa hata kidogo ni kama wao wanavyotuita wajamaa

WITO KWA WAZIRI KABUDI

Muiteni huyu mwandishi maana kituo chake cha kazi kiko hapa Dar mumuhoji kama mlivyomuhoji balozi wa U.S. ,m kimuacha kesho ataandika uongo tena

Chanzo BBC

USSR

Jinyonge! Ukweli ndiyo huo
 
Huyu muandishi ameandika ukweli mtupu, ila kwenye eneo ulilosimama ww ndio sio rafiki.
 
Uchochezi ni nini ndugu yangu ?
Mbona swala jamaa linawatoa utu na akili ?!. U communist hautatutoa mrisi. Amini usiamini . Ninao usoefu, siyo rahisi kihivyo
Sheria za nje lazima ziheshimiwa,sio ukomunist wala uonevu. Soma kifungu cha 52(1)(a) cha media services Act utajua uchochezi ni nini.
 
Mbona Makala ipo clear hakuna lililopotoshwa.. na nyie si msome makala ya kina Musiba.
 
BBC wakitoa taarifa nzuri juu ya magufuli mataga mnakenua meno. Wakitoa habari negative mnasema ni mabeberu.
 
Sioni tatizo katika andishi la BBC. Tatizo lipo kwa watu wasiopenda maoni tofauti na ya kwao.

Hizo hoja za uongo za BBC si zijibiwe tu kwa hoja? Au walalamishi hawaamini kuwa wasomaji tuna uwezo wa kutosha kuchambua pumba na mchele?

Kweli Rais wetu katufanyia mengi mazuri. Labda tukubaliane ukosoaji uwe na staha n a heshima. Na sio mara zote anae kukosoa hakupendi au hataki uendelee kuwa hapo ulipo.

Ni bora huyo mwandishi akashtakiwa mahakamani kuliko kuitwa kujieleza kwa mamlaka, itakuwa ni tangazo lisilo rasmi kuwa katika nchi hii sema au andika kile kitakacho furahisha watawala tu. Je, hiyo ni sahihi?
 
Na Sammy AwamiBBC News, Dar es Salaam

John Pombe Magufuli
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Rais wa Tanzania John Magufuli amekuwa akikosolewa kwa mashambulizi yake ya mara kwa mara dhidi ya "mabeberu" na tangazo lake la hivi karibuni kuwa maombi na sala vimeondosha virusi vya corona katika taifa hilo.
Lakini suala hilo la kukosolewa huenda lisimsumbue kwa kuwa katika kipindi chake cha miaka mitano ya urais, amekuwa akijipambanua kama mzalendo wa kiafrika na mcha Mungu ambaye yupo kwenye mapambano dhidi ya mataifa ya magharibi ambayo yanataka kupora rasilimali za taifa hilo la Afrika Mashariki.
"Nataka watanzania mjue kuwa mna rais jiwe kweli. Siwezi tishwa na sitishiki," bwana Magufuli alisema Machi 2018.
Magufuli ana matumaini kuwa kazi yake inajieleza na itamsaidia kushinda uchaguzi ujao mwezi Oktoba na kurejea madarakani kwa muhula wa pili.

captionBwana Magufuli amekosoa sana wawekezaji wa nchi za magharibi na China
Moja ya mpambano mkubwa wa rais Magufuli ilikuwa dhidi ya kampuni kubwa ya madini ya Barrick Gold Corp ya nchini Canada.
Alitaka serikali ichukue udhibiti wa 60% katika migodi mitatu ya kampuni hiyo ili kukomesha "unyonywaji" wa rasilimali za Tanzania.
Magufuli mwenye miaka 60 sasa alianzisha majadiliano na Barrick ambayo yalionekana kama mzozo wa ng'ombe na sungura, na ijapokuwa serikali yake ilikubali kuchukua 16% ya hisa, mazungumzo hayo yalitosha kupeleka ujumbe kuwa mambo hayakuwa kama zamani nchini humo.

Akataa mradi wa 'mwendawazimu' na China
Baada ya kuingiwa makubaliano mapya baina ya Barrick na serikali mwezi Januari bosi wa kampuni hiyo Mark Bristow alisema mbele ya rais Magufuli kuwa: " Kilichofanyika hapa ni changamoto kwa sekta ya madini na kwetu sote kuanza safari ambayo tutapata pamoja ama kukosa pamoja."
Akiongea katika hafla hiyo, rais Magufuli hakuonesha tu upande wake wa kizalendo bali ucha Mungu, na kusema: " Namshukuru Mungu kwa mafanikio ya makubaliano haya."

captionBwana Magufuli amehamasisha maombi ya pamoja wakati wa janga la corona
Rais Magufuli pia amesitisha miradi miwili mikubwa baina ya nchi yake na China: ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme ya kati na ujenzi wa bandari kubwa ziadi Afrika Mashariki katika eneo la Bagamoyo kwa gharama za dola bilioni 10.

Magufuli alisema ni "mwendawazimu" tu ndiye angekubali masharti ya mradi huo ambayo yaliingiwa na serikali ya mtangulizi wake Jakaya Kikwete ili kujenga bandari hiyo.
Magufuli pia amekuwa akilaumu ubinafsi wa viongozi na kushindwa kutanguliza maslahi ya taifa kama chanzo cha nchi hiyo kutopiga hatua kubwa kimaendeleo.
Lakini ni mataifa ya magharibi ambayo rais Magufuli amekuwa akiyatilia mashaka zaidi, na amekuwa akiwatuhumu "vibaraka" wa mataifa hayo ndani ya nchi yake - ambao ni mchanganyiko wa wanasiasa wa upinzani, watetezi wa haki za binadamu na waandishi wakosoaji - kwa kupigania maslahi ya "mabeberu".
 
Afrika hakuna kiongozi anayeweza ushindana na mabeberu tunajidanganya tu! Mfano vyombo vyote vya mawasiliano tunavyo tumia ni vyao, macamera yao huko angani yameelekezwa kwetu uchafu wote tunao fanya wanauona wakiamua kuuweka hadharani ni kiongozi gani atakuwa salama?
Wewe labda na genge lako. Tatizo huna maarifa mapana. Ungekuwanayo usinge wababaika mabeberu na kuwaogopa.

Nikupe tu siri ili ujue kwa taarifa yako watengenezaji wa hivyo vitu ulivyo vitaja kwenye hoja yako waafrika wapo na watanzania nao wapo. Kinacho shindikana mpaka hivi sasa ni communication. Viongozi wetu, hata Rais wetu wa sasa, bado hawajatambua umuhimu wa kuwatumia wasomi wetu ipasavyo.

Nimshauri Rais Magufuli awatumie wasomi wetu ipasavyo atakipata anacho kitafuta.
Labda nielezee kidogo hapa ili nieleweke.

Tanzania tumejaliwa madini ya chuma "iron ore" kwa wingi sana kulingana na taarifa ambayo niliipata kutoka kwa Prof. Kabudi akiwa Seattle, lakini cha kusikitisha ni kwamba mpaka sasa tumejipanga kuuza hayo madini badala ya kuwa na mtambo wetu sisi wenyewe wa kufua chuma.

Itakumbukwa kuwa miaka ya 80s mpaka mwishoni mwa 90s wajerumani walikuwa wanaongoza duniani kwa ku Supply chuma, yaani steel. Baada ya hapo mambo yakahamia Asia kwa wachina na wahindi.

Nakumbuka mwanzoni wa 90s Wachina walihamisha viwanda karibu vyote vya kutengeneza chuma na vinu vyake na kupeleka kwao. Kimojawapo kikiwa kiwanda cha Krupp mjini Rheinhause Ujerumani ambacho kilikuwa kinatengeza chuma ya quality babu kubwa. Na ndiyo sababu leo tunayaona maendeleo makubwa kwa wachina.
Hütten- und Bergwerke Rheinhausen – Wikipedia
Kuna watanzani nimekutana nao kwenye makampuni ya uundaji, wana maarifa mengi sana. Ila link kati ya viongozi na hawa wataalam wetu inakosekana.

Rais Magufuli yuko vizuri ila bado anashindwa kidogo nguvu ya kuamua kutumia njia iliyopo ili kuwainua vijana wetu. Achukue tu mkopo wa kutengeneza kiwanda cha kuoka chuma na kusindika gesi asilia atayaona mwenyewe matokeo yake baada ya mda mfupi.

Sisi hatujabahatika kuwa na mafuta, I mean crude oil, kwa hali hiyo sioni kama kuna product ambayo tunaweza uza na kutajirika haraka kama wa Saudis. Chuma yetu itatutoa kwa haraka sana ikiwa katika steel product, kwani kuwa na chuma iliyotengenezwa kuna professionals nyingi sana zitajitokeza kama Metallurgy, smithy, mechanical- na Design engineering. Ku base kwenye civil engineering peke yake sidhani kama kuna mafanikio chanya ya mda mrefu.

Hapa tukitaka kutoka tuna hitaji vijana wenye skil ya ku manipulate chuma na dhahabu zetu kwenye vitu "product creation" na sio ujenzi wa majengo tu ya concrete. Magufuli akiondoka kila kitu kita chaka na kuharibika. Hivi vitu vinapendeza hivi sasa kwasababu msimamizi yuko miaka kumi ijayo baada ya kumaliza muda wake tutarudi kule kule tulio toka. Tunakosa mfumo endelevu. Tunaishi kwa matakwa ya kiongozi aliyopo madarakani.

Tutumie natural resources zetu kupanua maarifa ya vijana wetu ili baadae waweze tengeneza vifaa tofauti vya kurahisisha maisha yao na jamii kwa ujumla kama Naibu waziri wa Afya Dr Mollel alisha wahi sema bungeni.

Tanzania inahitaji wana sayansi zaidi kuliko wapiga porojo na makarani.

Watanzania tukijipanga vizuri twaweza!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hata mimi nimeona hii habari hawa wazungu wameogopa ile hotuba yake ya kufunga bunge zile data zimewanyanya waone hata maana JPM hajaenda kwao sasa wanatumia BBC ambacho ni chombo chao cha propaganda
Yaani Uvccm bhana, tangu lini Mzungu akamuogopa Bush man?
 
Back
Top Bottom