BBC: Shehena ya makombora 1,500 ya Kutungulia ndege aina Strela na Bunduki 100 MG3 zimewasili nchini Ukraine

5525

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
5,412
Reaction score
6,279
Shehena ya makombora 1,500 ya kutungulia ndege aina ya Strela na bunduki 100 za MG3 zimewasili nchini Ukraine kutoka Ujerumani, Shirika la Habari la Ujerumani limewanukuu maafisa wa serikali ya Ukraine wakisema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock alisema Jumatano kwamba vifaa zaidi vya makombora ya Strela vilikuwa vinakwenda Ukraine kufuatia kucheleweshwa kwa uwasilishaji.

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umeifanya Ujerumani kubatilisha sera yake ya kihistoria ya kutopeleka silaha katika maeneo yenye mizozo.

"Sisi ni mmoja wa wasambazaji wakubwa wa silaha katika hali hii, haitufanyi tujivunie lakini ni kile tunachopaswa kufanya ili kuisaidia Ukraine," Reuters ilimnukuu Bi Baerbock akisema.

Makombora ya Strela yalikuwa katika orodha ya jeshi la zamani la Kikomunisti la Ujerumani Mashariki.

BBC.png

277523003_5354045121294982_2203160172104656260_n.jpg
 
View attachment 2165001

View attachment 2165005

Ukrein wanaitaji chakura na madawa ila nato wanawapelekea makombora [emoji16]
 
Ulisoma class moja na mwendazake nini? chakura ni nini hasa, lete hoja wenzako ndio wanaenda kuumizwa zaidi apo, hiyo mizinga 1500 lazima itue kwenye migongo ya warusi

Hawakosi cha kuongea kaka, hawana zuri, nato wakikaa kimya wanaanza sema wamesusa, wakijibu kwa vitendo namna hio wananza maneno tena wao na putin wao wafaa wavalishwe kanga sasa
 
Ukiona hivyo, maji yameshazidi unga!
... kuna uzi humu wa kuonekana Air Force One ikicharaza anga la Ulaya kwa fujo na hatimaye kutua Poland hapo jana. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba soon thereafter anga lote la Ulaya likawekwa under full control na muda mfupi baadaye deployment za kijeshi safu safu zimeonekana zikimiminka kwa fujo Ukraine. Taarifa zaidi zinatonya kwamba hiyo ni baada ya machuma chuma ya kirusi kupigwa full doze nusu kaputi "dawa" ya kisasa kabisa yasijue kinachoendelea.
 
Shehena ya makombora 1,500 ya kutungulia ndege aina ya Strela na bunduki 100 za MG3 zimewasili nchini Ukraine kutoka Ujerumani, Shirika la Habari la Ujerumani limewanukuu maafisa wa serikali ya Ukraine wakisema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock alisema Jumatano kwamba vifaa zaidi vya makombora ya Strela vilikuwa vinakwenda Ukraine kufuatia kucheleweshwa kwa uwasilishaji.

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umeifanya Ujerumani kubatilisha sera yake ya kihistoria ya kutopeleka silaha katika maeneo yenye mizozo.

"Sisi ni mmoja wa wasambazaji wakubwa wa silaha katika hali hii, haitufanyi tujivunie lakini ni kile tunachopaswa kufanya ili kuisaidia Ukraine," Reuters ilimnukuu Bi Baerbock akisema.

Makombora ya Strela yalikuwa katika orodha ya jeshi la zamani la Kikomunisti la Ujerumani Mashariki.

View attachment 2165001

View attachment 2165005
Hawa BBC jau sana habari za Urusi wanatangaza kama msiba, njoo sasa ukute Ukraine kafanya jambo zuri watatangaza siku nzima
 
Back
Top Bottom