BBC Swahili wadai umbali kati ya dunia na jua ni Kilomita 150

BBC Swahili wadai umbali kati ya dunia na jua ni Kilomita 150

Shoctopus

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
3,434
Reaction score
1,985
Assalamualaikum WanaJf.

Siamini kama nilichosikia leo tarehe 01/24/2022 asubuhi ktk 'BBC Swahili' kupitia RFA ilikuwa kweli au nilikuwa kwenye ndoto.

Mtangazaji aitwae R. Oditi amesema umbali kati ya dunia na jua ni kilometers mia na hamsini (150).

Na mbaya zaidi alirudia kusema hivyo mara kadhaa! Na mpaka mwisho wa kipindi chake hewani hakusahihisha usemi wake.

Hivi BBC nayo imeshakuwa radio mbao?
 
Pengine hukusikia vyema au kweli ilikuwa umesinzia.
Huenda walimanisha Million hizo kwenye namba ulizo taja

Rejea:

Umbali kutoka jua hadi dunia
Umbali kutoka kwa jua hadi duniani ni kilomita milioni 150, katika mwanga wa mwaka na hauzidi dakika nane na sekunde moja ya mwanga.

Ikiwa ni gari linalosafiri kwa kilomita 100 kwa saa, na kusafiri bila mapumziko, basi jua linaweza kufikia marudio yake katika miaka 106.

Ikiwa ndege itasafiri kilomita 246,960 kwa saa, kuna uwezekano wa saa 606 au siku 25 kusafiri kutoka duniani hadi Jua.
 
Nimewapigia simu direct ili kuomba ufafanuzi, wamesema, kutoka na muda kuwa mdogo asubuhi, hiyo milioni iliyosahaulika wataimalizia kwenye matangazo ya jioni.

Pls mtoa-mada jaribu kuwa na subira, mambo ni mengi, muda ni kiduchu!
[emoji1]wee Jamaa...
images-516.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwenye mitandao ya FB na website yao, waandishi wana makosa ya kutosha
 
Asante Mkuu! Kumbe na wewe umesikia, nilidhani ni mimi peke yangu.
Bibi-sea mnawaonea bure wale watangazaji! Kutokana na ubobezi wao kwenye tasnia ya habari na mawasiliano, unaweza usitambue baadhi ya maneno because wanaongea lugha professional.

So, maneno mengine, nguli kama hawa huyameza ili kusave muda, kutumia energy kidogo na kuleta mvuto kwenye uwasilishaji wa matangazo yao.

Kwa hiyo, hilo ni jambo la kawaida sana, na ni shock inayotegemewa kwa wasikilizaji wao ambao ni amateurs wasio na experience ya kutosha, kama huyu mleta-mada!
 
Pengine hukusikia vyema au kweli ilikuwa umesinzia.
Huenda walimanisha Million hizo kwenye namba ulizo taja.
Nami nimesikia hivyo hivyo, nikashikwa na bumbuwazi. Ila, akasema kulifikia, (nimesahau usafiri), utatumia miaka kadhaa!
 
Back
Top Bottom