BBC wachakachua uzi wa mwana JamiiForums

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Amani iwe kwenu wakuu

Kuna member wa JamiiForum aitwaye screpa alileta uzi kumhusu msanii dully skys naona leo BBC wamepita nao kiaina

Soma pia: Kwanini Dully Sykes anasema yeye ndiye Mwanzilishi wa Bongofleva?

dully.png
 
Attachments

  • Screenshot_20250118-184429.png
    Screenshot_20250118-184429.png
    438.5 KB · Views: 3
Haya mambo aongee na Watoto wenzake, Mike Mhagama ndio mtunzi wa neno Bongo Fleva Radio one.
Kwani issue ni mwanzilishi wa neno Bongo fleva au mwanzilishi wa muziki wa Bongo Fleva?.
Nikiwa RTD mwaka 1992 nimepiga wimbo wa ICE ICE Baby na OPP wa Saleh Jabir, wakaja kina Ramsey na kikundi Cha Kwanza Unit, cha kina Adili Kumbuka, hata Balozi Dola Soul, 2Proud, na Soggy Doggy walianza zamani, Radio One imeanzishwa 1994!.
P
 
Nikiwa RTD mwaka 1992 nimepiga wimbo wa ICE ICE Baby wa Saleh Jabir, wakaja kina Ramsey na kikundi cha kina Adili Kumbuka, Radio One imeanzishwa 1994!.
P
Mwaka 1992 huyo Abdallah Sykes alikuwa na miaka mingapi?
 
Kwani issue ni mwanzilishi wa neno Bongo fleva au mwanzilishi wa muziki wa Bongo Fleva?.
Nikiwa RTD mwaka 1992 nimepiga wimbo wa ICE ICE Baby na OPP wa Saleh Jabir, wakaja kina Ramsey na kikundi Cha Kwanza Unit, cha kina Adili Kumbuka, hata Balozi Dola Soul, 2Proud, na Soggy Doggy walianza zamani, Radio One imeanzishwa 1994!.
P
Ukiwa RTD nilikuwa Secondary school,
Naelewa vizuri tangu Kim and boys kwenye Yo Rap Bonanza.

Hapa hoja nataka ieleweke kwanza hapakuwa na Bongo Fleva kama jina.

Wakati wa mashindano ya Rap Taifa pale Avalon nilikuwepo hata huyo To Proud hakuwa mshiriki alifanya show tu na single yake ya siku yangu, maana hakuwa na kundi by that time Sugu alikuwa hajajiunga na DPT la kina Dola Soul Balozi.
 
Hadi miaka ya 1990 muziki uliokua unapigwa zaidi na wanamuziki wa kitamzania ilikua ni
Dansi
Taarabu
Muziki wa asili
Na band zilizokua zinagonga copy

Hadi kufika 1993 vinaja wengi wakaanza kujitokeza kufanya muziki kwa kuiga zaidi mahadhi ya muziki wa kimarekani yaani Rap na rnb pamoja na raggae
Na hii ilichagizwa zaidi na Saleh Jabir alipo tembea na beat za ice ice baby na kuweka maneno ya kiswahili

1994 Radio One ikaanzishwa na ikaanza kupiga kwa wingi nyimbo hizo, na hapo ndipo jina rasmi la BONGO FLEVA likazaliwa ndani ya kipindi maarufu enzi hizo kikiwa chini ya Taji Liundi na Mike Muhagama....... hawa ndio waanzilishi wa Jina BONGO FLEVA wakimaanisha muziki wa kitanzania wenye mahadhi ya kimarekani bila kujali kama ni Hip hop au rnb au raggae as long as uliimbwa na watanzania

Hadi kufikia mwishoni ya 90 wasanii wa hip hop hawakupendezwa na jina la Bongo fleva ila waimbaji waliokua wanafuata mahadhi yaki RNB wao walikubaliana na jina hilo na hapo ndio Dully anapoingia

Wana hip hop waliwaona waimbaji kama mabishoo fulani hivi wakati wenyewe ni wagumu flani hivi....... Dully ubishoo hakuuonea aibu aliubeba na kujisifia sana kwa ubishoo lakini sio kwamba yeye ndio muanzilishi wa Bongo fleva

So Baada ya Bongo fleva na hip hop kuanza kutenganishwa kwa upande wa Bongo fleva(waimbaji)Dully alikua kwenye pick yake na alikua anafanya vizuri sana, na ikumbukwe kwamba waimbaji walikua wachache kuliko wana hip hop

Wapo waimbaji walioanza kabla ya Dully kama Unique Sisters, Mr Paul, Krewz Flava na wengine siwakumbuki
 
Wapo waimbaji walioanza kabla ya Dully kama Unique Sisters, Mr Paul na wengine siwakumbuki
👍
 
Kwani issue ni mwanzilishi wa neno Bongo fleva au mwanzilishi wa muziki wa Bongo Fleva?.
Nikiwa RTD mwaka 1992 nimepiga wimbo wa ICE ICE Baby na OPP wa Saleh Jabir, wakaja kina Ramsey na kikundi Cha Kwanza Unit, cha kina Adili Kumbuka, hata Balozi Dola Soul, 2Proud, na Soggy Doggy walianza zamani, Radio One imeanzishwa 1994!.
P
Saleh jabir anastahili ,alifanya huo mziki kitambo tu
 
Kwani issue ni mwanzilishi wa neno Bongo fleva au mwanzilishi wa muziki wa Bongo Fleva?.
Nikiwa RTD mwaka 1992 nimepiga wimbo wa ICE ICE Baby na OPP wa Saleh Jabir, wakaja kina Ramsey na kikundi Cha Kwanza Unit, cha kina Adili Kumbuka, hata Balozi Dola Soul, 2Proud, na Soggy Doggy walianza zamani, Radio One imeanzishwa 1994!.
P
Vijana wa 2000 hawawezi kuelewa hii.
Watakuuliza 2proud ndio nani au Adili ni yupi huyu na Balozi je!
TwoProud na ile shauriTanga.
Walikuwepo HBC.
Mtu hafahamu hata kuhusu Solid ground family atajua nini kuhusu Saleh Jabri?
Gangwe Mobb....
Manduli Mobb
University corner...
Mabaga fresh..
Hivi Mark D yupo?
Mad I've je
 
Kwani issue ni mwanzilishi wa neno Bongo fleva au mwanzilishi wa muziki wa Bongo Fleva?.
Nikiwa RTD mwaka 1992 nimepiga wimbo wa ICE ICE Baby na OPP wa Saleh Jabir, wakaja kina Ramsey na kikundi Cha Kwanza Unit, cha kina Adili Kumbuka, hata Balozi Dola Soul, 2Proud, na Soggy Doggy walianza zamani, Radio One imeanzishwa 1994!.
P
Mzee Pascal shkamoo.
 
Wengi walikuepo
Sasa hivi wako wapi wako wapi
Balozi Bado nipo
Ninapanda kwenye chati kwenye chati
Nashuka Ile Ile
Ile Moja namba nataman

Sijui nani aliimba ila nilikua napenda kusikia hii chorous
 
Back
Top Bottom