Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Ukiwa Boy huwezi kuelewa nimeandija nini.Kwahiyo jina bongo fleva lilianza kabla ya wasanii hawajaanza kuimba bongo fleva?
A Man can understand what i wrote.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukiwa Boy huwezi kuelewa nimeandija nini.Kwahiyo jina bongo fleva lilianza kabla ya wasanii hawajaanza kuimba bongo fleva?
umemalizaHadi miaka ya 1990 muziki uliokua unapigwa zaidi na wanamuziki wa kitamzania ilikua ni
Dansi
Taarabu
Muziki wa asili
Na band zilizokua zinagonga copy
Hadi kufika 1993 vinaja wengi wakaanza kujitokeza kufanya muziki kwa kuiga zaidi mahadhi ya muziki wa kimarekani yaani Rap na rnb pamoja na raggae
Na hii ilichagizwa zaidi na Saleh Jabir alipo tembea na beat za ice ice baby na kuweka maneno ya kiswahili
1994 Radio One ikaanzishwa na ikaanza kupiga kwa wingi nyimbo hizo, na hapo ndipo jina rasmi la BONGO FLEVA likazaliwa ndani ya kipindi maarufu enzi hizo kikiwa chini ya Taji Liundi na Mike Muhagama....... hawa ndio waanzilishi wa Jina BONGO FLEVA wakimaanisha muziki wa kitanzania wenye mahadhi ya kimarekani bila kujali kama ni Hip hop au rnb au raggae as long as uliimbwa na watanzania
Hadi kufikia mwishoni ya 90 wasanii wa hip hop hawakupendezwa na jina la Bongo fleva ila waimbaji waliokua wanafuata mahadhi yaki RNB wao walikubaliana na jina hilo na hapo ndio Dully anapoingia
Wana hip hop waliwaona waimbaji kama mabishoo fulani hivi wakati wenyewe ni wagumu flani hivi....... Dully ubishoo hakuuonea aibu aliubeba na kujisifia sana kwa ubishoo lakini sio kwamba yeye ndio muanzilishi wa Bongo fleva
So Baada ya Bongo fleva na hip hop kuanza kutenganishwa kwa upande wa Bongo fleva(waimbaji)Dully alikua kwenye pick yake na alikua anafanya vizuri sana, na ikumbukwe kwamba waimbaji walikua wachache kuliko wana hip hop
Wapo waimbaji walioanza kabla ya Dully kama Unique Sisters, Mr Paul, Krewz Flava na wengine siwakumbuki
Dully Syjes hata siku za "Yo Rap Bonanza" ya Kim Mgomelo alikuwa hayupo.Dar young mob,wagume weusi asilia,mac muga,nigaz 2 public,deplomatz, kwanza unit, mawingu band list nyingine nmesahau hapo dully bado sana
Ova
Acha hizo Pas. Na wewe unataka kuwa kama Le Mutuz? 🙂Tafuta $5000 nikupatie working visa ya US.
P
Kaimba BaloziWengi walikuepo
Sasa hivi wako wapi wako wapi
Balozi Bado nipo
Ninapanda kwenye chati kwenye chati
Nashuka Ile Ile
Ile Moja namba nataman
Sijui nani aliimba ila nilikua napenda kusikia hii chorous
Mkuu Kiranga , umenikumbusha mbali!. Mimi ndio nilikuwa MC wa Yo Rap Bonanza ya DJ Kim!. Coincidently leo nikiwa joint fulani hapa Dodoma, nikakutana na mtoto wa DJ Kim anaitwa Kareem.Dully Syjes hata siku za "Yo Rap Bonanza" ya Kim Mgomelo alikuwa hayupo.
Tumeqnzisha hili game. Too Proud anaingia mjini na kukaribishwa na Dar Young Mob tunamuona.
Naam.Mkuu Kiranga , umenikumbusha mbali!. Mimi ndio nilikuwa MC wa Yo Rap Bonanza ya DJ Kim!. Coincidently leo nikiwa joint fulani hapa Dodoma, nikakutana na mtoto wa DJ Kim anaitwa Kareem.
Sponsor wa Yo Rap Bonanza, alikuwa Alex Massawe mzee wa AM investment.
P
TrueNaam.
Haya majina wanayajua watu fulani waliokuwapo siku fulani hivi Dar.
Bongoyo mtaa wa wazee wa Eagle!.Ile Yo! Rap Bonanza ndiyo ilikuwa mashindano ya mwanzoni kabisa ya hip hop /rap Tanzania ukiacha yale yaliyokuwa yanafanyika Lang'ata akashinda Fresh XE Eddo Mtui wa Oysterbay kwao pale kona ya Mkwawa na Bongoyo opposote na kwa Jaji Lubuva pale.
Hell do something.Yule dogo mtoto wa Kim kuna siku niligusia stories za baba yake alikuwapo hapa JF alifurahi sana, inaonekana Kim alifariki wakati yeye alikuwa mdogo sana hakupata kumjua baba yake.
Alikuwa natafuta sana stories za watu waliokuwapo siku zile. Kuna documents /videos anazo anaandaa kitu kama kitabu au documentary ya historia ya "Yo! Rap Bonanza".
Lile jengo next to nyumbani kwao, ile floor ya chini yote ndio ilikuwa ofisi ya PPR, kodi tuu ya pango NHC ni TZS. 3.5 per month, wakati mshahara wa DC ni 3.M halafu kuna majinga humu yakasema natafuta u DC!.Kim alikuwa Article Don. Nilikuwa namfuata nyumbani kwake pale City Centre nyuma ya Billicanas, tulikuwa tunapanga naye mikakati ya mashindano, mtu mmoja very cool anajua ku deal na watu wa kika aina vizuri kuliko maelezo.
Mimi na Kim tumejuana akiwa DJ pale hotel next to Tanganyika Meat, siu unajua tena ujana, nimetua mahali kumbe mali za DJ Kim, ma DJ wanapendwa tuu lakini hawana chapaa! sawa na sisi watangazaji wa RTD ile enzi za redio moja!.Maana yale mashindano yalijumuisha watoto wa mjini wote kuanzia wale ma summer boys wa IST kule Masaki na kina Raiders Posse/ Kwanza Unit, mpaka watoto wa Temeke kina GWM na Dar Young Mobb, na kina Ras Pompidou kutoka Chamazi huko, vichwa ngumu wote wa Dar walikuwapo halafu Kim akawatuliza wakae pamoja kwenye competition bila fujo.
Ilikuwa poa sana.
Naam shekheKwani issue ni mwanzilishi wa neno Bongo fleva au mwanzilishi wa muziki wa Bongo Fleva?.
Nikiwa RTD mwaka 1992 nimepiga wimbo wa ICE ICE Baby na OPP wa Saleh Jabir, wakaja kina Ramsey na kikundi Cha Kwanza Unit, cha kina Adili Kumbuka, hata Balozi Dola Soul, 2Proud, na Soggy Doggy walianza zamani, Radio One imeanzishwa 1994!.
P
Pasco Kamuacha y thang on purpsose because yumo humuNaam.
Haya majina wanayajua watu fulani waliokuwapo siku fulani hivi Dar.
Ile Yo! Rap Bonanza ndiyo ilikuwa mashindano ya mwanzoni kabisa ya hip hop /rap Tanzania ukiacha yale yaliyokuwa yanafanyika Lang'ata akashinda Fresh XE Eddo Mtui wa Oysterbay kwao pale kona ya Mkwawa na Bongoyo opposote na kwa Jaji Lubuva pale.
Yule dogo mtoto wa Kim kuna siku niligusia stories za baba yake alikuwapo hapa JF alifurahi sana, inaonekana Kim alifariki wakati yeye alikuwa mdogo sana hakupata kumjua baba yake.
Alikuwa natafuta sana stories za watu waliokuwapo siku zile. Kuna documents /videos anazo anaandaa kitu kama kitabu au documentary ya historia ya "Yo! Rap Bonanza".
Kim alikuwa Article Don. Nilikuwa namfuata nyumbani kwake pale City Centre nyuma ya Billicanas, tulikuwa tunapanga naye mikakati ya mashindano, mtu mmoja very cool anajua ku deal na watu wa kika aina vizuri kuliko maelezo.
Maana yale mashindano yalijumuisha watoto wa mjini wote kuanzia wale ma summer boys wa IST kule Masaki na kina Raiders Posse/ Kwanza Unit, mpaka watoto wa Temeke kina GWM na Dar Young Mobb, na kina Ras Pompidou kutoka Chamazi huko, vichwa ngumu wote wa Dar walikuwapo halafu Kim akawatuliza wakae pamoja kwenye competition bila fujo.
Ilikuwa poa sana.
Y-Thang Mnyamwezi wangu akianza kulitema ng'eng'e unaweza kufikiri huyu ni mtoto wa Colin Powell kashuka sasa hivi kutoka Bronx au Brooklyn hata joto la Dar hajalizoea tumtafutie sehemu yenye AC.Pasco Kamuacha y thang on purpsose because yumo humu
Out of contentY-Thang Mnyamwezi wangu akianza kulitema ng'eng'e unaweza kufikiri huyu ni mtoto wa Colin Powell kashuka sasa hivi kutoka Bronx au Brooklyn hata joto la Dar hajalizoea tumtafutie sehemu yenye AC.
Y-Thang alikioatia kiingerwza cha Wamarekani mpaka ikawa vigumu kumtofautisha nao.
Alikuwa A level mimi nipo O level Tambaza, basi kila mara akipenda kuniongelesha mambo ya unyamwezini, mambo ya ndoto zake za kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, akinionesha vitabu alivyokuwa anasoma. Kuna siku alikuwa anasoma kitabu kinaitwa "Gifted Hands" cha huyu top surgeon mweusi aliyekuwa Hopkins, Dr. Ben Carson.
Y-Thang akawa ananielezea huyu ni daktari bingwa anaheshimiwa sana Marekani, ila kazaliwa ghetto tu huko Baltimore Maryland USA, kasoma mpaka kawa bingwa kabisa. Ndiyo nikamjua Ben Carson hapo early 1990s Y-Thang yupo PCB Tambaza.
Siku hizi vijana wanajiongeza hivyo kusoma nje ya mitaala?
Hahaa. Mambo ya kawaida tu mkuu, mimi nilikuwa nasoma sana vitabu na magazeti.Out of content
braza Kiranga ww ulisomea combi gani hapo tambaza na chuo ulisomea wapi,course gani maana una madini siyo ya nchi hii.
Sawa sawaDar young mob,wagume weusi asilia,mac muga,nigaz 2 public,deplomatz, kwanza unit, mawingu band list nyingine nmesahau hapo dully bado sana
Ova
Hahahaha,ankal umeanza lini hizo mambo ya kutaafutia watu visa ya US?Tafuta $5000 nikupatie working visa ya US.
P
To proud au sugu nae katoa mchango mkubwa ktk huu mzikiMkuu Kiranga , umenikumbusha mbali!. Mimi ndio nilikuwa MC wa Yo Rap Bonanza ya DJ Kim!. Coincidently leo nikiwa joint fulani hapa Dodoma, nikakutana na mtoto wa DJ Kim anaitwa Kareem.
Sponsor wa Yo Rap Bonanza, alikuwa Alex Massawe mzee wa AM investment.
P